SaidAlly
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 2,393
- 2,367
Salaam kwa wote!
Hapa kijijini kwetu tuna utaratibu kwamba kuanzia alfajiri huwa tunaenda shambani mpaka mida ya saa 6 hivi mchana jua likianza kuwa kali, tunarudi majumbani kupata chakula cha mchana (ikiwa ndio kifungua kinywa pia).
Kipindi cha kulima na kupalilia, huwa tunarudi tena shambani majira ya saa kumi mpaka saa 12 mbili hivi tunarudi nyumbani kwa mapumziko ya jumla ya siku.
Kama si kipindi cha kulima na palizi, basi majira hayo ya saa 10 huwa tunajisogeza kijiweni kwetu (kilabuni) kupiga soga za hapa na pale, vijana wengine huingia uwanjani kufanya mazoezi ya kucheza mpira, si mbali sana na hapo kilabuni.
Kwa kuwa kijiji chetu sio kikubwa sana, basi sehemu kubwa ya wanakijiji tunakua eneo hilo isipokua baadhi ya akina mama ambao hubaki nyumbani kwa maandalizi ya chakula cha usiku na mambo yao mengine.
Muda huo pia hutumika kukutana na ndugu jamaa na marafiki, tukihabarishana mambo mbalimbali ya kutwa nzima, maendeleao na vioja pia (soga).
Lakini pia hiyo huwa ni fursa ya kukutana na wageni waliotutembelea hapa kijijini kufahamiana (hasa wanaume).
Hapa kijijini kwetu, tulibahatika kuwa na redio moja. Mwenyekiti wetu (amedumu muda mrefu sana na tunampenda kweli, tumeamua hatutachagua mwingine labda hadi afe) ana mtoto wake mkubwa msomi huko ulaya, ndio alimleteaga hiyo redio na huwa anakuja nayo kilabuni tunasikiliza habari za mkoani na hasa kuhusu wananchi wenzetu wa huko mjini.
Tuna washukuru sana wabunge wetu tunaowachagua kila mara kwani wao kipindi cha kampeni, hutuletea boksi la mabetri (kama sikosei huwa yanakua 36) na tuna tumia mpaka uchaguzi mwingine tena.
Uzuri yakiisha nguvu huwa tuna yaanika juani na yakipungua zaidi hiwa tunayaponda ponda yanaendelea kufanyakazi. Tunapenda sana aina hii kuliko yale aliyoleta disii ukianika au kuyaponda yanatoka ujiuji hayafanyi tena kazi.
Kikubwa ninachomkumbuka kila mara mtoto wa huyu mwenyekiti wetu. Alimwambiaga mzee wake kwamba huwa anapitaga angani hapa kijijini kwetu na kila akipita huwa anawasha kimwelumweli cha ndege tunaiona kwa chini. Hakika tukisikiaga ndege angani kijiji kizima huwa tunampungia mikono.
Leo mwenyekiti hakuwepo alienda mjini kwenye mkutano wa serikali, ilikuja gari teksii kumchukua. Tulifurahi sana. Ingawa tulijua hatutasikiliza redio lakini haina shida tuna furaha tu.
Vile vile mimi si mshamba. Nafahamu tivii pia kama wa mjini, mtoto wa huyu mwenyekiti wetu aliniachiaga zawadi ya gazeti lina picha ya tivii kwahiyo sina wasiwasi siku nikifika mjini sitashindwa kuitambua tivii nikiiona. Nalitunza sana hilo gazeti.
Leo tulipata mgeni ambae alijitambulisha ametokea mjini, na ameandikishwa katika kazi ya uaskari wa wanyamapori.
Baada ya utambulisho, mgeni wetu mtanashati hasa alianza kutusimulia mambo mengi mazuri ya huko mjini. Kadri alivyokua anatusimulia kwa mikogo yake, tulijikuta karibu wanakijiji wote tumemzunguka kama kocha anavyozungukwa na wachezaji kipindi cha mapumziko kupokea maelekezo ya ushindi.
Mgeni wetu mwenye mbwembwe nyingi na madaha, akatusimulia tabia mbili za ajabu za mnyama simba na moja ya nyoka ambazo zimetuacha na tafrani hapa kijijini hatujui hatma ya vijana wetu huko mbeleni katika maisha yao.
