Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 24,498
- 34,560
Nguvu kubwa inayotumika (vibaraka) kuhujumu juhudi za rais ni wazi kuna mkono wa wawekezaji wanaotuhumiwa kuhusika na wizi mkubwa wa madini kupitia utaratibu wa kusafirisha mchanga wenye madini hayo.
Haiwezekani Tundu Lisu asimame kupinga mkakati wa rais kwa ajili ya manufaa ya wajukuu wake waje kupata elimu bora na huduma nzuri za kijamii. Bali anafanya hivyo kuwatetea walipakodi wa mataifa ya kibeberu ambayo yamempa mafuzo maalumu ya Sleeping Agent ingawa kwa sasa anajisahau sana.
Sasa, taifa linaelekezwa kumpuuza rais, taifa linashawishiwa kuwa maamuzi ya rais ni ya kijinga. Taifa linajulishwa kwamba ripoti ya tume aliyounda rais ni rubbish (takataka). Taifa linashawishiwa kwamba anayeweza kumtukana rais na kumdhalilisha huyo ni mzalendo na anahitaji sala kumpa ujasiri zaidi. Hili limejitokeza kupitia matukio mbalimbali ya wanasiasa kusimama na wananchi waliothubutu kutukana mamlaka ya rais. Kesi zilizopo mahakamani ni ushahidi tosha.
Sasa nawauliza enyi manyakanga wa matusi na lugha za kudhalilisha, tukishamaliza mkumdhihaki na kumdhalilisha rais nini kifanyike? Je atahitajika tena kwenda kuongea na wawekezaji kurekebisha kasoro za mikataba yetu? Je anahitajika tena kureview mikataba ya madini?
Tukisha mtukana Amiri Jeshi Mkuu, je nini kifanyike baada ya hapo?