Tukiwa kwenye kufunga tuheshimu pia na wasiofunga

Pesanyingi

JF-Expert Member
Apr 15, 2023
397
662
Kufunga ni Imani, hivi kuna haja ya kujitangaza kuwa umefunga kwa kila mtu hadi kuwa kero kwa wengine,na wakati mwingine kuleta tafrani kwa wasiofunga kwa kuwazuwia wasile.

Kuna baadhi ya watu siyo wote wanakosa ustaarabu akifunga ye anakuwa kero kwa wengine.

Na wakati mwingine tusiofunga inabidi tujifiche vichakani tukila na kunywa kusubiri usiku ufike tujumuike wote kula nao tena.

Hili lipo sana kwenye kabila letu nisingependa kutaja ila mwenye kabila kama langu anaelewa, sijajuwa makabila mengine wakifunga wanakuwa wababe kama sisi.
 
We kula bn usiwabughusi na wasikubughusi.....sisi huku kijijini tunakula miwa na Wala hawatusumbui
 
Funga ni Imani...na watu hukumbushana wenyewe kwa wenyewe hakuna mtu anayemlazimisha mwingine afunge isipokuwa dini imehimiza watu wakumbushane...Sasa wewe kero sijajua unaipataje hapo?
 
Funga ni ibada mwisho wa siku Mungu ndio anajua mtu kafunga au laah , kingine ni ukumbusho binafsi hapa nilipo hakuna aliyefunga ila kama angekuwepo ,ningekuwa nakula kwa kujificha.

Tuheshimu ibada za mtu hata matangazo yanatolewa kweny sehemu za jumuiya kwamba watu fulani wamefunga ....Kikubwa unaweza kumsapot mtu indirectly kwa kuheshimu kama kafunga kutokana na imani yake.
 
sijajua kwa imani nyingine ila maelekezo ya kitabu changu mtu akifunga hatakiwa kua kama mfarisayo anaetaka aonekane kufunga ni siri kubwa unaweza ukaja kwangu ukapikiwa ukala ukanywa na juice na usijue kama nyumba nzima tumefunga au naweza nikakuspoil na biryan la mariam wa tabata vijijini uku tukipiga story na usijue kwamba nimefunga maana kufunga ni vita yangu binafsi kupambana na vitu vya mwilini natakiwa nizishinde hizo tamaa sio nijifiche nisikutane nazo
 
Kufunga ni Imani, hivi kuna haja ya kujitangaza kuwa umefunga kwa kila mtu hadi kuwa kero kwa wengine,na wakati mwingine kuleta tafrani kwa wasiofunga kwa kuwazuwia wasile.

Kuna baadhi ya watu siyo wote wanakosa ustaarabu akifunga ye anakuwa kero kwa wengine.

Na wakati mwingine tusiofunga inabidi tujifiche vichakani tukila na kunywa kusubiri usiku ufike tujumuike wote kula nao tena.

Hili lipo sana kwenye kabila letu nisingependa kutaja ila mwenye kabila kama langu anaelewa, sijajuwa makabila mengine wakifunga wanakuwa wababe kama sisi.

Mt 6:16 SUV​

Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
 
Funga ni ibada mwisho wa siku Mungu ndio anajua mtu kafunga au laah , kingine ni ukumbusho binafsi hapa nilipo hakuna aliyefunga ila kama angekuwepo ,ningekuwa nakula kwa kujificha.

Tuheshimu ibada za mtu hata matangazo yanatolewa kweny sehemu za jumuiya kwamba watu fulani wamefunga ....Kikubwa unaweza kumsapot mtu indirectly kwa kuheshimu kama kafunga kutokana na imani yake.
Mbona Kwaresma imeanza wiki ya pili hii, sijaona bandiko kama hili, kunani?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Dah kama vile uneniwahi hivi. Yaan hapa ndo nmetoka kukereka na hii tabia. Kuna jirani anadai kafunga,,,sasa kila akipita hapa ofisini kwangu ni kujitangazaaa,,,Watu wengine sijui wafundishwe vipi hadi waelewe maana halisi ya funga.
 
Back
Top Bottom