Tujue Daktari Wilbroad Slaa ana lipi moyoni juu ya Lissu kushambuliwa

Naomba ufafanuzi kidogo ndugu barafu...je kuna tofauti gani Dr. Slaa alivyokaribishwa Chadema na Lowassa alivyokaribishwa Chadema? Ninavyosimuliwa ni kwamba wote hawa wawili waliikimbia CCM baada ya majina yao kukatwa huko na Chadema kuwapa nafasi ya kupeperusha bendera. Dr. Slaa alipeperusha bendera katika kugombea Ubunge Karatu mwaka 1995 na Lowassa alipeperusha bendera katika kugombea Urais Tanzania mwaka 2015.

Mkuu Mag3
nimeiona hoja yako,na kwa kweli hapo umenibana,na uungwana ni vitendo,ninaomba kuchutama.

Lakini hoja inaweza kuwa moja katika mfanano,kuwa Eddo walimsema sana katika kashfa nyingi za ufisadi na ukwapuaji serikalini kuanzia 2007-2015,hii ingekuwa labda taswira mbaya kwa Dr kumnadi mtu ambaye alimsema kwa muda wote yeye akiwa kama katibu mkuu wa chama.

Lakini pia Dr,kama binadamu mwenye "egoism" nadhani aliona kudharaulika na kukosa heshima,ipo pia dhana ya shinikizo la mke na pia ahadi ya upande wa pili kumpa madaraka ili kupunguza ushindani.

Yote kwa yote,hayo ni mapungufu ya Dr,lakini katika mazuri yake,Dr ni mmoja kati ya wanasiasa wa upinzani ambaye Tanzania haitamsahau,mwaminifu,mjenga hoja na mnyoofu,ambaye kila uchafu waliokuwa wanampaka haufanikiwi.

Kwa heshima yake,na kwa mwisho ulio mwema,namuomba aliepuke sana suala la Lissu.Maana zaidi ya uanasiasa wake,kiapo chake cha Upadre kipo mpaka mauti yake.
 
Dr Slaa amekua CDM kwa miaka mingi na amekipigania sana chama, pamoja ni sarakasi walizomfanyia 2015 naamini moyoni bado ni mwanaharakati, ni vile tu umri umeenda na watu wenyewe aliokua akiwapigania walimgeuka, kumtukana na kumtupa nje as if he was nothing! ili tu kumpa nafasi waziri mkuu wa zamani ambaye alikimbilia CDM sio kwakua anapenda itikadi au falsafa za chama bali ili atimize ndoto yake binafsi ya kugombea urais.
Dr. akiongea anaweza kujihatarishia mkate wake kwa ajili ya watu wasio na shukrani, ni vema akae kimya na aendelee kula kivulini, mwisho wa siku JPM anekua mwema zaidi kwake.
Hata maoni tu haruhusiwi kuyatoa?
Dr. Slaa hatoweza kuongea chochote zaidi atawajibu wamfuate Kamanda Sirro au uchunguzi ukikamilika yeye ndipo ataongea, Tatizo hili suala tunalijadili kisiasa zaidi lakini hili jambo liliitaji wataalamu wa uchunguzi na hii ndiyo kete wanaiyotumia wakina Lissu maana hili jambo baada watoe ushirikiano kwa vyombo husika wenyewe waliona bora ata dereva akimbizwe ili litumike kama mtaji wa kisiasa na hapa ndipo linanifanya niamini huu mchezo walicheza wenyewe.
 
nimeiona hoja yako,na kwa kweli hapo umenibana,na uungwana ni vitendo,ninaomba kuchutama.

Lakini hoja inaweza kuwa moja katika mfanano,kuwa Eddo walimsema sana katika kashfa nyingi za ufisadi na ukwapuaji serikalini kuanzia 2007-2015,hii ingekuwa labda taswira mbaya kwa Dr kumnadi mtu ambaye alimsema kwa muda wote yeye akiwa kama katibu mkuu wa chama.

Lakini pia Dr,kama binadamu mwenye "egoism" nadhani aliona kudharaulika na kukosa heshima,ipo pia dhana ya shinikizo la mke na pia ahadi ya upande wa pili kumpa madaraka ili kupunguza ushindani.

Yote kwa yote,hayo ni mapungufu ya Dr,lakini katika mazuri yake,Dr ni mmoja kati ya wanasiasa wa upinzani ambaye Tanzania haitamsahau,mwaminifu,mjenga hoja na mnyoofu,ambaye kila uchafu waliokuwa wanampaka haufanikiwi.

Kwa heshima yake,na kwa mwisho ulio mwema,namuomba aliepuke sana suala la Lissu.Maana zaidi ya uanasiasa wake,kiapo chake cha Upadre kipo mpaka mauti yake.
Amini nakuambia hili la mkewe kumfungia ndani na kuahidiwa madaraka zilikuwa Propaganda tu ili kupunguza joto la kipindi kile na Chadema kitengo cha Propaganda hasa kwenye mitandao kiko vizuri sana kikiongozwa na wakina Mdude Chadema, Kama utakumbuka Lissu aliposhambuliwa Mh Rais alitweet kwa kumpa pole na kuviagiza vyombo vya usalama kushughulikia lile suala kwa haraka na wahalifu wakamatwe! Lakini Mdude Chadema ndiye alianza kwa kureply ile Tweeter ya Mh Rais kuwa akaandika "Ukimuona mtu anakimbilia kukupa pole huyo ndiyo mchawi wako" Hii ilikuja kubadili upepo kabisa wa tukio lile na mwisho wa siku mpaka leo wanamsema Mh Ndiye muhusika.

Dr. Slaa hatoongea lolote juu ya shambulizi lile zaidi ya kusema atatoa maoni yake mara baada ya uchunguzi kukamilika labda.
 
Mkuu Britannica, kwanza asante kuniweka kwenye wachambuzi nguli wa jf kwa viwango vyako Ila kiukweli mimi sio nguli ila humu jf manguli wa ukweli tunao.

Pili msimamo wa Dr. Slaa utapatikana iwapo waratibu wa ziara za Mh.Tundu Lissu watampangia kwenda Sweden na afanye mahojiano kama yale ya VOA, huku Lissu, huku Dr. Slaa

Kiukweli sijapenda unavyosema kwenye suala la Lissu mimi nazunguka zunguka tuu, sii kweli

Wengi wanazungumzia tukio na waliotenda shambulio lile na kulaanu lakini sii wengi wanaozumzia waliopanga na the motive behind na jinsi ya kusaidia kuwabaini wasiojulikana

Mkuu Britanica, kwanza nilisisitiza humu
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Kisha nikataja aina mbili za wasiojulikana.
Shambulio la Lissu: Wajue Wasiojulikana Watakaojulikana na 'Wasiojulikana' Ambao Kamwe, Hawatajulikana!. - JamiiForums

Kisha nikasema sisi waandishi wa habari wenye uwezo wa kufanya IJ, tunaweza kuwabaini.
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija - JamiiForums

Na mwisho nikasema, watu wenye uwezo wa kuwabaini wasiojulikana hawa, wapo, ila serikali yetu haijashindwa, kuwabaini, ikifikia mahali ikashindwa, itasema na itaomba msaada, watu wa kusaidia watajitokeza.

WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi? - JamiiForums

Tena nikasisitiza watu humu jf wapo sana tuu wenye uwezo wa kusaidia
TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums

P.
Nimekupata vema sana
 
Back
Top Bottom