Tukiacha unafiki kusema kweli Magufuli anapiga kazi ila kuna mapungufu madogo sana akiweza kuyafanyia kazi atakuwa rais bora sana

Babaako

Member
Mar 10, 2016
15
45
Mimi sio mfuasi wa chama chochote cha siasa na huwa sipendi sana kuongelea siasa lakini huwezi kuikwepa siasa kwa sababu tunaishi kwa kuongozwa na wanasiasa, tunafuata sheria zilizotungwa na wanasiasa kwa hiyo japo sipendi kujihusisha na siasa lakini maamuzi ya wanasiasa yana effect kwenye maisha yetu. Chanzo cha matatizo yote duniani ni siasa. Duniani kote ambako kuna machafuko chanzo ni siasa.

Anyway acha niende kwenye mada moja kwa moja. Kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha habari tukiacha unafiki na kusimama kwenye haki rais anapiga kazi. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake. Anachokifanya Magufuri hakuna mtangulizi wake aliyeweza kukifanya.

Tukianzia kwenye ajira serikalini zamani ilikuwa karibia na kwamba haiwezekani kwa mtu wa asiyekuwa na mtu anayemjua kupata kazi nzuri serikalini. Kupata kazi kama tra, wizara ya fedha na mashirika ya serikali ambayo yana maslahi mazuri ilikuwa haiwezekani kwa mtoto wa mkulima asiyekuwa na refa huko juu. Lakini sasa hivi kila mwenye sifa anapata kazi (zinapotangazwa). Ukija kwenye miundo mbinu, japo watu wanabeza, rais anajitahidi sana.

Bila kuboresha miundo mbinu huwezi kukuza uchumi. Magufuri ana vision, ana malengo ya muda mrefu. Watu wanaweza wasione effects za hii standard gauge kwa sasa lakini hii inakuja kuchochea uchumi kwa kasi sana. Nchi zote zilizoendelea zimewekeza pakubwa kwenye miundo mbinu na mawasiliano. Bila miundo mbinu bora kukuza uchumi haiwezekani. Kwa wachumi hilo wanalielewa.

Pamoja na kazi kubwa anayoifanya kuna mapungufu madogo madogo bado yanaendelea kumharibia. Ningependa kuyataja mambo mawili ambayo yanawagusa moja kwa moja raia wa kawaida.

1. Swala la fao la kujitoa kusitishwa hapo anahitaji kupaangalia kwa jicho la tatu. Haiwezekani mtu aishi maisha ya tabu baada ya kuacha kazi wakati hela anayo. Hiyo sio haki hata kidogo. Mtu asipangiwe jinsi ya kutumia hela yake aliyoitafuta kwa jasho. Apewe hela yake aanze maisha mapya. Ukisema asubiri mpaka afikishe miaka 60, unategemea ataifikishaje hiyo miaka bila kufa na magonjwa au stress kwa sababu ya ugumu wa maisha? Mpe mtu mafao yake afanye hata biashara ili ajihudumie yeye na familia yake.

2. Hili sina uhakika nalo sana ila nina imani lipo ndani ya uwezo wake kulifanyia kazi. Siasa sio uadui, kama watendaji wake wa chini wanafanya haya mambo bila ridhaa yake inabidi aliangalie vizuri.

All in all Tanzania haijapata rais kama huyu. Tunaweza tusiyaone matunda kwa sasa ila vizazi vyetu hakika vitakuja kuishi kwenye nchi ya asali na maziwa.
 
Last edited by a moderator:

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,065
2,000
Yani we kama baba mkeo anakusifia watimiza wajibu sahihi huo ni wajibu wako . We umeona moja tu umesahau milion ya mapungufu
1. Demokrasia
2. 1.5 tr
3. Katiba mpya
4. Upendeleo wa kikabila au ukanda
5. Uhuru wa wewe hadi vyombo vya habar
6. Ajira.
7. Kauli zake
8.uchumi wa mmoja mmoja
9.....
KAZI ANAPIGA ILA NI WAJIBU WAKE
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,842
2,000
Akimaliza mihula yake ndo ukwel utajulikana tu kwa sasa Kuna mgongano wa kimaslahi siyo rahisi kuacha unafiki.
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,704
2,000
'All in all Tanzania haijapata rais kama huyu. Tunaweza tusiyaone matunda kwa sasa ila vizazi vyetu hakika vitakuja kuishi kwenye nchi ya asali na maziwa' said it well...
 
kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,584
2,000
Mimi sio mfuasi wa chama chochote cha siasa na huwa sipendi sana kuongelea siasa lakini huwezi kuikwepa siasa kwa sababu tunaishi kwa kuongozwa na wanasiasa, tunafuata sheria zilizotungwa na wanasiasa kwa hiyo japo sipendi kujihusisha na siasa lakini maamuzi ya wanasiasa yana effect kwenye maisha yetu. Chanzo cha matatizo yote duniani ni siasa. Duniani kote ambako kuna machafuko chanzo ni siasa.

