Tukae upande wa "Ceteris Paribus", Sijui tunaruhusiwa

Tukae upande wa "Ceteris Paribus", Sijui tunaruhusiwa

Thinker96

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
347
Reaction score
135
Chaguzi za kidemokrasia zimeanza 1995 na zitaendelea ila ushindi mkubwa katika historia mpaka wa leo ni 2025 kwa aslimia 96.7%. na walioshindwa ni asilimia 3.3%.

Kwa akili za wataalamu wetu wanaotuaminisha:-

1) Kulitokea mpango wa vurugu za mapinduzi yaani hiyo asilimia 3.3% ina mwamko mkubwa wa kimapinduzi kabisa. Sasa basi imepelekea vifo vya watu (sijui ndìo waasi wenyewe) na mimi ndugu yangu mmoja walimpiga risasi nadhani mbili tumeshazika tulipewa mwili.

2) Sasa wale wahaini waliokuwa wanashirikiana na wale waasi wameachiwa kwa msamaha tunashukuru sana wasomi kwa hilo. Ila kuna wengine bado wameshikiliwa itakuwa ndo wenyewe wala si kwamba wametolewa kafara au kwanza sheria ichukue mkondo wake

3) Uwepo wa siku ya kuwakumbuka waharifu walioleta vurugu (kwa hotuba ya Chande inavyoeleza) sidhani kama ni sahihi kwa kuwa walikuwa wanataka kuipindua serikali halali ya kiraia mfano Operation MKIRU nao watataka tuwawekee siku wakumbukwe kwa kuwa pia wapo waliofuata mkumbo hata kwenye uharifu huo. Au itakuwa siku ya kumbukumbu kwa maafisa usalama basi watajwe majina tunaowakumbuka na tuwaandike katika mnara wa kumbukumbu kwa kuwa serikali yetu ni imara itaandika majina ya mshujaa wetu na Siku ya kuwakumbuka itakuwa October. 29 ili tuunganishe na ya 2001 Zanzibar au iwe November.

3. Mengine hapa mtaongezea . . .

Kinachoonekana wakati huu kwa maoni yangu binafsi:-

1) Nafasi za kufaidi keki ya taifa zinatolewa kwa upendeleo na wengine wanafika mbali zaidi kuwapachika ndugu na watoto wao katika nafasi za uongozi waTanzania hawa watatulia? Pia kuna jinsi hao mnaowaweka kwenye nafasi wanaona jinsi mnavyoongoza kwa roho nzuri au mbaya ndo wanajifunza kupitia kwenu. Kwa hiyo mnaweza kuwa mnaowasaidia nafasi za ajira au vyeo mmewaweka katika nafasi hatari kama msipowapa msingi bora.

Kwa hili cha kwanza kufanyika viboko shuleni vitiliwe mkazo ili kizazi cha waoga kiendelee kuwepo mli muwasaidie hao mnaowaweka kwenye nafasi lakini kama viboko vikifutwa hao watakuwa katika nafasi hatari zaidi (tufikirie kwa utashi).

2) Hata kama ni uhaba wa ajira kiasi gani ajira na nafasi zitolewe kwa haki. Yaani watu wawe selected kwa mfumo waingie hata watu asilimia 100 ya wale wanaohitajika washide oral harafu zitolewe number binafsi harafu waachie kompyuta ichague hao asilimia kumi wanaohitajika. Kwa ufupi kompyuta ndo ifanye random selection iwe programmed hivyo ili tutoe upendeleo.

3) Kuwe na mfumo wa kompyuta wa upigaji wa kura na pia number za Nida ndo zitumike kupiga kura mfumo wa physical wa makaratasi sio wa haki sana na pia unaamsha hisia. Wataalam wa kumpyuta wapo hata kama tutataka usalama wa kimtadao mashirika makubwa ya kiulinzi yapo yanayotumika na mabank ni salama sana kwa kuwa tunaweka cross security ambayo ni ngumu hata kwa kuingilia siri za ndani. Mfano wanapewa Sisco(USA) na Huawei(China) walinde mifumo wakati wa uchaguzi.

4) Ifanyike namna ili kuondoa visasi kwa kuwekwa ukweli hadharani na uwajibikaji. Kwani hali kama hii ilifanyika South Africa na Rwanda mpaka wa leo wanaishi kwa amani. Tofauti na hivyo isipofanyika basi visasi kwa madhaifu ya kibinadamu vitakuwepo na baadhi mkikumbuka kuna nyinyi wenyewe au watoto wenu mliowaweka au watakaokuja kwenye mifumo vitawafuata. Okay, hili nilielezee kwa jinsi hii hakuna wakati ambao gharama ya ulinzi wa viongozi wakiwa ndani inatumika kubwa kama kipindi hiki na kila siku ikipita pasi na kuona kisasi ni suala la kushukuru kwa Mungu maana ukweli tupo kwenye hali mbaya maana hata wananchi kwa wananchi uvumilivu umekuwa mdogo. Yaani kwa kifupi bampa to bampa hata wananchi kwa wananchi sasa angalau nyinyi wachache mnaulinzi yaani viongozi.

Watu walichojifunza huenda tusipofanikiwa kumaliza tofauti zetu na kuweka ubabe bila watu kuondoa vinyongo ( Inaweza kutokea kwa mliopo kwenye nafasi au watoto/ndugu zenu mliowaweka au kuwapambania au kujipambania wakapata nafasi). Kwanza kiukweli huenda ikatokea "assassination" za kibinafsi mtu anapanga bila kushirikisha yeyote yule kwa kuwa viongozi wetu wa kiimani, afisi zetu za usalama na walezi wetu wapo vizuri sana. Mtu anajua nikiwashirikisha nitaghairi kutekeleza hili:-
Mfano zilizofanikiwa na kushindwa
-2024 Donald Trump, Alikoswakoswa na FBI, CIA walikuwepo.
-1981 Ronald Reagan, Alikoswakoswa pia
-1981 John Paul II Walinzi waKirumi walikuwepo kakoswakoswa
-1972 Abeid Karume, Aliuwawa

Wote hao baadhi watendaji hawajawahi kueleweka malengo wala sababu zao za kufanya walichokifanya. Hata wataalamu wa historia makosa walishindwa kujua malengo ya watendaji wa huo uharifu. Sasa hivi visasi vya kunyemelea ni vibaya sana kwa kuwa kila siku mtu unadhani unawindwa na inapelekea mtu unakuwa katili sana kwa kuwa unajua haukutengeneza na uliowakosea.

Nitaendelea kuelezea ila na pia nipo tayari kurekebishwa kwa mawazo mbadala!
 
"Ceteris peribus" hautaeweka na watu kibao humu bwashee! 😁

Enzi zetu tukishiba mihogo na pesa ya bumu, tunasema tumefikia "Marginal Propensity to Consume".
Wazee wa kulipa kwa "Promissory note"....

Economics ni tamu sana!
 
Back
Top Bottom