Tukizubaa tutaanza kuabudu kanisani na misikitini huku tumezingirwa na polisi

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Watanzania tuamke tafadhali na tumkatalie Magufuli utaratibu wake mbovu wa kuongoza nchi.

Ameanza kuzuia mikusanyiko ya kisiasa kwa hofu tu kwamba watu watasema mabaya yake akiwa Waziri na mabaya yake mengi zaidi katika kipindi cha miezi 6 akiwa Rais...sauti za kumpinga na kumkosoa muda si mrefu ujao zitaanza kusikika kutoka katika nyumba za Ibada - vile asivopenda kusemwa, hakika Magufuli ataagiza polisi wake wazingire Makanisa na misikiti zinakosikika sauti za wakosoaji, na pia ataagiza nyumba za kuishi za viongozi wa kiroho pia zizingirwe na polisi na kwamba viongozi hao wakamatwe na kufunguliwa mashtaka, kama ilivyotokea kwa Askofu Gwajima.

Sasa mimi nasema miaka mi-5 ya kuishi katika vurugu hizi za Magufuli ni madhila makubwa mno, tumkatalie ili yumkini akipenda ajirekebishe, asiposikia basi,Mungu yupo na ndiye Mkuu kuzidi watawala wote!
 
Tuamuke mara ngapi? tulishaamuka ndo maana hatutaki maandamano ya kilofa,huu muda sio muafaka kwa kufanya maigizo kwenye barabara za serikali kama unataka kuandamana,kaandamane kwenye viunga vya chama chako na si public areas,HAPA KAZI TU
 
Pale Mwembechai ilikuwa balaa, sasa sijui kwa Magufuli itakuwaje manake Sheikh Ponda bado hajaanza shughuli na mtiti wake ni balaa. Ngoja tusubiri tuone itakuwaje.
 
Wewe Ni mchochezi Na sio mzalendo ulaaniwe, mnataka mfanyiwe jema lipi kila Mara Ni kukosoa tuu, Na utawala umeingia madarakani Mda c mrefu
 
'Rais wetu mpendwa,chaguo la Mungu,anajua anachokifanya'
'msilete usumbufu tafadhali'

Hahaaaaa
 
Pale Mwembechai ilikuwa balaa, sasa sijui kwa Magufuli itakuwaje manake Sheikh Ponda bado hajaanza shughuli na mtiti wake ni balaa. Ngoja tusubiri tuone itakuwaje.
Yaani we unafurahia ponda anapokaaga gerezani wakati we unakula bata uraiani. Awamu hii imekula kwenu.
Zamu ya kina Mbowe kwenda gerezani ikiwa watakaidi kutii sheria bila shuruti.
 
Tuamuke mara ngapi? tulishaamuka ndo maana hatutaki maandamano ya kilofa,huu muda sio muafaka kwa kufanya maigizo kwenye barabara za serikali kama unataka kuandamana,kaandamane kwenye viunga vya chama chako na si public areas,HAPA KAZI TU
Watu wameandamana ndani ya ukumbi wa mahafali ?
 
Basi Wewe mtoa mada hujui mipaka ya nin vizungumzwe kwe majengo ya ibada ,,,

Kwenye majengo ya ibada siyo mahala pa siasa watu huenda kwa masuala ya ROHONI

SEMA MAKANISANI SASA HV HAKUNA DISPLINI YA ROHO KWA SABABU WATU WAPO WANAJIWEKA WENYEWE TU KWA AJILI TUMBO
 
Yaani we unafurahia ponda anapokaaga gerezani wakati we unakula bata uraiani. Awamu hii imekula kwenu.
Zamu ya kina Mbowe kwenda gerezani ikiwa watakaidi kutii sheria bila shuruti.
Hapana mie huwa napenda sana mahubiri ya Ponda. Na jinsi viongozi wanavyojisahau na kuingiza siasa kwenye nyumba za ibada. Atapoanza watu wasije lalamika.
 
Serkali ya China wanayadhibit sana makanisa kwa kuingza mifumo yao ya utawala, na hapa napo ndo tunakoelekea na hasa kwasasa wachina ndo wajanja wetu
 
Tuamuke mara ngapi? tulishaamuka ndo maana hatutaki maandamano ya kilofa,huu muda sio muafaka kwa kufanya maigizo kwenye barabara za serikali kama unataka kuandamana,kaandamane kwenye viunga vya chama chako na si public areas,HAPA KAZI TU
Nadhani kauli mbiu sawia ingekuwa HAPA NI UDIKTETA TU.
 
Itafika mahala kila sala au kila ibada tunaenda kuombea kibali polisi.
Hayo yanakuja muda si mrefu. Katika historia ya nchi, kwa mara ya kwanza, tena ni katika utawala huu watu wanaambiwa ili kuadhimisha sherehe ya kuhitimu masomo yao kama siyo wana-CCM ni lazima wapate kibali cha polisi.

Utawala huu wa kibabe, sitashangaa kama hata kufanya sherehe za arusi, kama wewe si mwanaCCM, utatakiwa upate kibali cha polisi.

Ni utawala unaoamini kuwa polisi ndiyo suluhisho la kila kitu!
 
mnaingilia mamlaka iliyowekwa duniani na mungu,Rais wetu ni mzuri sana na mwema,acheni uvunjifu wa amani
Tusidanganyane, siyo kila utawala hutoka kwa Mungu. Tawala nyingine huwa ni adhabu kwa wanadamu waliomkosea Mungu. Hitler aliyewaua Waisrael milioni 2 ulikuwa ni utawaka toka kwa Mungu? Utawala wa Amin ulioua vilema kwa kwenda kuwatumbukiza ziwa Victoria, ulitoka kwa Mungu? Mti mzuri hutambulika kwa matunda yake mazuri, na utawala uliotoka kwa Mungu hutambulika kwa matendo mazuri kwa watu wake.

Mimi sina uhakika kama utawala huu umetoka kwa Mungu au hapana, lakini nijuacho ni kwamba Mungu ameruhusu uwepo kwa makusudi ayajuayo mwenyewe. Kama ni utawala wenye baraka za Mungu au la, tutaupima kwa matendo yake.
 
Back
Top Bottom