Anyway acha niende kwenye mada moja kwa moja. Kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha habari tukiacha unafiki na kusimama kwenye haki rais anapiga kazi. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake. Anachokifanya Magufuri hakuna mtangulizi wake aliyeweza kukifanya.

Tukianzia kwenye ajira serikalini zamani ilikuwa karibia na kwamba haiwezekani kwa mtu wa asiyekuwa na mtu anayemjua kupata kazi nzuri serikalini. Kupata kazi kama tra, wizara ya fedha na mashirika ya serikali ambayo yana maslahi mazuri ilikuwa haiwezekani kwa mtoto wa mkulima asiyekuwa na refa huko juu. Lakini sasa hivi kila mwenye sifa anapata kazi (zinapotangazwa). Ukija kwenye miundo mbinu, japo watu wanabeza, rais anajitahidi sana.

Bila kuboresha miundo mbinu huwezi kukuza uchumi. Magufuri ana vision, ana malengo ya muda mrefu. Watu wanaweza wasione effects za hii standard gauge kwa sasa lakini hii inakuja kuchochea uchumi kwa kasi sana. Nchi zote zilizoendelea zimewekeza pakubwa kwenye miundo mbinu na mawasiliano. Bila miundo mbinu bora kukuza uchumi haiwezekani. Kwa wachumi hilo wanalielewa.

Pamoja na kazi kubwa anayoifanya kuna mapungufu madogo madogo bado yanaendelea kumharibia. Ningependa kuyataja mambo mawili ambayo yanawagusa moja kwa moja raia wa kawaida.

1. Swala la fao la kujitoa kusitishwa hapo anahitaji kupaangalia kwa jicho la tatu. Haiwezekani mtu aishi maisha ya tabu baada ya kuacha kazi wakati hela anayo. Hiyo sio haki hata kidogo. Mtu asipangiwe jinsi ya kutumia hela yake aliyoitafuta kwa jasho. Apewe hela yake aanze maisha mapya. Ukisema asubiri mpaka afikishe miaka 60, unategemea ataifikishaje hiyo miaka bila kufa na magonjwa au stress kwa sababu ya ugumu wa maisha? Mpe mtu mafao yake afanye hata biashara ili ajihudumie yeye na familia yake.

2. Hili sina uhakika nalo sana ila nina imani lipo ndani ya uwezo wake kulifanyia kazi. Siasa sio uadui, kama watendaji wake wa chini wanafanya haya mambo bila ridhaa yake inabidi aliangalie vizuri.

All in all Tanzania haijapata rais kama huyu. Tunaweza tusiyaone matunda kwa sasa ila vizazi vyetu hakika vitakuja kuishi kwenye nchi ya asali na maziwa.
Hata kuandika jina la Rais hujui?! Halafu nyie mnaojifanya hamna vyama ni wanafiki wakubwa.
Eti mambo madogo. Mafao ya kujitoa umeona ni jambo dogo? Watu wanajiua kwa hasira? Mtu amefanya kazi miaka 20 ananyimwa mafao yake uneona jambo dogo?
Halafu unazungumzia ajira, unayajua mateso yake?
Go back to school
 
gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Yaani akiweza kurekebisha hapo atakuwa rais kipenzi cha watu wote, japo najua huwezi kupendwa na watu wote lakini atawin trust ya watu wengi sana.
Unasemaje awe kipenzi cha watu wote kwa sababu ya hilo moja tu wakati Tundu Lissu akiuguza majeraha ya risasi sababu za siasa zake za chuki dhidi ya wapinzani! Ukimkosoa tu uhai wako unakuwa hatarini!

