Tujuzeni matokeo : Cameroon vs manyara stars....mliopo uwanjani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujuzeni matokeo : Cameroon vs manyara stars....mliopo uwanjani

Discussion in 'Sports' started by only83, Apr 9, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...WanaJF tupeni updates za game la Cameroon na Manyara Stars... wengine presha inapanda na kushuka....
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  hata mimi nayangojea mkuu nadani jamaa wata tu updates
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  Jeshi la Julio laivaa Cameroon Send to a friend Saturday, 09 April 2011 09:56 0diggsdigg

  [​IMG] Mshambuliaji wa timu ya taifa U/23 Mrisho Ngasa akipita katikati ya mabeki wa timu hiyo wakati wa mazoezi jana jioni kwenye Uwanja ea Karume jijini Dar es salaam

  Sosthenes Nyoni
  TIMU ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 23, leo inatarajia kushusha ama kupandisha presha za Watanzania pale itakapovaana na Cameroon katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpiki utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Kushusha ama kupanda kwa presha za Watanzania kutategemeana na matokeo ya mchezo huo yatakayoamua timu hiyo kusonga mbele au kubaki.

  Tanzania inashuka dimbani ikiwa na deni la bao moja tu baada ya ule wa awali ulifanyika nchini Cameroon kukubali kipigo cha mabao 2-1kutoka kwa wenyeji.

  Tayari kocha Jamhuri Kihwelo'Julio' ameongeza baadhi ya wachezaji katika kikosi chake kitakachoikabili Camoroon leo akiwemo nyota wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mrisho Ngassa akisaidiana na washambuliaji chipukizi wenye kasi Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.

  Hata hivyo vijana hao watamkosa nahodha wake Salum Telela aliyeonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa awali na tayari nafasi yake amepewa kipa Shaaban Kado akisaidiwa na Himid Mao.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Julio alisema kuwa watalazimika kupigana kufa au kupona ili waweze kushinda mpambano huo huku akiwataka wachezaji wake wacheze kwa tahadhari.

  "Tuna bao moja la ugenini, lakini hii haitoshi na kujiona tumeshinda kwa vile tunacheza nyumbani, zinahitajika jitihada za dhati ili tuwewe kupata mabao ikiwezekana mengi,"alisema Julio.

  Kwa upande wa Ngasa mwenye thamani ya Sh 54m, alisema atajituma kwa uwezo wake wote kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili waweze kushinda mchezo huo dhidi ya Cameroon.

  "Nipo hakuhakikisha tunaipeperusha vema bendera yetu, ni matumaini yangu kwa kushirikia wote na mashabiki wetu basi tutashinda na kusonga mbele."Naye kocha wa Cameroon, Dieudonne Nke alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha kwaajili ya kukabiliana na wapinzania wao.

  "Tuko vizuri sasa, hali ya hewa ya hapa haitusumbui kwasababu inafanana na ya kule kwetu hivyo kilichobaki ni kupigana uwanjani tu na nina hakika tutashinda,"alisema Nke.
   
 4. RR

  RR JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Dk 17.... 1-1
   
 5. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #5
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Tunawashambulia sana Cameroon tatizo ni umliziaji tu.....Pia mabeki wamefanya uzembe wa hali ya juu sana kuruhusu goli hili moja.....

  Mrisho Ngasa hayupo hata kwenye subs(safi sana hii,naona TFF wamestuka)
   
 6. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #6
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Dakika ya 35 bado ngoma nzito 1-1 Ngassa hayumo ni bora tumestukia...
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  natumai tutashinda , naomba gundu lisiwepo ili haya mashambulizi yazae matunda
   
 8. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Half time sasa

  Manyara Stars 1 Cameroon 1
   
 9. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #9
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Half time score 1-1, umaliziaji bado ni issue, samatta na ulimwengu wanapoteza nafasi kibao za wanahitaji kutulia 2nd hafu, kwenye kiungo kigi makassy na abubakari salumu 'sure boy' bado hawajakaa vizuri. HIVI BAADA YA MECHI YA LEO TUKISHINDA NDIO TUMEFUZU AU BADO MECHI NGAPI?
   
 10. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #10
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mdau endelea ku2juza,by the way goli le2 kafunga nani?
   
 11. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #11
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  tafadhali naomba kujuwa wafungaji(mfungaji wa goli la manyara)na lango kasimama nani?
   
 12. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #12
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  bado kuna raundi ya pili,vp maudhulio?
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kipindi cha pili tayari kimeanza...........Kila la heri Manyara Stars
   
 14. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #14
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nani alitangulia kufunga? na mfungaji wa Manyara Stars ni nani? Na mazingira ya goli ilikuwa vipi? Ni penati, kona, shuti au....?
   
 15. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mbwana samatta anakosa nafasi ya wazi yeye na kipa dakika ya 58 bado 1-1
   
 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Tunashambuliwa sasa......Beki yetu inavuja ile mbaya
   
 17. m

  mbezibeach Senior Member

  #17
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Goli la la PILI TUMEFUNGA MFUNGAJI NI THOMAS ULIMWENGU
   
 18. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #18
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  dakika ya 65 guess who? Thomas Ulimwengu anatunyanyua vitini sisi 2 wao 1
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  tuongeze mawili sasa an tusiruhusu goli lingine hapa
   
 20. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama ni hivi basi matumaini yapo! Tutashinda!!
   
Loading...