Tukiwa wa kweli,tutavuka salama

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
TUKIWA WAKWELI TUTAFIKA SALAMA

Januari 14,2019 Mahakama ilitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na vyama vya upinzani kupinga muswada wa sheria ya marekebisho ya vyama vya siasa mwaka 2018.

Muswada huo unaopingwa na vyama hivyo ulisomwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba 16 ,2019 unaonekana kupingwa kila kona na vyama hivyo.

Kuupinga muswada sio hoja, hoja ni sababu zinazotumiwa na wapinzani kuhalalisha upingaji wao.Lakini tatizo lingine ni kuupinga muswada wote kana kwamba haujabeba hata jambo moja la maana.

Makala haya yana lengo la kuelezea kwa kifupi vifungu vinavyopingwa,faida za muswada huo,maoni ya wapinzani na imani za vyama vya upinzani kwa taasisi za kimaamuzi zilipo nchini.

HISTORIA YA MUSWADA HUU

.Mchakato wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa ulianza mwaka 2013.Baadaye ukashindikana kuendelea kutokana na mwaka 2014 kulikua na mchakato wa katiba mpya na mwaka unaoufuata (2015) uchaguzi mkuu.Sababu hizi mbili kubwa zikasababisha kusimama kwa mchakato wa kukusanya maoni kwa ajili ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa.

Na bango kitita la maoni lilisaanza kuandaliwa mwaka huo wakati wa kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere.

Katika kongamano hilo wawasilishaji walikua Profesa Benadeta Killian na aliyekua mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa wakati huo marehemu Peter Kuga Mziray.

Mei 2014 lilifanyika baraza la vyama vya siasa katika ukumbi wa New Afrika Hotel lenye lengo la kukusanya maoni kwa ajili ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa ambapo polisi pia walishirikishwa kutoa maoni yao.

Kipindi chote hiko cha Chantal huu (2013-2014) rais wa sasa alikua ni waziri wa Ujenzi na miuondo mbinu.Na inawezekana kabisa hata ndoto za urais hakua nazo wakati huo.

Wapingaji wanatumia kitendo cha kusomwa kwa muswada huo wakati wa utawala wa Magufuli kama hoja ya kumuhusisha rais wa sasa na muswadq huo.Ukweli ni kwamba mchakato wa muswada huo ulianza kipindi cha utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete.

Muswada huo uliosomwa kwa mara ya kwanza bungeni ijumaa Novemba, 2018 ni sehemu ya maoni yalioanza kukusanywa na kutolewa tangu mwaka 2013 Magufuli akiwa waziri.Hivyo kumhusisha nao sio sahihi.

VIFUNGU VINAVYIPIGIWA KELELE NA WAPINGAJI.

Vifungu vinavyolalamikiwa na na wanaopinga muswada huu ni vifngu vya 5A & B6,12,19,20,22,23,24 na32.

Kimsingi vifungu hivi vinazungumzia mambo kadhaa ikiwemo marufuku ya kurejesha chama kilichofutwa,kukifuta chama cha siasa.

Mengine ni uratibu wa elimu kwa umma,maamuzi ya msajili kutohojiwa,zuio la ruzuku,uwezo wa msajili kumuagiza mkaguzi mkuu wa serikali kukagua hesabu za vyama.

Aidha pia msajili kumsimamisha mwanachama yeyote wa chama cha siasa,zuio la misaada ya fedha kwa vyama vya siasa toka nje ya nchi.

MAONI RASMI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

Kwenye maoni hayo ya Chadema kifungu kidogo 3.5 wanasema "Itakua ni jukumu la serikali kutoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu ili kujiendesha"

Hawataki kusema ruzuku hii ambayo ni pesa za watanzania zitakaguliwaje,ikionekana zimetumika hovyo hatua gani zichukuliwe wala hawatengenezi ulazima wa kisheria vyama hivi kukaguliwa matumizi ya fedhq hizi za ruzuku.

Chama kinachotoa maoni haya ndicho kinachoongoza kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ruzuku toka kwa wanachama wake .

Ikumbukwe huko nyuma waliokua wanachama wa chama hiko kadhaa walifukuzwa ama kuondoka baada ya kuhoji matumizi ya ruzuku ndani ya chama.

