Tujipange: Kutaifishwa mzigo wa almasi Airport ni mwanzo wa vita ya kibiashara kati ya Tz na De-Beers

Thamani ya almasi imekuzwa mno.

Kifupi almasi ni carbon tu.

Ukichukuwa mkaa ukaweka kwenye mgandamizo mkubwa na joto kali unapata almasi.

Almasi haina thamani kama watu wanavyodanganywa.

Pia si haba kushinda tanzanite au Ruby.

Almasi inatengenezwa hata laboratory. Na quality ni ile ile.

Hawa De Beers wahuni sana hawa.

Yani wamefanikiwa kuihadaa dunia kuhusu thamani ya almasi.

Nashangaa baadhi ya wenzi wanaotaka kuoana wanakwangua account zao kisa wapate kipande cha "mkaa" kwaajili ya pete ya ndoa.

Bora ununue Tanzanite, 1000 times rare than diamond.
Ha ha ha ha umenchekesha sana
 
Mkuu,haya alotaja sio mapya ni mambo ambayo ukiwa na utamadunu wa kujisomea na kufuatilia historia ya vitu mbalimbali utayajua tu.baada ya kusoma bandiko kama hili ni vyema kuzidisha udadisi na kujifunza zaidi
Sawa sio mapya. .
Mbona yeye tu ndio huwa anatushushia hizi nondo na sio wewe! ?
Just appreciate mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I hate so much such comments. sasa ungependa tuwaachie tu waendelee kuchota bila kunawa mikono? faida itakuwa wapi? tunachohitaji warudi kwenye utaratibu wa 'win-win situation. Mtu mwoga katika mapambano haya akae kimya aache wenye nia tusonge mbele. Kama Botswana na Namibia wanafaidika na madini hayo hayo kwa nini sisi tusifaidike?? Tunajua madhara ya hao watu na JPM mbona ameshasema amejitoa kwa niaba ya wanaqnchi sasa kilichobaki nikuwaleta mezani tukubaliane wapate kwa upande wao na sisi pia tupate lakini sio kupinga kila kitu ukiendeleea na woga wako utaibiwa mpaka mke wako
Mbona hasira kaka!?
Hakuna anaefurahia kuibiwa. Ila tutumie njia sahihi kupambana na sio lazima tulete mikwaruzo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine hujiuliza wale walimu na wahadhiri wa Historia na Uchumi hufanya nini shuleni au ni vichwa vibovu vyetu wanafunzi! Nina hakika kama tungekuwa katika ubora wa kufundisha na kupokea mafundisho yanayoandamana na uzalendo naamini tungekuwa mbali kidogo au tungehisi mabadiliko.
Kwa nini tunashindwa kujifunza kwa Watswana au Wanamibia waliopata uhuru juzi juzi tu!? Kwa nini wao wameweza kuwa na kiburi cha kugoma kuburuzwa na hawa De-beers na wengine?
Upo uwezekano kweli wa hawa jamaa kutuwahi sokoni kama walivyomfanyia Williamson haha kumuua kwa ulevi.
Na kwa kuwa wanajua sisi tuna NJAA kubwa na hatuna ujanja na hayo watatuvuruga tu.... soko ni lao, madini ni yao, wateja ni wao! Hakika kama kwenye hiyo timu ya mazungumzo hawatokuwemo Wanahistoria- Uchumi wabobezi wazalendo tutapigwa.....hakika tutauziana almasi kama ndizi pale Mabibo kwani haitokuwa na thamani yoyote.
Kama walitulazimisha kufunga kiwanda cha kuchonga Almasi pale Iringa ili kuwapatia ajira ndugu zao India na kwingine si ajabu kuishusha daraja almasi yetu kwa motto wao mpya wa ajabu wa A KIMBERLEY DIAMOND FOREVER....na wataweza tu...
Suluhu ya hakika ni Win-win situation

Big up Barafu kwa tafakari tunduizi...
 
