Tujuzeni kinachoendelea Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Wenye kujuwa kinachoendelea watwambie. Tetesi zimekuwa nyingi kuhusu mwenendo wa huko.

Kuna taarifa mambo hayaendi sawa serikalini hasa ukata wa fedha na kukosekana madawa hospitalini.

Kuhusu siasa kuna tetesi za kuwepo ujumbe kutoka UN kufuatiia mzozo wa uchaGUZI NA DELEGATION HIYO KUKUTANA NA CUF NA CCM NINI KINAENDELEA HAKIJULIKANI.

Kuna tetesi za CUF kutaka kufunguwa kesi The Hague na kuwashtaki viongozi akiwemo Dr Shein, Mwanasheria mkuu wa serikali (SMZ) na Jecha jee kuna ukweli?

Maisha ya huko yanaripotiwa kuwa magumu mara dufu na kule kususiana kunaendelea kwa kasi hasa kisiwani Pemba.

Leteni ukweli.
 
maisha yanaenda vizuri sana,,, wananchi wanaipenda sana serikali yao na rais wao kipenzi Shein... kiufupi maisha ya Zanzibar ni kama Dubai vile..
 
maisha yanaenda vizuri sana,,, wananchi wanaipenda sana serikali yao na rais wao kipenzi Shein... kiufupi maisha ya Zanzibar ni kama Dubai vile..

Nilipata taarifa ya kususiwa maziko mwanachama mmoja huko Pemba, watu walifunga msikiti kwa kufuli na polisi kuingilia kati kufunguwa kwa nguvu na kuchukuwa jeneza.

Hata hivyo taarifa zinasema watu walisusia na maiti kuswaliwa na watu wachache wa familia tena chini ya mti.

Inasikitisha.
 
We ukiona watoto wa kike wa kizanzibar wamekubali kuwa ma barmaid kwenye local pubs basi ujue mambo ni "mazuri" mno
 
Kwa nini usiende mwenyewe kujiona hali halisi...ya kuona sio ya kusikia...ukiona utaelewa zaidi unachokitaka!
 
Nilipata taarifa ya kususiwa maziko mwanachama mmoja huko Pemba, watu walifunga msikiti kwa kufuli na polisi kuingilia kati kufunguwa kwa nguvu na kuchukuwa jeneza.

Hata hivyo taarifa zinasema watu walisusia na maiti kuswaliwa na watu wachache wa familia tena chini ya mti.

Inasikitisha.
huo ni uongo mkuu. Zanzibar mambo safi sana
 
Uchaguzi ushapita sasa ni kazi tu

Usijifariji.

Uchaguzi umepita madhambi ya uchaguzi huo yapo na hayakwisha.

Ndio kwanza wadau (CUF) wanafunguwa kesi.

Hili la ukata na kukosekana dawa vile vile lipo. Wagonjwa pale mnazi mmmoja zanzibar wananunulishwa hadi mirija ya dripu Taarifa zipo ukata mbaya sana
 
Kwa hiyo CUF wangeshinda dawa zingepatikana?
 
Nilipata taarifa ya kususiwa maziko mwanachama mmoja huko Pemba, watu walifunga msikiti kwa kufuli na polisi kuingilia kati kufunguwa kwa nguvu na kuchukuwa jeneza.

Hata hivyo taarifa zinasema watu walisusia na maiti kuswaliwa na watu wachache wa familia tena chini ya mti.

Inasikitisha.
Sasa Muungwana mbona una taarifa moja tu na nikama huna uhakika nayo hayo mengine yote yame tokea wapi?
 
Zanzibar sukari ipo? Maana huku kwetu Gezaulole sukari inazidi bei ya petrol.
 
Kwa hiyo CUF wangeshinda dawa zingepatikana?

Hayo ni maneno yako. Uchaguzi wa Zanzibar wa marudio umelazimishwa kwa gharama ambazo zimeathiri mipango katika sekta nyengine na kumbuka bajeti haikuwepo popote. Leo hospitali kukosa dawa sio jambo geni
 
Sasa Muungwana mbona una taarifa moja tu na nikama huna uhakika nayo hayo mengine yote yame tokea wapi?

Hii ya kususia mazishi nimeithibitisha na ile ya ukata na kukosa dawa nimethibitisha kwa vyanzo binafsi. Aidha hili la CUF kutaka kufunguwa kesi lipo kwenye gazeti la "The Guardian la IPP Media la tarehe 12 Mei, 2016.

Zanzibar kuna kitu kinaendelea tujuvyeni zaidi
 
Mliweka mpira kwapani leo mnajipendekeza un nyambafu mwacheni shein apige kazi nchi imetulia sana
 
Back
Top Bottom