Tukicheza na elimu taifa litaangamia

roservelt

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,418
1,510
TUKICHEZA NA ELIMU TAIFA LITAANGAMIA
Kama tutaendelea kuwa na elimu ya kusubiri kuajiriwa badala ya kujiajiri,basi tutegemee siku zijazo tutegemee wasomi wetu kuendelea kuwa mafisadi watakaowanyonya walala hoi. Kuendelea kuwa na elimu yenye mfumo ule ule wa kikoloni hautausaidia taifa letu.Kuwa na elimu ambayo inazalisha wahandisi ,ambao hata kutengeneza baiskeli ni tatizo,basi elimu hii ni janga.Hivi lini tutajitengenezea vitu vyetu na sisi tukavithamini na kujikisikia fahari kwamba tuna bidhaa ambazo tunazomiliki
Tusipobadilika tutaendelea kuwa manamba wa wawekezaji wa kibeberu.Tutakuwa na idadi kubwa ya watu wanaohudhuria shule kwa miaka mingi na hawana ujuzi wowote ule.Na kwa hilo hatupaswi hata kushangaa kwamba makundi ya kiovu kama mbwamwitu,panyaroad na mengineyo kutoepuka kujitokeza.
Kwa nchi makini tunaweza kutoka hapo kwa kuwekeza kwenye elimu tu,elimu itakayotoa ujuzi kwa wanafunzi,ambayo itawasaidia kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea serikali ambayo siku zote ikilalamika kushindwa kuajiri ,lakini ikiendeleza kuzalisha wasomi wakimbizi katika ajira.Nasema ni nchi makini tu huchagua kuwekeza katika elimu kwa zaidi ya miaka 50.Kwa nchi ambazo si makini huwekeza katika elimu kama wakulima,kwa maana ya miezi mitano au wakijitahidi sana kama wakulima wa miti ambao hutmia miaka kumi halafu wanategea kuvuna.Kwa kufanya hivi tuendavyo hatutafika.
Hatutafika kwa sababu ,tutaendelea kubadili mfumo wa elimu kwa kujinasibu kuwa elimu imepanda kwa uwingi wa kudahili wanafunzi wengi bila kuangalia ubora wa elimu inayopatikana.Tutakwenda kwenda kwenye majukwaa na kuwatangazia wananchi kwamba elimu ni bora ili kuwahadaa wananchi watupatie kura na mtaji wa kisiasa uweze kuimarika.Ni kweli tutaimalika kisiasa lakini kwa miaka zaidi ya hamsini vizazi vyetu watakuwa watumwa zaidi katika elimu yao.
Ni ukweli mchungu ukikosea kuwekeza kwnye elimu,huwezi kupata athari papo hapo,athari zitapatikana baada ya miaka kadhaa ijayo,na ndio maana hata wadau muhimu wa elimu wakilalamika,umuhimu wao hauonekani papo hapo kwa sababu jamii na serikali haiathiki moja kwa moja.Ni tofauti na madaktari ,madereva,waandishi wa habari,wafanyabiashara,askari na makundi mengine ,yakilalamika na kugoma athari zake zitaonekana hapo hapo. Watu wataathirika,na serikali itapoteza mapato.
Kwa walimu hali itakuwa tofauti kabisa,huenda kwa sababu elimu yetu ya Tanzania hata kama walimu wakilalamika na kugoma wanaoathirika ni watoto wa kimaskini na ndio maana hata serikali inaacha walimu waendelee kulalamika.Vyovyote vile ,athari za migomo ya walimu ndio inayotuletea madaktari feki,waandishi wa habari makanjanja,walimu wasiostahili,madereva wasiojali na kufuata sheriawafanya biashara wakwepa kodi na kadhalika.
Nchi za Singapore na Malaysia ni kupigiwa mfano duniani kwa kuwa viongozi wao waliamua kuwekeza katika elimu,ikumbuke kuwa kuwa mwaka wa uhuru wa Tanganyika 1961 nchi hizi tulizipita kiuchumi.Kwa sasa wametupita kiuchumi ,hatuna tofauti sana na Yule aliyeanza safari kwa kutumia baiskeli ya miti na kuendelea kuitukuza teknolojia hiyo hiyo miaka nenda rudi.Viongozi wao wakajipanga vizuri ili wasafiri haraka kiuchumi ni vizuri kuboresha baiskeli zao toka kwenye miti hadi za kisasa,ndio maana wakatukuta njiani tukiendelea kujikokota na baiskeli zetu za miti.Wakatukuta na kutupita.Ndio Singapore ni cnhi iliyokuwa maskini ukilinganisha na Tanzania.Nchi iliyokuwa na madimbwi yaliyokuwa yakizalisha mbu,nchi iliyokuwa ikitoa harufu mbaya,harufu isiyostahili kuvutwa na binadamu,nchi ambayo haikuwa na raslimali yoyote ya kujivunia.Kwa kuwa viongozi wao walitambua kuwa hakuna nchi nyingine ya kwenda basi waliamua kuaandaa rasilimali watu.Wakawekeza kwenye elimu,elimu iliyowatoa kwenye madimbwi machafu,magonjwa,harafu safi na kujiwezesha kujenga viwanda,madimbwi kugeuzwa sehemu ya maji safi na yaliyowezesha kuanzisha kilimo. Hiyo ndio Singapore ambayo siku zote viongozi wetu ,kazi yao kwenda kujifunza kinadharia na hufika kuleta porojo za kinadharia tu,huenda kwa sababu ya elimu waliyoipata viongozi wetu.Ukiwekeza vibaya kwenye elimu basi tutegemee tu baada ya kuhitimu wasomi wetu wazunguke maofisini na bahasha zao kusaka ajira hadi soli za viatu vyao ziishe.
Nchi za Singapore,Malaysia na Venezuela ni nchi ambazo zinawaheshimu na kuwathamini walimu wao,wanaamini ndio waliotoa nchi zao katika wimbi la umaskini,ndio maana kwao walimu ni kama lulu au dhahabu .Tanzania walimu ni watu wasiothaminika ,wanaodharaulika katika jamii,wamekuwa wakilalamia miaka nenda rudi kuhusu maslai yao.Serikali ya Tanzania imeziba masikio na kufukia mabonde yasiyoweza kufukika katika uhalisia.Tumekuwa watu wa kufika na mipango zima moto ya kufurahisha wananchi.Mara kuunganisha masomo ya sayansi,kufuta masomo ya biashara na kilimo,mara matokeo makubwa sasa,mara tubadilishe divisheni kwenda GPA,GPA kwenda divisheni,elimu bure.Ni kuhangaika tu hakuna suluhisho.Inaonekana hauna dhamira ya dhati kuikomboa elimu ya kitanzania na viongozi wetu wamekuwa kama ni wahamiaji vile,hata wataalamu wamekuwa sio wazalendo kabisa kana kwamba ni wageni kabisa na mfumo wa elimu ya Tanzania.
Nchi inayotegemea kilimo katika uchumi wan chi unafuta masomo ya kilimo na biashara hapo nafikiri utandawazi ulikuwa unafikiri badala ya akili zao,matokeo makubwa sasa hivi unawezaje kuwa na matokeo makubwa katika elimu kwa kutoa semina kwa maafisa ili hali wapiga kazi wakiwa na malalamiko kuhusu malimbikizo ya mishahara,mazingira bora ya kufundishia,mishahara kiduchu ukilinganisha na gharama za maisha,maabara ,vifaa na zana za kufundishia ni haba.Walimu walewale wachache wa sayansi ndio watakaoleta matokeo makubwa?Kwa motisha gani?Tumekuwa watu wa kudanganyana kwa takwimu ili kupata mtaji wa kisiasa na sio kuangalia mustakabali wa taifa letu.Divisheni au GPA zina tija gani kama watu wanashindwa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine
Matokeo mabaya ya elimu ni kuwa na wanasheria wabaya watakaofikiria zaidi rejea za vifungu vya sheri kutoka katika nchi za magharibi badala ya kuwa wabunifu kutunga sheria kupitia mazingira wanayoishi,kuamini kujua kiingereza ni kusoma kumbe ni lugha ya biashara kama ilivyokuwa lugha ya Kiswahili na lugha nyinginezo,kuamini utamaduni wetu wakishenzi na sio kiistarabu isipokuwa ule wa kimagharibi wa kutembea nusu uchi,kuvalia nguo makalioni kana kwambwa unafanya biashara ya matangazo ya nguo za ndani. Tukitamba tunakwenda na wakati ,huko ni kutojitambua .
Nimalizie kwa kusema kuwa tusipobadilika kwa kuwajali walimu maslai yao taifa litaangamia,taifa litakuwa na viongozi vibaraka na mazuzu wengi wenye kujali maslai binafsi na mataifa ya kibeberu.tunatakiwa kupata elimu itakayotukomboa kutoka kwenye lindi la umaskini kama ilivyo kwa nchi za Singapore,Malaysia,Venezuela,Botswana na nchi nyingine zenye kufanya vizuri
GODFREY ELZIAR kwa maoni na ushauri namba 0655544847,baruapepepe:godelziar@gmail.com( Mwalimu mwanafunzi chuo kikuu cha Iringa)
 
Back
Top Bottom