Sawa sio mapya. .
Mbona yeye tu ndio huwa anatushushia hizi nondo na sio wewe! ?
Just appreciate mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naona uliisoma comment yangu kwa mrengo wa jazba,mkuu barafu namkubali sana na hata yeye analijua hilo na nishamweleza mara kedekede.nilikuwa najaribu kumwelekeza mdau aliyekuwa anahoji hayo mambo anayapata wapi.na nikweli sio mapya sababu ni historia na nikamshauri aendelee kudurusu atajifunza mengi zaidi.Pia sio wote tuna uwezo wa uandishi kuweza kufikisha jambo likaeleweka na kumvutia msomaji ila nondo zipo za kutosha,na sio wote waliousoma uzi huu walikuwa hawayajui hayo yaloandikwa.ila bado unapitia tena na kujifunza zaidi so thats thats no offense.
 
Tupo pamoja...Tuendelee kujadiliana mkuu ktk jukwaaletu pendwa
 
Ki ukweli nimepata elimu ya historia bila kulipa ada!!

Williamson nilikuwa nasikia story zake juu juu kumbe angalau alikuwa mzungu mwenye akili na upendo

Mi naona kama noma na iwe noma tu, tutaifishe migodi yote hata kama watatubania mitambo na kuleta figisu soko la dunia tutaanza moja kuliko kuendelea kuwatengenezea bajeti kubwa ya serikali zao halafu bakaa wanatupa kama msaada tena kwa kutunanga

Kwa wale mliosimuliwa maisha ya Libya ya Gaddafi jinsi kulivyokuwa kuzuri hata wengi kupata wivu na kiu ya maisha yale ingawa Gaddafi alikuwa akijinufaishaakijinufaisha kwa kiwango cha juu ( wizi wenye upendo). Wahenga walisema UKITAKA KULA NA KIPOFU USIMSHIKE MKONO.....ndivyo ilivyokuwa LIFE ya Mwadui kabla ya miaka 90.
Williamson na timu yake walikuwa wanatuibia bila sisi kujijua. Ukimweleza kijana/ mtu aliyezaliwa na kuanzia maisha Mwadui township kuwa Williamson na timu yake walikuwa WEZI hatokuelewa, ni sawa kuwaambia Walibya kuwa Gaddafi alikuwa mwizi. Huyu jamaa ALIJUA KULA KIPOFU.
Hawa Petra na vibaraka wao (walioko serikalini) ndio MIJIZI.....ingawa hii vita ni ngumu acha tupambane labda tutashinda miaka 10-15 ijayo.
Tumeibiwa kiasi cha kutosha, sasa tuamke, NIA tunayo,SABABU tunayo labda uwezo wa kupambana nao.
 
Na kwa kweli Williamson alijua kula na kipofu
 
Mkuu naona uliisoma comment yangu kwa mrengo wa jazba,mkuu barafu namkubali sana na hata yeye analijua hilo na nishamweleza mara kedekede.nilikuwa najaribu kumwelekeza mdau aliyekuwa anahoji hayo mambo anayapata wapi.na nikweli sio mapya sababu ni historia na nikamshauri aendelee kudurusu atajifunza mengi zaidi.Pia sio wote tuna uwezo wa uandishi kuweza kufikisha jambo likaeleweka na kumvutia msomaji ila nondo zipo za kutosha,na sio wote waliousoma uzi huu walikuwa hawayajui hayo yaloandikwa.ila bado unapitia tena na kujifunza zaidi so thats thats no offense.
Pamoja kiongozi. ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andiko hili lisichukuliwe kama ni uwoga au ukibaraka wa mabeberu,bali ukweli na uhalisia juu ya biashara ya madini ya vito duniani.Uzalendo ni pamoja na kuambiana ukweli na uhalisia wa kile dunia inachokijua.

Mara moja tulijadiliana hapa juu ya fitna na hujuma za biashara ya madini duniani.Mjadala niliouleta ulikuwa ni juu ya "wamiliki" wa madini ya almasi duniani na wale wa dhahabu.Kupitia uzi huu
Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere
tulijadiliana juu ya familia mbili za kiyahudi "zilizojimilikisha" madini katika ardhi ya dunia hii,almasi ikiwa chini ya De-Beers Co. Ltd na dhabahu ikiwa chini ya Barrick Gold Corporation.

Hawa De Beers wanaamini,popote katika ardhi ya dunia hii,almasi ni mali ya familia yao.Hii ni familia ya Oppenheimer,Wayahudi wenye makazi yao katika ardhi ya Afrika Kusini.Ujio wao Kusini mwa Afrika,ilikuwa ni kuifuata almasi ya Kimberley ambayo,kwayo ni "mali" yao.

Hao Petra Diamond wa Mwadui ni kama "vibaraka" tu wa De-Beers Co.Ltd,almasi yote inayochimbwa Mwadui inaenda mikononi mwa De-Beers ambao toka mwaka 1950's walikuwa na 50% ya hisa za mgodi wa Mwadui,kutaifishwa kwa mzigo wao uwanja wa ndege Dsm,kunawakumbusha machungu ya safari ya damu na jasho walioianza miaka 100 iliyopita katika sekta ya madini ya almasi.Hawatakaa kimya

Hapo kabla katika ulimwengu wa madini,madini ya vito kama almasi hayakuwa na thamani yoyote,iwe katika soko la dunia au katika uhitaji wa kutengeneza urembo.Dhahabu ilikuwa ndio kila kitu,dhahabu ilikuwa ni alama ya utajiri,ufahari,urembo na utanashati miongoni mwa matajiri na wafalme wa Ulaya na Afrika.Kutokea "Gold Coast" magaharibi mwa Afrika (Sudanic States) mpaka Uyunani,Ulaya ya Mapinduzi ya viwanda, Amerika ya Kaskazini mpaka Vatican ya Kanisa Katoliki,ufahari ilikuwa ni dhahabu.

Kampuni ya De-Beers iliamua kuanzisha kampeni maalumu kuhakikisha kuwa almasi inapata umaarufu wa kibiashara katika dunia.De-Beers wakaamua kuiweka almasi ya Afrika Kusini kama alama ya upendo,utajiri na ufahari wa watu wote duniani,kwa watu maarufu kama wafalme na malkia.Lengo la De -Beers ilikuwa ni ile leo Clouds Media wanaita "Fungua Fursa".Kuongeza thamani ya almasi katika soko la dunia.

Haikuwa kazi rahisi,kuchukua soko la dhahabu na kuiweka almasi kama mbadala wa ufahari,utajiri na alama ya upendo kwa wapendanao duniani.Ilikuwa ni vita ya kibiashara,vita ya jasho na damu,utu na uhai,vita ambayo haikuwaacha watu wengine waliokuwa kama kuzuizi salama.Hii ni vita ambayo De-Beers walijimilikisha,wakaifanya almasi kuwa "fahari" katika urembo,utajiri na alama ya ufalme na umalkia.Gharama ya majitoleo haya ya De-Beers,huwa hayamuachi mtu salama anayeingia kwenye maslahi yao.

Ili kufikia lengo lao,mwaka 1938,Harry Oppenheimer mmiliki wa De-Beers Co.Ltd aliingia mkataba na kampuni ya matangazo ya N.W.Ayer & Son ya jijini New York,Marekani.Lengo ilikuwa ni kuhakikisha Wamarekani na dunia yote wanahamisha mawazo yao toka kwenye madini mengine na kutazama almasi ya Afrika Kusini kama ndio madini ya vito yenye thamani na ufahari.Haikuwa kazi rahisi kwa kampuni ya N.W.Ayer & Son,ilikuwa ni mapambano ya "jasho na damu" ili kuiweka almasi katika macho ya dunia.

