Tukinunua tumerogwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukinunua tumerogwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 24, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji (Tanzania Daima Jumatano Machi 18, 2009)

  WAKAKAA katika kikao chao wakakubaliana; “Tuwaambie kuhusu majenereta.”

  Huku wakiwa wametulia mahali wanapojua wao na Mungu wao wakasemezana; “tuhakikishe mjadala unahusu majenereta na siyo mmiliki.” Wakahimizana wakijua ya kwamba dili lao limeshtukiwa na Watanzania.

  “Ndiyo.” Wakagongesheana gilasi wakijua kabisa ya kuwa wakibadili mkakati majenereta yatanunuliwa tu.

  “Tusisitize kuwa ni mapya,” mmoja wao ambaye ni kinara kati yao akawaambia. “Ndiyo!” Mwingine akakubali. “Tuwaambie majenereta tayari yako Tanzania na ni mapya kuna ubaya gani kuyanunua,” wakapanga hoja zao. “Tuhakikishe hawazungumzii Dowans. Wasizungumzie umiliki, wasizungumzie tuliingiaje; wasizungumzie tulitokea wapi.” Wakakumbushana.

  “Ndiyo, sasa tuwaambie mmiliki wake basi.” Likatolewa wazo.

  “Si we bwana jina lako tayari linaonekana, kubali tu na tutawapiga maneno yatakwisha. Mjadala wa mmiliki tutaufunga na turudi kuzungumzia majenereta,” akasema mmoja wao kisha wakacheka. Wakakubaliana, wakatawanyika kama walivyokutana.

  Mmiliki wa Dowans hatimaye akajitokeza na kukubali. Mara ya kwanza nilipozungumza naye alikataa kuijua Dowans; alikataa kabisa kusema amewahi hata kusikia; alikataa akisema kuwa kampuni hiyo haipo Uarabuni. Ndiyo! Alikiri kuwa na urafiki na Rostam lakini alikataa kabisa kuwa Rostam hakuhusika na ujio wa Dowans. Kwa sauti thabiti ya Brigedia Jenerali Suleiman Al-Adawi alikataa kuitambua Dowans! Nikakubali. Sikuridhika.

  Nikapata fomu za BRELA (Wakala wa Usajili wa Makampuni na Utoaji wa Leseni). Nikaziangalia. Nikakuta jina lake, anuani yake, na sahihi yake. Nikasema alinidanganya. Nikasema mheshimiwa huyu aliniuzia kanyaboya. Nikatambua kuwa kama hakusema ukweli, kama hakutaka watu wajue ukweli, kuna kitu alikuwa anaficha. Kitu ambacho hakutaka watu wajue; nikakumbuka.

  Nilipozungumza naye Jumamosi ile tulizungumza vizuri mpaka aliponiniuliza kama mimi ni Mtanzania. Nikamwambia “ndiyo”. Akaniuliza; “unaandika mambo ya systems ya Tanzania?” Nikamjibu “ndiyo mkuu”. Akasema; “Oh”. Haikuwa Oh ya ‘nakuelewa’; ilikuwa ni Oh ya kukata tamaa, ya kukutwa ukifanya usichotakiwa. Ni hapo nikakumbuka alipoanza kukataa kujibu maswali yangu; ambayo naamini ni ya Watanzania wengi.

  Dowans ni kampuni ya nani? Je, anajua Kampuni ya Dowans Holdings ya Uarabuni? Vipi ile Dowans ya Costa Rica; ziko Dowans ngapi? Imeandikishwa wapi na nani? Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz anahusika vipi? Hakutaka kujibu. Akabakia kunipiga mkwara; “Usiandike jina la mtu ambaye huna uhakika naye. Nitakutumia wanasheria wangu waje wazungumze nawe.” Nikakumbuka amenidanganya.

  Jumamosi iliyofuata nikarudi tena nikiwa na ushahidi mkononi. Nikitambua kuwa kati ya Jumamosi ile na Jumamosi hii walifanya kikao chao cha makubaliano. Kikao cha kuhakikisha kuwa lolote liwalo majenereta ya Dowans yatanunuliwa na Jenerali lazima alipwe hela yake kwani “ahadi ni deni”. Walimuahidi kuwa mwisho wa mkataba serikali itanunua majenereta; walimpa moyo kuwa hata wakisitisha msaada kabla afungue kesi Paris ambayo hatutajiandaa kushinda ili hata kama tukikataa kununua bado tumlipe! Ndiyo! Nikarudi tena kumuuliza.

  Nilipompata mara ya pili alikuwa mnyenyekevu zaidi, lakini safari hii alikubali. Hakuzungusha maneno. “Ndiyo mimi, ndiyo namiliki Dowans,” alisema. Nikamuuliza mbona “ulinifunga kamba bosi?” Akasema; “sikujua nani anazungumza na mimi.” Nikacheka. Nilikumbuka nilijitambulisha kwake kuwa naandika kwenye gazeti moja la Tanzania na ninaandika kuhusu suala la ufisadi linalohusisha Kampuni ya Dowans.

  Akajibu maswali yangu mengi; mengine alishindwa kujibu kwa sababu tayari nilikuwa na majibu.

  Dowans haikuingia kwa bahati mbaya. Ilialikwa. Ilialikwa na wakubwa wa nchi hii na wenye nguvu. Sijui nia yao ilikuwa nini, lakini kutatuta tatizo la nishati haikuwa mojawapo. Ulikuwa ni uamuzi wa kibiashara. Uamuzi wa “nikune nami nikukune”. Wakawaalika baada ya Richmond kushindwa; hawakuwa na kampuni ya nishati kwani Al-Adawi mwenye utajiri mkubwa tu anahusika zaidi na mambo ya ujenzi kama rafikiye Rostam.

  Vyanzo vyangu vya uhakika vikanidokeza kuwa ni Rostam aliyemfuata kumpa mwaliko huo ambao naye aliupata kama ombi kutoka “juu”. Akaambiwa walete wala jamaa zako najua wana uwezo wa kuweza kufanya hivyo. Jamaa akashawishiwa alipohakikishiwa kuwa baada ya mkataba serikali itanunua. Hakuna mnunuzi mwingine, asiwadanganye mtu. Serikali isiponunua jenerali amekula hasara.

  Hivyo wanajitahidi. “Fungeni mjadala wa Dowans, na tuiache TANESCO ifanye maamuzi yake,” akasema waziri mhusika. Kwa maneno mengine, “acheni kuhoji-hoji”. Tumeambiwa tunyamaze; tumeambiwa tusizungumzie Dowans tena, tuiache serikali ifanye maamuzi.

  Tutakuwa tumelogwa tukifanya hivyo; tutakuwa tumelaaniwa tukikubali serikali ifanye mambo sirini; tutakuwa tuna kaugonjwa fulani tukiwaacha watawale wapendavyo. Nikasema kwa nini mtu wa porini na mvi hizi nahangaika na mambo ya Dowans? Kwa nini kujihangaisha kupambana na Goliathi na ‘ka kombeo kangu ka kalamu?’ Kwa nini namimi nisikubali tu yaishe? Nikasema nitakuwa msaliti wa ndugu zangu! Nitakuwa ni msaliti wa nchi yangu, nitakuwa msaliti wa dhamira yangu!

  Lakini pia nikajiuliza; hivi kuna ubaya gani wakiyanunua hayo majenereta na kuleta umeme unaohitajika sana? Kuna ubaya gani kutokujali “mmiliki” au jinsi gani alivyoingia nchini? Kama jamaa anakuja na dawa naye ni jambazi si tuchukue tu (rafiki yangu mmoja alinipa mfano huo). Nikakumbuka msemo wa kiswahili “baniani mbaya kiatu chake ni dawa”. Nikasikiliza hoja za watetezi wa “tununue mitambo hii kwani itatupa umeme sasa na tayari iko nchini”. Nikakumbuka kikao “chao”.

  Lakini nikakumbuka kisa cha utotoni. Nilipokuwa mtoto kulikuwa na jamaa mmoja mwizi. Jamaa huyo alipita usiku akaiba jogoo letu moja kubwa na lililonona. Tulipoamka asubuhi tukatafuta jogoo wetu. Hayupo. Majira ya mchana, kuna mtu akapita akiita “nauza jogoo, nauza jogoo”. Tulipofungua mlango tulimuona huyo “njemba” mwizi mwizi na jogoo lake mkononi. Tukakimbia! Aliyekuwa mkubwa nyumbani ikabidi “anunue” jogoo huyo! Alikuwa ni yule yule jogoo wetu! Jamaa alirudia mara mbili, mwisho ikabidi tuwaambie wazazi!

  Ndiyo, tukinunua mitambo ya Dowans itatusaidia kuwa na jogoo wetu; lakini mbona tulishamnunua na kuwa naye bandani? Nikakumbuka. Watanzania hawajali jogoo katoka wapi hata kama alikuwa ni wa kwao alimradi wakiambiwa anatotolesha vizuri! Tuko tayari kumnunua kwa gharama yoyote ile!

  Ndipo nikakumbuka walipobadili sheria iliyotengenezwa kuidhoofisha TANESCO. Yaani wale wale waliotunga sheria ya kuidhoofisha TANESCO leo wanasimama kutuambia ati wanaitetea TANESCO! Nimebakia kucheka tu. Kama kweli wanataka kuisadia TANESCO wabadilishe sheria na kuruhusu kampuni yoyote inayotaka kuzalisha nishati ifanye hivyo na isambaze nishati hiyo yenyewe. Wakitaka kutumia nyaya za TANESCO au miundombinu, TANESCO ndiyo iwachaji. Mtashangaa!

  Leo wametengeneza sheria ambayo wao wenyewe wamejihakikishia ndiyo wanaleta makampuni ya nishati na kuiuzia TANESCO! Nikasema tumelogwa!

  Niseme nini basi? Naweza kusema mengi. Lakini hapa nitasema machache tu. Tuna uamuzi wa kufanya. Kumnunua jogoo tuliyeibiwa au kumwambia mwizi wetu “huyo jogoo ni wetu!” Tunaweza kununua mitambo ya Dowans na suala hili likaisha. Lakini nawahakikishia mapema kabisa; tukinunua mitambo hiyo haina maana kesi yao kule Paris itafutwa! Tunaweza kununua na jamaa wakashinda kesi! Tukawalipa dola milioni 100 wanazotudai kule, na hizi milioni 60 za kununulia mitambo! Halafu tunawapigia magoti kina Brown ati tunaomba “msaada” tumelogwa sisi au tumejiloga wenyewe kwa wenyewe!

  Vinginevyo tunaweza kuwakatalia. Tukawaambia “Hapana Dowans”. Zungumzeni na watengenezaji; tangazeni tenda mpya na wapeni jamaa miezi minane ya kuleta na kufunga mitambo mipya kwa bei nafuu ya hiyo; tuone makampuni mangapi yatajitokeza! Tusikae pembeni tuwaambie watawala wetu hivyo. Tuwaambie kina Rostam na wenzake “inatosha kutuburuza”.

  Nakupa namba za simu, tuma sms au piga waambie: “Tunahitaji Umeme, siyo wa Dowans, zungumzeni na watengenezaji”. Namba ya Rais Kikwete 754 777 775, namba ya Dk. Idris Rashid 754 – 280 442, ya Rostam 754-555 555 na ya Mhe. William Ngeleja ni 754 710 070. Tuwaheshimu lakini tusiwaogope. Ni ndugu zetu hawa, ni Watanzania wenzetu hawa ninaamini kwa wingi wetu tukiwashawishi kwa hoja hatimaye watatusikiliza.

  Kama Al-Adawi ataingia hasara msiwe na wasiwasi. Yeye mwenyewe aliniambia kuwa “kwenye biashara kuna hasara na kuna faida”. Kasema yuko tayari hata wakiamua kuitaifisha mitambo hiyo (itakuwa hasara kwake).

  Lakini niwahakikishie sijui kama sikio la kufa linaweza kusikia dawa. Kwa kadiri mipango ilivyo, Dowans lazima alipwe tu! Aidha kwa kununua mitambo hiyo au kwa kushindwa kesi! Wako tayari kuliachilia moja; yote mawili kuna mtu akili zitamruka.

  Lakini wakiamua kununua kama walivyodhamiria tangu miaka miwili iliyopita, mjue taifa zima sisi tumelogwa! Tukubali tu yaishe tuanze mijadala mingine hii ya ufisadi tutakuwa tumeipoteza rasmi.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  ..kazi nzuri sana.

  ..hii ndiyo investigative journalism tuliyokuwa tukiililia.

  ..again, kazi nzuri. asante sana.
   
 3. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2009
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 35
  Kazi njema hii; Natamani haya mawazo yangemfikia na mjomba wangu kule Byang'ombe
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Mar 24, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Nasubiri ligi ianze.......
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkijiji, kazi nzuri sana, ila inaamsha machungu sana.. mwe Tanzania yangu..
   
 6. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #6
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yaani mungu wa majeshi akulinde na kukubariki sana, asante kwa kazi nzuri unayofanya, utapata dhawabu yake. We are proud ofyou, indeed! Aluta continue!
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,

  Tukinunua tumerogwa! "kwani kidogo basi yani tumisha rogwa ni kmitambo sasa"

  MwnKijiji kazi ni swafi sana, na nilisoma nakara yako last week on the same matter. Je wajua kinachonishangaza nikipi?
  1:Mwandishi kama mwandishi anaweza kuja na document za upelelezi wake na ni swafi na baada ya muda ndio ati serikali yashtuka, ivi wataka kuniambia serikali haina kitengo maarumu cha upelelezi?? plz usije ingiza Takukuru ati nacho ni kitengo cha upelelezi hapa nchini.

  2: Maafisa usalama wetu wapo kweli na kama wanazijua hizi njama zote huwa wanakuwa wapi kuzi fichua au basi hata wazizimio huko kabla hazijafika ndani ya nchi yetu

  3.Nilini nchi i mean serikali yetu itaunda vitengo(vyombo/mashirika) maalumu vya kipelelezi vitakavyo shughurikia mambo haramu kama hayo na viwe na nguvu.

  Sina mengi ya kusema ila inanisikitisha sana kwa mtu kama Mnkijiji mwenye machungu na inchi yake anvyo sakanya habari huku serikali ikikaaa tu kujishebedua na kushindwa fuatilia mambo nyeti kamam hayo wapi uhalisi au umuhimu wa securty Agency yetu??

  Mwanakijiji nasema tena kazi nzuri
   
 8. Poetik Justice

  Poetik Justice Member

  #8
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13


  Hivi…?? beyond the debate on Dowans, shouldn’t it boil down to our values and principles? What signal will we be sending our children if we were to acquire an item or equipment for that matter that has been shrouded in controversy from the very beginning? I am new to forums and debates on politics and the search for social justice and so far what I have learnt inatisha na ninajiuliza maswali mengi nakutamani kurudi kwenye ile dunia yangu comfortable ya ku-pretend everything is alright in TZ and we are a very ‘peaceful’ country and we should forever strive to preserve the ‘peace’!!
   
 9. Sabode

  Sabode Senior Member

  #9
  Mar 24, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ooh God.
  I dont know what's up next coz the move seems to be quet now. It's as if they are in side eating and drinking while we out shouting and starving. THEY JUST DONT' MIND.
  Coz they hear nothing of us. But as time goes on a way to make them hear will be found and they gonna regret.
  Good job Mzee Mkjj keep us informed
   
 10. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nimekupata vilivyo mkuu Mwanakijiji, na tayari nilishaanza kutuma message kwa hawa wahusika. Nimeanza na mkulu wa kaya! Nimemwambia ahakikishe serikali yake inataifisha mitambo ya dowans kwani tayari ni mali ya watanzania! Pili ahakikishe serikali inashinda kesi iliyofunguliwa na dowans na ikiwezekana afungue kesi dhidi ya dowans ya kudai turudishiwe pesa yetu yote tuliyomlipa dowans isivo halali! La sivyo kura yangu 2010 haipati ng'o!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  This is what I'm talking about..! keep up the good work!
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  ..we need to send messages to someone who has a leverage on our President's decisions.unfortunately there is no such person.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  aaah! Mwakijiji, si ulishawahi kusema kuwa majenereta yatanunulwia tu! Basi tumesharogwa tayari au tumsubiri yule ajaye?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  RA vipi yeye?
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Mar 24, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,

  ..RA owns Caspian,JK, etc etc.

  ..tunahitaji mtu anayeweza kumlazimisha JK kusimamia maslahi ya wananchi. RA is not that person.

  NB:

  ..nadhani kesi ya JK and Co., ipelekwe kwa wananchi.

  ..lakini sina uhakika kama wananchi wanaweza kulielewa hili suala la Dowans na Richmond kiasi cha kuwafanya wachukue uamuzi wa busara na wenye manufaa kwao wakati wa kupiga kura.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  MKJJ mimi nakuombea sana tupate vichwa kama wewe 50 tunchi itachangamka...bado naogopa juu yasirikali naombaujilinde na hila za maisadi ambao wengi wao wakoserikalini na wana nguvu sana hata ya dola wasije wakaku......nakuombea maishamarefu...na msimamo usiobadilika....kazi nzuri sana...najua unazidi kuongezamaadaui....
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mzee.. wengine tulishatangaziwa kuwa tushakufa machoni mwao! so why not go out in the "blaze of glory".?
   
 18. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  MMk,

  Asante sana kwa kazi nzuri. Niliweza kumpigia simu Al-adawi na majibu yake kwangu hayakuwa na tofauti na yale aliyokupa wewe.

  Ila kwa upande wangu aliendelea kusema kwamba maamuzi kuhusu kununua ama kutonunua mitambo hiyo yako mikononi mwa "serikali" na wala si shirika. Alinikatisha maongezi kwa kusema kwamba anasubiriwa katika mkutano.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Asante sana Kidatu... of course yeye mazungumzo yake yako na Serikali. Tanesco wataambiwa tu cha kufanya lakini hili ni la serikali na nyuma yake ni JK mwenyewe. Msikose magazeti ya kesho kwa walioko Bongo kwani mengine yataenda mbele zaidi kwenye hili...
   
 20. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Do we have shared values? That has been my question always! Values of can guide our behaviours even if nobody is watching! what is our collective values of Tanzania! It is hard to fight with people of no value, unless you decide to be a maniac! People of no value, have no reasons! So using logic to explain their wrong, we will always loose.
   
Loading...