KUHUSU SIMBA:
1. Alisema simba anatabia moja, kama hajawahi kula nyama ya mtu na ikatokea siku moja akaila, basi hata kuja kuacha kuwinda watu kamwe. Na hatahangaika kuwinda wanyama wengine tena. Itakua ni watu tu. Akasema na ndio maana wao huko kazini kwao wakisikia simba kala mtu, basi lazima asakwe mpaka apatikane na wamuue.
Hakika wote tulibaki kimya na hamna hata aliyeuliza swali.
2. Mgeni wetu akaendelea kuhusiana na simba. Akasema, kwa kawaida simba mtoto anapokua hufuata tabia za simba wakubwa (wazazi wake - sijui kama ni sahihi kuita hivyo). Akasema simba huyu mdogo huanza kujifunza kuwinda wale wanyama ambao amewahi kuona wazazi wake wakiwinda. Na kamwe hawezi kuwinda mnyama tofauti na aliyewahi kuona kwa wazazi wake.
Nifafanue vizuri, kwa mfano ni kawaida kwa binadamu baba anaweza kuwa mfugaji, lakini mtoto akaja kuwa rasta asiyekula nyama kabisa. Au baba anaweza kuwa mchungaji au sheikh, lakini mtoto akaja kuwa mwanamuziki wa ile mnaita ara endi bii.
Baada ya simulizi hiyo ya pili nikaona vijana karibu wote wamenyong'onyea sana huku wakiwatazama wazee (hii huwa ni ishara katika desturi zetu hapa kijijini kwamba vijana wanaomba msaada wa imani kwa wazee kama kijiji kiko salama). Mara nyingi ikitokea hali kama hiyo basi Mzee mmoja husimama kwa niaba ya wazee wengine na kutoa ufafanuzi wa kuwatia moyo vijana. Na kama kuna mkosaji basi hukemewa hapo hapo mbele ya wote ili aaibike na asirudie. Safari hii hakuna mzee aliyesimama bali wote tukabaki tumejikunyata kwa hofu. Wazee kwa vijana.
KUHUSU NYOKA
Mgeni wetu nafikiri alihisi tumekosa amani kwa simulizi zake kuhusiana na simba, akaamua kuhamia kwa nyoka. Akasema, kuna nyoka wa aina nyingi mbalimbali wasio na idadi (akimaanisha aina za jumla ya maelfu huko ya nyoka).
Akasema pamoja na kuwa na aina nyingi zote hizo, nyoka hao hufahamiana kutoka na hizo aina zao. Na wala hawajichanganyi au kukosea. Akaendelea kusema, kuna aina fulani ya nyoka wao huwa na tabia ya kufuata njia aliyopita nyoka wa aina yake hata kama itapita miaka mia moja.
Yani huyo nyoka aliyepita mwanzo anaweza kuwa aliishakufa kitambo na kuna hata vizazi vingine vitano vikapita hapo katikati lakini nyoka wa kizazi cha sita anaweza kuja kupita mlemle alimopita yule wa kwanza kabisa wa kizazi cha kwanza.
Hakika kabla huyu mgeni wetu hajaendelea na mbwembwe za hadithi yake, alistukia wanakijiji wote tumesimama na kila mmoja akiondoka kufuata njia ya nyumbani kwake kimya kimya bila hata kuongea. Hatua zilikua kali sana na sifikiri kama kuna hata mmoja wetu aligeuka kuangalia nyuma.
Tulitawanyika kama vile tuliambiwa ikipulizwa filimbi basi tutawanyike kimya kimya kila mmoja kwake. Hii si tabia ya kijijini kwetu, mara nyingi wakati wa kutawanyika huwa tunaondoka makundi tofauti tofauti huku tukiendelea na soga tukiongozana tulio majirani na kuachana kila mmoja anapofika kwake mpaka yule wa mwisho.
Pia hutakiana usiku mwema na kupeana ahadi za mambo mbalimbali ya kesho yake.
Lakini leo imekua tofauti kabisa na hofu imetujaa sana kwa tukio hili.
Tafadhari Admins, sijakosea jukwaa. Nimekusudia jukwaa hili hili la siasa.
Wakatabhahu!