Nilifikiri Chadema ingekua ya kwanza kuukubali muswada huu ili iweze kuwathibitishia wanachama wake ukweli juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya ruzuku,badala yake kimekua chama cha kwanza kuupinga muswada huu unaoruhusu msajili ukaguzi na adhabu kwa vyama vitakavyotumia vibaya ruzuku ya serikali.

Kupinga muswada huu kwa chadema kunathibitisha hofu waliyokua nayo kwa Zitto Zuberi Kabwe wakati akiwa mwenyzkiti wa PAC alipokitaka chama hiko kuwasilisha taarifa zake za fedha kwq ajili ya ukaguzi.

Kuupinga muswada huo unaotoa nafasi kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuvikagua vyama hivyo unathibitisha maneno ya Mwita Waitara,Juliana Shonza,Mtela Mwampamba na wengine walipiga kelele kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku kwa chama hiko.

JE MUSWADA HUU UNA TIBA YOYOTE KWA VYAMA VYA SIASA ?

Ndio hasa kwa vyama vya upinzani.Mfano kuna vyama vya upinzani vinatawaliwa kufalme na kisultani.

Vina viongozi waliodumu kwenye vyama hivyo kwa zaidi ya miaka 10-20 na inaonekana inahitajika nguvu toka nje ya vyama hivyo kuweka mambo sawa.

Kifungu cha 21 E kinatoa tiba ya tatizo hili kwa kumruhsu msajili kumsimamisha mwanachama wa chama chpchote kwa muda.

Sio siri kuna baadhi ya katiba za vyama vya siasa zimezidiwa uzito na viongozi wa vyama hivyo.Mwaka 2006 Chadema walifanya mabadiliko ya katiba kuondoa ukomo wa muda kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hiko.

Haitaji elimu kubwa kung'amua kua mabadiliko hayo yalikua na lengo la kumuongeze muda Freeman Mbowe katika nafasi hiyo.Uwepo wa kifungu kama hiki katika sheria hii kutapunguza nguvu za "miungu watu" waliopo ndani ya vyama vya upinzani waliojuu ya katiba za vyama hivyo.

Kifungu cha 39 kinahusu vikundi vya ulinzi vya vyama vya siasa kama Red Brigade cha Chadema na Green Guard cha CCM na vinginevyo.

Kumekuwapo na malalamiko ya mara kwa mara hasa nyakati za chaguzi mbalimbali kuhusu vikundi hivi vya vyama kuhusika na vurugu.

Mathalani mwaka 2013 wakati wa marudio ya uchaguzi mkoani Iringa ,chama cha demokrasia na maendeleo kililalamika kua aliyekua mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wakati huo Jesca Mpangatazanga kwa kutumia Green Guard alimteka na kumfanyia vurugu mbunge wa viti maalumu wa chama hilo Bi Rose Kamili.

Ukiacha hilo la Iringa yapo matukio mengi tu ambayo vyama vya upinzani vilalamika na kuhusisha uwepo wa Green Guard ikiwemo Igunga mwaka 2011 na maeneo mengine.

Kwa nini sasa upinzani hautaki kuondolewa ama kudhibitiwa kwa vikundi hivi walivyovilalamikia?Je wanataka iaminike vilio vyao vya siku za nyuma vilibeba mkakati wa kisiasa kutafuta kura za huruma?

CCM INATAKA KUUA VYAMA VYA UPINZANI?

Serikali ya iliyopo madarakani inaoongozwa na chama cha mapinduzi tangu mwaka 1977 ilipozaliwa ccm ndani ya ndoa ya ASP na TANU.

Tusisahu kuwa hata mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulivyoruhusiwa nchi ilikua inaongozwa na CCM.Chama kilichoruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka huo ndio hiki hiki kilicholeta muswada wa mrekebisho kwa nini baadhi waseme tunarudi kwenye mfumo wa chama kimoja?.

Kwa maoni yangu sioni sababu ya kufanya propaganda kwenye mchakato huu.Ni vyema tuoneshwe udhaifu wa muswada lakini pia vipengele vinavyofaa vizungumzwe kwa ukubwa na upana ule ule wa vipengele vingine ili kuutendea haki muswada huo

Sheria ya zamani inasema mtu akifanya makosa iwe makubwa au madogo katika chama basi chama hiko kifutwe,lakini muswada wa sasa umetoa adhabu ndogo ya kumsimamisha kwa muda kutojihusisha na shughuli za siasa ama kulipa faini kama vyama hivi havitakiwi mabadiliko haya yasingekua hivi.

JE HATA VYOMBO VINAVYODAIWA KUA HURU WAPINZANI WANA KAWAIDA YA KUTOVITUHUMU?

Mfano kwenye mapendekezo rasmi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kifungu cha 2.1 wanasema kutakua na ofisi ya msajili itakayokua huru na kujitegemea pamoja na fedha za kujitegemea

Na hili ndio tatizo la msingi.Hoja sio ubovu wa muswada hoja ni mchakato wa upatikanaji wa msajili wa vyama .

Wapingaji hawataki kusema hofu yao juu ya muswada huu unatokana na msajili wa vyama kua na vinasaba na rais.Hivyo kwao kama msajili angepatikana kwa mchakato mwingine nje ya kuteuliwa na rais wasingekua na muswada huu.Hii ni hoja iliyojificha ndani ya kinachoitwa uhuru wa msajili.

Lakini tukumbuke zipo taasisi za kimaamuzi nyingi tu ambazo watendaji wake wanapatikana katika mchakato huru na zimewahi kutoa maamuzi kwa vyama hivi hivi vya upinzani na uamuzi huo pia hakuaminika.

Mathlani muda huu Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema yupo mahabusu baada ya kunyimwa dhamana na mahakama kwa kitendo cha kudharau taasisi hiyo.

Kila mmoja nafahamu upatikanaji wa mahakimu,na wengi tunafahamu uhuru na kinga walizonazo majaji na mahakimu na inatambulika pia mhimili huo wa mahakama ulivyo na Uhuru uliokamilika.

Pamoja na uhuru huo wa mahakama lipo kundi kubwa tu la wafuasi na viongozi wa chadema lenye kuamini haki haikutendeka kwa mwenyekiti huyo.

Mitazamo hii ya kutoafiki kwa adhabu za mahakama imewahi pia kutokea kwenye kesi za Godbless Lema Arusha,Joseph Mbilinyi Mbeya na Peter Lijua likakali wa Morogoro.

Kama hata taasisi zilizo huru na zisizofungamana na masuala ya kisiasa zinapotoa maamuzi bado zinalalamikiwa na uhuru wa aina gani ambao msajili akipewa vyama hivi havitolalamikia?Bungeni tunaweza kushawishika labda kwakua mchakato wa kumpata spika ni wa kisiasa na anatokana na chama cha siasa,vipi kuhusu majaji na mahakimu wetu?

HITIMISHO

Ndio inawezekana kabisa muswada huu ukawa na kosoro kwa sababu umetungwa na binadamu wasiokamilika.Lakini na wapingaji wajijue pia na wao sio malaika wana udhaifu ule ule walionao waliotunga hivyo wasilazimishe mawazo yao yaonekane ya maana zaidi pasipo kuacha nafasi ya kukosolewa.

Haiwezekani muswada wote ukawa hauna jambo la maana.Ni vizuri sana wakati tunataja vifungu vibovu tukataja pia vilivyo bora ili kuwapa nafasi wananchi wa kawaida kuchuja pumba na mchele.

Upinzani uanze kuaminika upunguze kupinga kila kitu ili wakati mwingine wanapokua na hoja za msingi upate uungwaji mkono.Vinginevyo inaonekana ni kasumba yao ya miaka yote kama walivyopinga vita vya mashoga,ununuzi wa ndege,ujenzi wa mradi wa umeme Strigles Gorge na mengine

TUKIWA WAKWELI TUTAFIKA SALAMA

NA NOEL NGUZO

Upinzani uanze kuaminika upunguze kupinga kila kitu ili wakati mwingine wanapokua na hoja za msingi upate uungwaji mkono.Vinginevyo inaonekana ni kasumba yao ya miaka yote kama walivyopinga vita vya mashoga,ununuzi wa ndege,ujenzi wa mradi wa umeme Strigles Gorge na mengine.

Noel Nguzo.R.
 
Back
Top Bottom