SoC03 Kilimo chenye kuleta faida kwa mkulima na Taifa

Stories of Change - 2023 Competition

fortu255

Member
Jan 20, 2020
37
37
Moja wapo ya mahitaj makuu ya mwanadamu ni chakula, Kilimo ni mojawapo ya shughuli za mwanadamu zinazomsaidia kupata mazao ya chakula na biashara yanayomuingizia kipata kwa ajili ya maisha yake na kukuza uchumi wa nchi yetu.

Andiko langu limejikita katika wilaya ya MAGU katika mkoa wa MWANZA ambapo asilimia kubwa ya watu wa magu wanalima kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia vyanzo vya maji kama mto simiyu,mto matu na mto gangara japo kua hua inakauka pia kwa wakati mwingine na mazao yao makuu ni mpunga,mahind,dengu,choroko na mbogamboga. Kama tujuavyo kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu hivyo bas serikali haina budi kuwekeza katika kilimo chenye tija kwa kuwawezesha wakulima ili kupata faida katika kilimo chao bas serikali inalo jukumu la kushirikiana na wakulima katika vitu vifuatavyo.

1: Kuwapa mafunzo wakulima kuhusu utunzaji na uendelezaji wa vya vyanzo vya maji pamoja na kuwaunganisha na watabir wa hali ya hewa ili kulima kwa uhakika pasipo kua na hofu ya mazao yao kuharibika.

2: Kuwaunganisha wakulima na Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na kilimo pamoja na zinazotoa mikopo ili kumsaidia mkulima kulima kwa uhakika zaidi na pia kupata ushauri wa kanuni bora za kilimo cha mazao na udhibiti wa wadudu waharibufu wa mazao.

3: Kuanzisha na kusimamia vyama vya ushirika kwa weledi zaid hii itawasaidia katika kushirikiana kwenye kilimo chao na kupata misaada pale wanapokwama au wanapopata changamoto katika kilimo.

4: Kuwapa wakulima elimi ya kutunza takwimu za gharama walizotumia katika kilimo chao ili wahakikishe wanalima kwa faida na sio hasara.

5. Kupata taarifa sahihi ya hali ya hewa kwa maana kwamba kuna baadhi ya mazao yanahitaji mvua nyingi na mazao mengine hayahita mvua nyingi hvyo bas ukosefu wa taarifa sahuhi ya hali ya hewa ni miongon mwa changamoto zinazosababisha wakulima kuvuna mazao kidogo sababu wanalima bila kujua kiwango cha mvua kwa msimu husika.


HITIMISHO.
Kilimo kinachukua sehemu muhimu katika kukua kwa uchumi na kupunguza umaskini,Hata hivyo, kuna vikwazo vya aina mbalimbali mfano, pembejeo zisizotosheleza kama vile mbegu bora, mbolea na dawa za kilimo, mfumo wa kizamani wa uoteshaji mazao bila kupata ushaur kwa wataalam pamoja na miundombinu ya masoko,Zaidi ya hayo, uwekezaji wa sekta binafsi na mipango mizuri ya kisera hujenga mazingira wezeshi kibiashara na ukuaji wa sekta ya kilimo.

Hivyo basi serikali inalo jukumu la kushirikiana na mkulima katika kuboresha kilimo bora na chenye faida kisichomnyonya mkulima kwa kiasi kikubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom