Tukifanya hivi,Jumuiya ya Afrika Mashariki haitakufa tena

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,146
3,791
1. Kuwe na sera moja ya Uchumi hasa wa viwanda.
2. Thamani ya fedha,iwe moja (iliwahi kuwa hivyo kabla ya uhuru).
3. Kuwe na katiba moja,rais mmoja, nchi wanachama ziongozwe na mawaziri wakuu.
4. Vyama vya siasa viwe na sura ya kijumuiya (mfano kama ilivyo Tz bara na Visiwani).

Kwa uelewa wangu,haya ni kati ya mambo ambayo yakifanyika,jumuiya yetu itakuwa imara.

Nimeangalia kwa umakini,ziara, mikutano ,mahusiano na hoja na hotuba za viongozi wetu wakuu, naona bado kuna hatari ya kutokea yale yale ya 1977.

Kuna migawanyiko inaanza kujitokeza kwa kasi.
 
Kila aliyeshika kamba anavutia kwake. Hili ni soko la bure, soko ambalo halitakuja kuwa na vikwazo kwa nchi wanachama. Lakini kila mwanachama hamuamini mwenzake.
 
Tanzania yenyewe peke yake imewashinda., kubwa mno., Had kuna maeneo mengine yanasahaulika., Leo hii E. Africa iwe na serikali moja. !! Nchi ikiwa ndogo inakua more efficient.
 
Ngumu kumeza, ukizingatia muungano wenu na Zanzibar umejaa utata, kale ni kakisiwa kadogo tu lakini figisu za muungano wenu nao huo haueleweki. Mara mnatishia kuwakatia umeme, mara hiki mara kile. Wanzazibari wenyewe huwa wanaona kama kwamba nyie mnawachelewesha, yaani wao husema wangekua kivyao wangekua mbali kiuchumi.

Tuendelee jinsi tulivyo, kila mtu abaki na makelele yake ya ndani, tuhusiane tu kwenye biashara na ikiwezekana elimu. Pia hilo la fedha naona sawa.
 
1. Kuwe na sera moja ya Uchumi hasa wa viwanda.
2. Thamani ya fedha,iwe moja (iliwahi kuwa hivyo kabla ya uhuru).
3. Kuwe na katiba moja,rais mmoja, nchi wanachama ziongozwe na mawaziri wakuu.
4. Vyama vya siasa viwe na sura ya kijumuiya (mfano kama ilivyo Tz bara na Visiwani).

Kwa uelewa wangu,haya ni kati ya mambo ambayo yakifanyika,jumuiya yetu itakuwa imara.

Nimeangalia kwa umakini,ziara, mikutano ,mahusiano na hoja na hotuba za viongozi wetu wakuu, naona bado kuna hatari ya kutokea yale yale ya 1977.

Kuna migawanyiko inaanza kujitokeza kwa kasi.
Unafaham kuwa changamoto za kufanya hivyo zitakuwa kubwa zaidi ya zilizopo sa hizi?

Hicho kitu sahau hata vilembwekazi vyako havitalikubali hilo
 
Ngumu kumeza, ukizingatia muungano wenu na Zanzibar umejaa utata, kale ni kakisiwa kadogo tu lakini figisu za muungano wenu nao huo haueleweki. Mara mnatishia kuwakatia umeme, mara hiki mara kile. Wanzazibari wenyewe huwa wanaona kama kwamba nyie mnawachelewesha, yaani wao husema wangekua kivyao wangekua mbali kiuchumi.

Tuendelee jinsi tulivyo, kila mtu abaki na makelele yake ya ndani, tuhusiane tu kwenye biashara na ikiwezekana elimu. Pia hilo la fedha naona sawa.

Chokochoko ya Muungano kwa Zanzibar inatoka kwa Wapemba tu na sio Wazanzibari wote. Waunguja na Wapemba wao pia ni maadui wakubwa na wala hawana maelewano.

Kudai kuwa nje ya Muungano Zanzibar ingekuwa mbali ni upuuzi wa hali ya juu. Nje ya Muungano Zanzibar ingekuwa sawa na ndugu zao wa damu Komoro.
 
Ngumu kumeza, ukizingatia muungano wenu na Zanzibar umejaa utata, kale ni kakisiwa kadogo tu lakini figisu za muungano wenu nao huo haueleweki. Mara mnatishia kuwakatia umeme, mara hiki mara kile. Wanzazibari wenyewe huwa wanaona kama kwamba nyie mnawachelewesha, yaani wao husema wangekua kivyao wangekua mbali kiuchumi.

Tuendelee jinsi tulivyo, kila mtu abaki na makelele yake ya ndani, tuhusiane tu kwenye biashara na ikiwezekana elimu. Pia hilo la fedha naona sawa.
Iliyokuwa EAC ya kwanza(1967) kabla ya kuvunjika 1977,inawezekana ilijipambanua zaidi kuliko inayotaka kujengwa sasa. Kulikuwa na commonalities nyingi za kiuchumi ,kiutamaduni na kisiasa, tofauti na ilivyo sasa. Maraisi wale,ndio walikuwa viongozi wa kwanza baada ya kukabidhiwa nchi kutoka wakoloni,na malengo walioanza kujiwekea yalifanana kwa kiasi fulani. Alipoingia Idd Amini 1971,miaka 4 baada ya kuundwa EAC,ndo mambo yalianza kuvurugika! Laiti,wale maraisi wa mwanzo,wangeafiki,akawepo raisi mmoja kwa EAC yote,kusimamia malengo waliyojiwekea, naamini tungekuwa na hatua zaidi za kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.
 
labda tupachikane mimba ndio tutakua na uelewano ,bila hivo hakuna kitu

Na hiyo ndio hoja inayoushikilia muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Eti tumeshatiana mimba miaka mingi.

Sasa, Kenya, Rwanda na Burundi kuna ukabila, sidhani kama watakubali kutiana tiana mimba na Watanzania.
 
Kwani mimba inajua ukabila? Rwanda ,Burundi those are non issue ,kwanza tutiane tiane mimba na watanzania hapo itakua sawa na hii chuki ya Tanzania didi yetu itaisha,,,, si mkubali tuaoe ninyi nyote muwe wake zetu ama niaje my friend?
 
1. Kuwe na sera moja ya Uchumi hasa wa viwanda.
2. Thamani ya fedha,iwe moja (iliwahi kuwa hivyo kabla ya uhuru).
3. Kuwe na katiba moja,rais mmoja, nchi wanachama ziongozwe na mawaziri wakuu.
4. Vyama vya siasa viwe na sura ya kijumuiya (mfano kama ilivyo Tz bara na Visiwani).

Kwa uelewa wangu,haya ni kati ya mambo ambayo yakifanyika,jumuiya yetu itakuwa imara.

Nimeangalia kwa umakini,ziara, mikutano ,mahusiano na hoja na hotuba za viongozi wetu wakuu, naona bado kuna hatari ya kutokea yale yale ya 1977.

Kuna migawanyiko inaanza kujitokeza kwa kasi.
Point namba 2 inashughulikiwa tayari.
Point ya tatu wameamua kuwa na confederate government kwanza kabla ya kuwa na shirikisho.
 
Back
Top Bottom