Mwaka 1943,Kampuni ya N.W.Ayer & Son ilimpa kazi mwanamke aitwaye Frances Gerety,kazi yake ikawa ni kuhakikisha almasi ya De-Beers inatangazwa duniani na kuteka soko la dunia.Gerety hakuwa na kazi nyingine,bali kuhakikisha kuwa almasi inatamkika na watu wote,kuanzia masikini mpaka matajiri,wafalme pamoja na malkia.

1947,Gerety akawasilisha "kauli mbiu" ya kuitambulisha almasi duniani,ambayo mpaka leo ndio kama motto wa kampuni ya De-Beers na ndio [HASHTAG]#tag[/HASHTAG] yao katika mitandao kama Tweeter nk.Hii ni kauli ya "A DIAMOND IS FOREVER".

Slogan hii ilianza kama mzaha,lakini baadae ikaenea kwa kasi,kwamba "A Diamond is forever".Kauli ikasambaa na Wamarekani wakaiona katika majarida,magazeti,Tv na Radio zao.Ikaingia akilini kwa wengi kuwa almasi ni alama ya utajiri,upendo wa pete ya umpendaye,alama ya ufalme,urembo na fahari pindi ivaliwapo.

N.W.Ayer & Son wakatumia vyombo vya habari na wasanii wa Hollywood kuitangaza almasi huku wakiwa na msemo wao wa "A Diamond is Forever".Kufukia mwaka 1950's, Wamarekani 55% wakawa wanatumia almasi kama pete za uchumba na harusi.Mauzo ya almasi yakapanda maradufu,na malengo ya De-Beers yakawa yamefanikiwa kwa asilimia kubwa sana.

De-Beers kama "Client" wa N.W.Ayer & Son,baada ya kupewa "slogan" hii waliandika katika taarifa zao "De Beers Consolidated Mines Ltd., owner of diamond workings in South Africa, plans a fall campaign in leading national magazines which will stress the engagement-ring tradition. Four-color ads will reproduce paintings by well-known artists and carry the slogan 'a diamond is forever.' N.W. Ayer & Sons, Inc., Philadelphia, is the agency."

Kwenye report yao ya kiabishara,N.W.Ayer & Son ya mwaka 1951,waliandika "Our 1951 annual report, N. W. Ayer noted that, for a number of years we have found evidence that the diamond engagement ring tradition is consistently growing stronger. Jewelers now tell us ‘a girl is not engaged unless she has a diamond engagement ring.’ ”

Almasi ikachanganya sana katika soko la dunia,De-Beers wakawa wamefanikiwa sana.Almasi ya Afrika Kusini ikawa inatajwa sana katika soko la dunia.Ile ya Mwadui Shinyanga,mgodi wa Dr John Williamson ikawa haisikiki sana.Dr Williamson hakukaa kimya,na yeye alitumia mbinu yake kuitangaza almasi yake katika dunia(Wakati huo De-Beers wakiwa hawajampoka 50% ya mgodi wake)

1948,Dr Williamson akishauriana na mshirika wake wa kibiashara na mwanasheria wake Iqba Chandi Chopra aliyekuwa anakaaa Mwanza,waliamua kuchukua almasi ya "pink" ya uzito wa carat 23.6 na kumpa Princess Elizabeth ili kuitangaza zaidi almasi ya Mwadui na kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia(Almasi hiyo huvaliwa na Malkia wa Uingereza sehemu ya kushoto mwa bega lake).Hii ikafanya soko la almasi liimalike na litangazike,sasa ikawa ni "vita" ya almasi ya Afrika Kusini na almasi ya Mwadui.Matokeo ya vita hivi,tuliyajadili katika uzi huu

Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere
De-Beers wakatumia njia nyingi kuendelea kujitangaza.Mwaka 1956,Ian Fleming alidhaminiwa na De-Beers na kuandika kitabu cha "A Diamond is Forever",baadae wakaisimamia James Bond Series ya "A Diamond is Forever",mtengeneza filamu na maandalizi ya mapambo ya filamu hiyo akatunzwa tuzo iliyoandaliwa na De-Beers Annual Diamond Award.