Watumishi wote wa umma miaka mitatu sasa hakuna nyongeza ya mishahara wala kupanda madaraja kama sheria ya utumishi wa umma inavyotaka, hivyo mvunja sheria hawezi kuwa rais bora kamwe labda kwa jamii iliyojaa wajinga wengi
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,000
2,000
2. Hili sina uhakika nalo sana ila nina imani lipo ndani ya uwezo wake kulifanyia kazi. Siasa sio uadui, kama watendaji wake wa chini wanafanya haya mambo bila ridhaa yake inabidi aliangalie vizuri.
Kwa hili mkuu unajiuma uma sana. Kama ndio hilo unalosema, sioni kama ataweza kulifanyia kazi, dalili zote na vitendo ambavyo yeye ndiye anae ongeza zina niaminisha kuwa RAISI wangu anachukulia kuwa SIASA NI UADUI. Walio chini yake wanajua analo lifanya-sijaona hata mmoja akikemewa sana sana wanapandishwa vyeo. Na hili si dogo.
Hayo unayo ona ni mazuri, tatizo kubwa yeye ana utaratibu wake aujuao yeye ambao sisi wengine tunaona unakwenda kinyume na sheria tulizojiwekea. Miradi inafanyika nnje ya bajeti kwa kipaumbele cha nani kwa mfano madege hayo? Mimi nikikuambia elimu ndiyo inahitaji uwekezaji mkubwa kuliko vyote nchi hii utasemaje?
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
2,000
Maneno yake na Vitendo vyake vinatosha kutupa Tafsiri ya ni Mtu wa namna gani ,wewe msifie tu ongeza na Mapambio kabisa.Alie juu ana waona .
 
Babaako

Member
Mar 10, 2016
15
45
Kwa hili mkuu unajiuma uma sana. Kama ndio hilo unalosema, sioni kama ataweza kulifanyia kazi, dalili zote na vitendo ambavyo yeye ndiye anae ongeza zina niaminisha kuwa RAISI wangu anachukulia kuwa SIASA NI UADUI. Walio chini yake wanajua analo lifanya-sijaona hata mmoja akikemewa sana sana wanapandishwa vyeo. Na hili si dogo.
Hayo unayo ona ni mazuri, tatizo kubwa yeye ana utaratibu wake aujuao yeye ambao sisi wengine tunaona unakwenda kinyume na sheria tulizojiwekea. Miradi inafanyika nnje ya bajeti kwa kipaumbele cha nani kwa mfano madege hayo? Mimi nikikuambia elimu ndiyo inahitaji uwekezaji mkubwa kuliko vyote nchi hii utasemaje?
Mkuu miundo mbinu na elimu vyote ni vyanzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi. Kwa hiyo kama uwezo upo wa kuvitekeleza vyote kwa wakati mmoja basi vitekelezwe ila kama huo uwezo haupo basi tekeleza kimoja kwanza ukimaliza tekeleza kingine, na hicho ndio kinachofanyika. Rais kachagua kwanza kutekeleza miundombinu.
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,563
2,000
Mkuu hilo la Tundu Lisu kila mcha Mungu analilaani. Nimeliongelea hapo chini kama mambo mawili anayotakiwa kuyaboresha. Hakuna uhakika wa moja kwa moja kama yeye aliagiza Tundu Lisu kushambuliwa, huo uhakika hakuna ila kwa sababu yeye anauwezo wa kuamrisha vyombo vya ulinzi na usalama kuwapata wahusika nafikiri lawana ndio inapoanzia, ndio maana nikasema siasa sio uadui, kama kuna watendaji wake wa chini wanafanya siasa za hivyo au ndio waliohusika na hicho kitendo cha kutaka kujipendekeza kwake, lipo ndani ya uwezo wake kulikemea na kulikomesha maana uwezo anao. Lakini huwezi kumhusisha moja kwa moja na hicho kitendo kwa sababu ukweli ni kwamba hakuna mwenye uhakika anayemjua aliyefanya hicho kitendo. Usihukumu usije ukahukumiwa, nina imani hata wewe unaamini Rais hajafanya hicho kitendo maana huo uhakika huna. Kwa hiyo tusimhukumu kwa sababu hatujui mhusika.

Mkuu Chakaza tunaomba utuwekee humu ile kauli yake ya kumtaka Ndugai awafukuze Wapinzani Bungeni ili yeye adili nao Mtaani..

Labda huyu Jamaa atatuelewa kirahisi ya ni kwa nini Serikali yake inahusika ktk Tukio lile baya kabisa la kushambuliwa kwa Mh Lissu..Pamoja na Hatua zilizo chukuliwa baada ya Tukio lile ndio zime pigia Mstari kabisa .
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,000
2,000
Kwa hiyo kama uwezo upo wa kuvitekeleza vyote kwa wakati mmoja basi vitekelezwe ila kama huo uwezo haupo basi tekeleza kimoja kwanza ukimaliza tekeleza kingine,
Na hapo ndiyo pakuangalia. Ni vipaumbele vya nani vitekelezwe? Tatizo hapa ndiyo mwenye meno anakula nyama nyingi au yote. Kwetu mkalia kiti anauwezo wa kuamua vipaumbele vya taifa yeye mwenyewe, hela anatoa wapi anajua yeye na hakuna wa kumuuliza. Hili ndiyo naliona tatizo.
 
laki si pesa.

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
10,016
2,000
Yaani akiweza kurekebisha hapo atakuwa rais kipenzi cha watu wote, japo najua huwezi kupendwa na watu wote lakini atawin trust ya watu wengi sana.
fao la kujitoa ndio upuuzi gani huo?….. Mimi mkulima wa viazi huku Njombe linanisaidia nini hilo? au unadhani watanzania wote wameajiriwa
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,834
2,000
Mimi sio mfuasi wa chama chochote cha siasa na huwa sipendi sana kuongelea siasa lakini huwezi kuikwepa siasa kwa sababu tunaishi kwa kuongozwa na wanasiasa, tunafuata sheria zilizotungwa na wanasiasa kwa hiyo japo sipendi kujihusisha na siasa lakini maamuzi ya wanasiasa yana effect kwenye maisha yetu. Chanzo cha matatizo yote duniani ni siasa. Duniani kote ambako kuna machafuko chanzo ni siasa.

Anyway acha niende kwenye mada moja kwa moja. Kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha habari tukiacha unafiki na kusimama kwenye haki rais anapiga kazi. Mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake. Anachokifanya Magufuri hakuna mtangulizi wake aliyeweza kukifanya.

Tukianzia kwenye ajira serikalini zamani ilikuwa karibia na kwamba haiwezekani kwa mtu wa asiyekuwa na mtu anayemjua kupata kazi nzuri serikalini. Kupata kazi kama tra, wizara ya fedha na mashirika ya serikali ambayo yana maslahi mazuri ilikuwa haiwezekani kwa mtoto wa mkulima asiyekuwa na refa huko juu. Lakini sasa hivi kila mwenye sifa anapata kazi (zinapotangazwa). Ukija kwenye miundo mbinu, japo watu wanabeza, rais anajitahidi sana.

Bila kuboresha miundo mbinu huwezi kukuza uchumi. Magufuri ana vision, ana malengo ya muda mrefu. Watu wanaweza wasione effects za hii standard gauge kwa sasa lakini hii inakuja kuchochea uchumi kwa kasi sana. Nchi zote zilizoendelea zimewekeza pakubwa kwenye miundo mbinu na mawasiliano. Bila miundo mbinu bora kukuza uchumi haiwezekani. Kwa wachumi hilo wanalielewa.

Pamoja na kazi kubwa anayoifanya kuna mapungufu madogo madogo bado yanaendelea kumharibia. Ningependa kuyataja mambo mawili ambayo yanawagusa moja kwa moja raia wa kawaida.

1. Swala la fao la kujitoa kusitishwa hapo anahitaji kupaangalia kwa jicho la tatu. Haiwezekani mtu aishi maisha ya tabu baada ya kuacha kazi wakati hela anayo. Hiyo sio haki hata kidogo. Mtu asipangiwe jinsi ya kutumia hela yake aliyoitafuta kwa jasho. Apewe hela yake aanze maisha mapya. Ukisema asubiri mpaka afikishe miaka 60, unategemea ataifikishaje hiyo miaka bila kufa na magonjwa au stress kwa sababu ya ugumu wa maisha? Mpe mtu mafao yake afanye hata biashara ili ajihudumie yeye na familia yake.

2. Hili sina uhakika nalo sana ila nina imani lipo ndani ya uwezo wake kulifanyia kazi. Siasa sio uadui, kama watendaji wake wa chini wanafanya haya mambo bila ridhaa yake inabidi aliangalie vizuri.

All in all Tanzania haijapata rais kama huyu. Tunaweza tusiyaone matunda kwa sasa ila vizazi vyetu hakika vitakuja kuishi kwenye nchi ya asali na maziwa.
tu rimuvi fridomu ov wot😂😂😂😃😃
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom