Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi, ijui FireChat chat bila internet connection

Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi, ijui FireChat chat bila internet connection

Kang

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2008
Posts
5,701
Reaction score
2,613
Link: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.opengarden.firechat

FireChat ni application ya chat mithili ya WhatsApp au FB Messenger.
Tofauti kubwa ya Firechat ni kwamba inakuruhusu kuchat na watu hata kukiwa hakuna mtandao wa simu wala wifi/3g.

App hii ilipata umaarufu katika maandamano ya Occupy Wallstreet USA ambapo iliwawezesha waandamanaji kuwasiliana hata pale mitandao ya simu ilipokuwa haifanyi kazi kitu ambacho wengi wanadai kilifanywa na Polisi.

20a8f8m.jpg


Firechat inaweza kufanya hilo kwa kutengeneza network moja kwa moja baina ya simu za watu kwa kutumia bluetooth na peer to peer wifi. Pia kama mtu unayechat nae hayupo kwa hiyo network msg za firechat zinahifadhiwa katika simu za watumiaji wake na kutumwa pale mhusika anapopatikana.

So kwa mfano John anataka kumtumia Msg Bob lakini Bob hayupo katika range ya Bluetooth au Wifi.
Basi hiyo Msg inaweza kupokelewa na Neema, Bakari na Ally na mmoja wao akifika karibu na bob basi Bob atapokea ujumbe wake au mmoja wao akipata internet connection basi ujumbe wa Bob utatumwa kwa kutumia Internet!

Msg inapoenda kwa mfumo huu inakuwa encrypted kiasi kwamba Bob peke yake ndo atakuwa na uwezo wa kuisoma hiyo Msg.

Na pia kwa utaratibu huu jinsi watu wengi zaidi wanavyokuwa na FireChat App ndo msg zinafika kwa urahisi zaidi.
 
ila kwetu mwamko mdogo na hata adapter zetu ni dhaifu sababu wengi tunatumia simu za kichina ambao hata hawahangaiki kueka powerfull wifi adapter. labda watngaze kitu kama hichi kwenye kila mkutano wa campaign ndio inaweza fanikiwa.
 
Back
Top Bottom