Uchaguzi 2020 TUJISAHIHISHE : Huu ni mjadala wa kutaja makosa yanayofanywa na kiongozi wa chama chako na chama kingine tuweze kupata viongozi bora mwaka 2020

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,332
17,835
Nimehamasika kuandika uzi huu kutokana na kitabu cha baba wa Taifa Julius K. Nyerere cha mwaka 1962 kiitwacho TUJISAHIHISHE.

Kitabu ni kirefu kuweza kuwekwa hapa kilichomo chote, lakini ni kifupi ukitaka kukisoma kwani kina kurasa 12 tu ktk mfumo wa kielektroniki wa PDF.

Kwa muktadha wa mada yangu na kwa mwenendo wa yanayo endelea kwenye vyama vikubwa vya siasa nchini Tanzania hasa awamu ya kwanza ya uongozi wa Mh. John P. Magufuli nitaenda kuzungumzia kifupi na kunukuu haya ya mwisho ya kitabu husika.

Yapi yanayo endelea kwenye vyama vya siasa kwa sasa? Ni ukweli ulio wazi karibu ndani ya vyama vyote kumetokea kulaumiana na kunyoosheana vidole miongoni mwa wanachama wa kawaida na viongozi wao, au baina ya viongozi wenyewe kwa wenyewe au viongozi wastaafu na walio katika nyadhifa zao wakati huu.

Lawama na manung'uniko haya vimepelekea baadhi ya wanachama kufukuzwa au kujitoa kwenye vyama vyao na kwenda vyama vingine au kukaa pembeni na kutojihusisha na kile wanacho ona sio sahihi.

Msingi wa maridhiano ni kuambiana ukweli na kuoneshana makosa yetu, kisha kujisahihisha.
Mara nyingi watu huoneana aibu, au wengine wapo ngazi za chini hawawezi kupata nafasi ya kuwaeleza viongozi wao yale wanayo ona hao viongozi wanakosea.

Hii sasa ni nafasi hadhimu ya kuwaeleza ukweli.

Kabla ya yote ningeomba ninukuuu hiyo haya niliyosema na ujumbe uliomo ndio uwe msingi wa mjadala wetu yaani tunapotaja makosa ya chama shindani au kiongozi shindani tusisahau kutaja mabaya ya vyama vyetu au viongozi wa vyama vyetu sabubu ya ukaribu wetu au kuogopa kuwachukiza wana JF. n.k.

Maana sasa hivi kumeibuka kikundi cha wanachama flani toka vyama viwili au vitatu vikubwa wa kutukana matusi mazito mtu yeyote anae jaribu kukosoa au kuonesha udhaifu wa kiongozi wao au chama chao, Hivi vyama sio kificho ni CCM, CHADEMA na ACT.

Kuna kundi la vijana kama wameagizwa kuja kutukana yeyote anae toa mawazo kinzani na chama chao au kiongozi wao.

Kujifanya hauoni au kujiaminisha hakuna tatizo kwenye chama chako au kiongozi wako wa ngazi yeyote hakuondoi tatizo husika, na huenda likaleta madhara makubwa na kukikosesha ushindi chama chako au kukisambaratisha kabisa miaka michache ijayo. Waambieni hapa makosa yao viongozi au wanachama wenu wa kawaida.

" ........
Sitaki mtu yeyote afikiri kuwa mimi niliye andika maneno hayo sinayo makosa hayo. Hivyo si kweli. Kosa moja kubwa sana ambalo pia linatokana na unafsi ni kutaja makosa ambayo sisi wenyewe hatunayo, na kuficha makosa ambayo sisi wenyewe tunayo.

Hii ni kosa lile lile linalotufanya tulaumu tusiowapenda, na kutolaumu tunaowapenda, bila kujali ukweli. Nimetaja makosa haya ili yatusaidie, siyo katika kuwahukumu wenzetu tu ambalo ni jambo rahisi, lakini katika kujihukumu sisi wenyewe, ambalo ni jambo gumu na la maana zaidi"
Julius K. Nyerere.

http://hakielimu.org/files/publications/document149tijisahihishe.pdf



KARIBUNI, WELCOME, BIENVENIDOS, BIENVENUE, WILLKOMMEN, BEM-VINDO, RECENTI!
 
Wale wa kila kitu mabeberu someni hapa Nyerere anawaambia nini ..
Sababu-rahisi-Nyerere.JPG
 
Ndio mlivyopanga kututoa katika reli kwa hizi proganda za kishamba, kiongozi bora anatoka miongoni mwa watanzania kama tungekuwa tunazingatia haki, uwazi na usawa, hizi vitu hakuna Tanzania vyama baadae.

Unawauliza maustazi Nguruwe kachinja nani? ili ujue kama ni halali au haramu!!! hata akichinja shekh Juma wao kwao ni haramu na hawali. Kama unataka mjadala wa kupata viongozi bora weka katiba mpya kwanza, na vyombo vya dora viache kutia najisi chaguzi zetu hii ni pamoja na tume.
 
Kutaja makosa hakutatufikisha kokote kama;
1. Hatuna tume huru ya uchaguzi
2. Kama viongozi wataendelea kupatikana kwa kificho kificho bila kushindanishwa kwenye midahalo shirikishi, ya wazi na ya muda mrefu!

Chaguzi za kitapeli tapeli...zitaendelea kutupa viongozi tapeli tapeli!!

Tuanzie hapa...!!
 
Kwaza ungeweka pdf ya hizo page chache hapa.
Lakin mi naamini hakuna chama chenye nguvu kazi watu ya kutosha.CCM haina watu makini.CDM ina watu makini lakini si wengi kuweza kuongoza nchi.ACT haina watu kabisa.Ila Tanzania Inawatu wa kuipeleka mbele.

Fikiria kama Wabunge wote wa upinzani na wa chama tawala na wale maprofesa wetu wangeacha siasa za kishamba na kufanya jambo moja kubwa kwa Tanzania.!Naamini Tanzania ingekuwa mbali.Ila kwa mawaziri hawa akina Jafo,Mwigulu,Makamba JR,Zitto na wengineo wenye ndoto za kuwa rais naona bado hawana pa kuipeleka nchi ila kama tungefanya kama timu ingewezekana.

Kule WWE leo mnapambanishwa kama maadui,kesho mnapangwa timu moja na mnafanya vizuri mnapewa mkanda.Hata sisi tungeacha uadui tujenge nchi.Yote haya kwa sababu TISS hawajitambui wote wala hawajui nini cha kufanya.Wameshindwa kuvuka kivuli Cha CCM.sasa wao wanaamini ccm ndio nchi.Wao wangesuka mpango wa kuiua kabisa ccm na kuinua vyama vingine japo viwili au vitatu na vile vidogo visivyo hata na wanachama 200 nchi nzima wavifute kimkakati kisha tupambane kwa uhuru na haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio mlivyopanga kututoa katika reli kwa hizi proganda za kishamba
Unaposema "mlivyopanga" unamaanisha mimi na akina nani?
Natanguliza shukrani.

Angalizo: Usiishi au usichukuie kila jambo kwa hisia sana unaweza kukosa good judgement kwenye mambo ya msingi.
 
Nawalaumu viongozi wa CHADEMA ambao wanaamini kuwa kuna ccm itatenda haki kwa kuwa tu wao wanawahubiri uvumilivu. Twende underground, ccm hawa mbona weupe mno!

Kuna siku isiyo na jina idadi ya waliokata tamaa itakapofikia optimum level hakuna cha Mabeyo, Sirro au TISS itakayofua dafu. Watatupa bunduki zao na kutoroka.

Mungu Jehovah atujaalie uhai tutakiona nilichoandika hapa muda si mrefu ujao.
 
Nimenote commdnt yako
Nawalaumu viongozi wa CHADEMA ambao wanaamini kuwa kuna ccm itatenda haki kwa kuwa tu wao wanawahubiri uvumilivu. Twende underground, ccm hawa mbona weupe mno!

Kuna siku isiyo na jina idadi ya waliokata tamaa itakapofikia optimum level hakuna cha Mabeyo, Sirro au TISS itakayofua dafu. Watatupa bunduki zao na kutoroka.

Mungu Jehovah atujaalie uhai tutakiona nilichoandika hapa muda si mrefu ujao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom