Tujizuie kutoa majibu mepesi kwenye mambo mazito ya kitaifa, kwa sasa kuna wasomi kila sehemu nchini

Mimi ni msomi mjasiriamali ninayeridhika na vipato vyangu. Sijawahi kulipwa na chama kwenye lolote.
Wee ni muongo, nani hakujui ni Chawa wa Veggies, tena kindaki ndaki.
😂😂😂😂😂 kwani imekuaje mbona ghafla sanaa?
Kulikonii?? 😂😂😂😂😂
 
Kuna chanzo kimoja kilisema kuwa TZ ina tani 9 za dhahabu, Algeria tani 173+ za dhahabu, swali likaja, Je, hawa Algeria wao hawaangalii mizania ya akiba ya dhahabu ni sisi tz tu?. NB: Kama na wewe jellyfish (kiumbe wa baharini asiye na ubongo wala moyo, na hajui kama yupo hai, joking) umeanza kuona madudu haya, basi kumekucha.
 
Wee ni muongo, nani hakujui ni Chawa wa Veggies, tena kindaki ndaki.
😂😂😂😂😂 kwani imekuaje mbona ghafla sanaa?
Kulikonii?? 😂😂😂😂😂
Mbona kwa miaka mingi nimekuwa nikidhani una akili timamu?! Nini kimekupata?
 
Hadi wewe umesanuka?? Kweli tumefikia patamu.
Wallah kila mtu atafikiwa, tuwe wapolee.
😂😂😂😂
Ndiyo maana Mimi hapa JF Huwa simIgnore mtu,
Mtu akiwa tofauti na wewe katika jambo Fulani, mpuuzie katika jambo Hilo.
Katika mambo mengine mnaweza kuwa pamoja.
 
Binafsi sina tatizo na dhahabu kuuzwa ili kujenga miundombinu ila hayo majibu kuwa imeuzwa ili kusawazisha mizania hayajakaa sawa.
Hakuna mwana ccm mwenye akili timamu ya kuweza kujibu hoja . Wanachoweza wao ni kuiba kura Kisha kuua watu na kusingizia wengine
Yani unajua watu Kisha unasema nchi yetu tajir sijui inaonewa wivu
Ni upuuzi Toka juu Hadi chini
 
ha ha ha akiba ya dhahabu thamani ni ya 2 billion usd, vipi yule fisadi aliyesema kwamba belarus anainvest 7 billion usd in tanzagiza kujenga viwanda? aliishia wapi? mbona tunakimbizana na ''vijisenti ya 2 billion'' wakati belalus analeta 7 billion usd? ..
 
Kungekuwa limitations za kiwango Fulani cha dhahabu basi USA wasingeruhusiwa kuhifadhi zaidi ya tani 8,000..
Tanzania hatupo kwenye list ya nchi 30 Bora za uhifadhi wa dhahabu kwakifupi bado tupo nyuma sanaaa
Screenshot_20260131-100525.png
 
"Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo"

Nimeandika huu uzi baada ya kusoma hayo majibu ya BOT kuhusu kuuza dhahabu. Kiukweli hili ni jibu la kipropaganda toka kwa mtaalamu wa BOT. Hiyo mizania ya kazi gani kwenye nchi ambayo bado inajitafuta? Yaani sisi Tanzania tukishakuwa na dhahabu ya $2b hatutaki tena zingine? Binafsi sina tatizo dhahabu kadhaa kuuzwa ili kujenga miundombinu ila haya majibu kuwa imeuzwa ili kusawazisha mizania sikubaliani nayo.

Niikumbushe serikali yangu ya chama pendwa CCM ni kuwa kwa sasa wasomi wapo kila sehemu kwenye kila sekta. Mwaka 2018 kwenye mgahawa wangu jijini Dsm dada aliyekuwa anaandaa vitafunwa alikuwa ni graduate Bcom from UDSM (UDBS). Kwenye vijiwe vya bodaboda, site za ujenzi, mashambani, uvuvi na sehemu zingine zote zilizoonekana kuwa sio kwa wasomi kwa sasa zimejaa graduates. Kuwajibu kisiasa ni kuzidi kuharibu image ya serikali.

Nilishangaa hivi karibuni huko Facebook kwenye page ya madereva wa malori yanayosafiri nchi jirani wanachambua sheria mpya ya uhamiaji nchini Zambia ambayo itakuwa kero kwa truck drivers. Yaani huwezi amini jamaa wameandika barua kwenda SADC kupinga hiyo sheria. Kimsingi wasomi kwa sasa wapo kila sehemu.
Washauri wetu kuna Mgalu wa Bagamoyo na kuna walindi, sijui ni graduates WA wapi
 
Tafakuri yangu baada ya kumsikia yule kiongozi wa Benki Kuu

Dhahabu imeuzwa kwa ajili ya reserve manajimenti (balance sheet ya akiba) ili kuweka Sawa kiwango cha dhahabu veza vi fedha za kigeni.

Mfano mdogo
Kama akiba ya nyumbani kwako ni mchele, mahindi na maharagwe. Na wewe unadunduliza akiba hiyo, sasa Ukizidisha Sana mchele(dhahabu) kuna hatari utaipata ya kifedha, mfano akiba ya dhahabu haina riba imekaa Tu mpaka utakapoiuza. Pia ipo hatari ya bei kushuka.

Kupungunza hatari hizo, wameuza sehemu kidogo ya akiba ya dhahabu na fedha hizo kama Benki Kuu zingine zinawekezwa kwenye dhamana za nje kama sehemu pia ya akiba na mapato yake kuongeza akiba.

Kinyumbani akiba nyingi ya mchele pia inaweza haribika, kushuka bei na kadhalika. La misingi kuweka uwiano wa akiba zako, chungu kimoja kisiwe na aina moja kwa wingi.

BIla ya Shaka hii haizuii Benki Kuu ya Tanzania kuendelea na ununuzi wa dhahabu kuongeza akiba, na bilashaka watauza sehemu inayozidi kubalansi uwiano wa aina za akiba nyingine kwenye kibubu cha Taifa.

Sasa Hilo la kuuza dhahabu kugharamia miundombinu halijafanyika, kwani fedha yoyote ya ziada lazima ipite na kuidhinishwa na Bunge.

Serikali ikiagiza azimio Hilo litapelekwa bungeni, labda ipigwe kimya kimya ambalo litakuwa uvunjifu wa taratibu. Na tutaimba Mkulima Kala Mbegu anataka kutuua njaa.

Kwa hili nawasikiliza wataalam, likifika huko bungeni kuomba fedha hizo za akiba utakuwa story mingine
 
Kwenye Bodaboda na vibanda vya M-Pesa wasomi ni wengi wenye Bachelor Degree
 
Majibu mepesi, kwenye mambo mazito ya nchi
 
Back
Top Bottom