Tukisema Akili Duni huwa zinapatikana Jangwani tu pekee muwe mnatuelewa tafadhali

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Katika hali ya Kushangaza na iliyojaa Upuuzi kama si Uduni wa Akili Klabu ya Yanga imepanga kwenda nchini Nigeria na Msafara wa zaidi ya Watu 50 wenye Wachezaji, Waganga wa Kienyeji, Wapishi, Walinzi wa Chooni na Makomandoo.

Inadaiwa kuwa hao wengine ni Makomandoo wao ili wasifanyiwe Fujo kama sehemu ya Kulipiziwa Kisasi baada ya Makomandoo wa Yanga SC kumpiga Rungu la Kichwa Msemaji wa Rivers United FC na Kumpasua.

Hivi Yanga SC Vichwani mwenu zinawatosheni kweli? Mnaenda Ugenini ambako 99% ya Watu ni Wanaijeria wanaojua Kona zote za Mji wa Port Harcourt mnakoenda hao Makomandoo wenu mnaowategemea na Maafisa wa Ubalozini ndiyo watafanya au watazuia nini ili msilipiziwe Kisasi kwa Upuuzi wenu mlioufanya / mliowafanyia?

Kwahiyo mlitegemea muwapige Wanaijeria wa Watu mpaka na Virungu / Magongo ya Mninga kutoka Njombe, Makambako na Mafinga hadi muwapasue kama mlivyowapasua Mkapa Stadium halafu mkienda Kwao wawaonyesheni Uungwana na Ustaarabu wa Kuwapetipeti?

Na huko Nigeria si tu kwamba mtalipiziwa Kisasi kwa Kupigwa ( Kufanyiwa Fujo ) bali kuna uwezekano mkubwa tu hata baadhi ya Wachezaji wenu Wakaolewa na Wapopo ( Wanaijeria ) na wakabakia huko Kimoja.
 
Hasa huyu roporopo huyu lazima wazae naye.

FB_IMG_1631647099990.jpg
 
Back
Top Bottom