Mwaka 1999,Slogan ya "A diamond is forever" ikapata tuzo ya "Slogan of the Century" kutoka "Advertising Ages".Mwaka 2005,hawa De- Beers Co.Ltd walikuwa na support kubwa ya kifedha nyuma ya wimbo wa Kanye West wa "Diamond From Siera Leone",na wimbo huu uliandandaliwa "kimkakati" ili kuijibu movie ya "Blood Diamond" ambayo ililenga kuwachafua wafanya biashara wa madini ya almasi.

Kanye West akatumika kuisafisha De-Beers na kupigia debe biashara ya almasi,ndio maana sehemu ya mistari ya West inasema "Please Purchase Conflicts free diamond";na mwanzoni mwa wimbo wake pale unapoanza tu,yanatokea maandishi yanasema "Little is known of Siera Leone,and how it connects to the diamonds".Hii yote ni kazi ya De-Beers wenye almasi zao. De-Beers wakamzawadia Kanye West pete ya almasi yenye uzito wa carat 15 ili amvalishe mpenzi wake Kim Kardashian.

Mpaka sasa,kwenye "Business and Marketing Classes" katika vyuo vikubwa kama New York University na The University of Massachusetts,slogan ya "A diamond is forever" hutumika kama "Case Study" ya moja kati ya slogan za kibiashara zilizofanikiwa sana.Maprofesa na Wahadhiri waandamizi huitukia sana katika kufundisha kwao.Si ajabu ukakutana na swali linasema "A dimond is Forever.Discuss in reference to De-Beers Co.Ltd"

Jitihada hizi za De-Beers kuliteka soko la almasi la dunia,kwa jasho na damu,zinaifanya kampuni ya De-Beers ambayo tumetaifisha almasi yao uwanja wa ndege Dsm,kuwa ndio "Monopoly and Monopsony" wa soko la almasi duniani.Walio na ABC ya Uchumi,wataelewa tunaposema "Monopoly na Monopsony of the diamond market",inamaanisha nini.

Kuitaifisha almasi yao,haliwezi kuwa jambo dogo na la kawaida katika ulimwengu wa biashara ya madini.Iwe ni katika soko la hisa London,New York,Japan na Australia.Mtikisiko wenye mwangwi utakaofika mpaka Tanzania lazima usikike.Hawa wanajua walipoitoa hii "almasi yao".Ni lazima patakuwa na mapambano ya jasho na kukamiana

Usishange almasi ya Mwadui ikapigwa "ramli nyekundu" ikawa haiwezi kununulika wala kuwekwa hata "bond" popote duniani.Ni ukweli unaouma kuwa,hata tukiwa na tani 100 za almasi,kama huko duniani hao wenye "monopoly na monopsony" wamekaza,hakuna tutakapopenya.

Jambo hili lisitutie woga,jambo hili lisitutie wasiwasi na kutukatisha tamaa.Tupambane na Rais wetu kuhakikisha sheria zetu za mambo ya madini zinabadilika.Wale waliotuingiza kwenye majanga haya wanawajibishwa na mwisho wa siku,tunakaa mezani na "wenye madini yao" na kufanya biashara ya "win to win" kama wenzetu Bostwana.Tukitaifisha tu bila kuwa na mbadala,tutabaki na viroba vya almasi uvunguni mwetu,wakati tunapiga miayo kwa njaa.Kushinda njaa wakati una chakula ndani sio ushujaa.Tuchukue hatua

barafu wa Jf

Umeona mbali!
Umenukumbusha kisa cha Marehemu Nyerere na Tan Cut Almasi! Tulishindwa kuuza almasi ya Mwadui pamoja na kuikata! Wenye soko huko Belgium huwa hawanunui diamond from despots kumbuka almasi ya Sierra Leon ilivyowatesa! The bloody diamonds. Labda iliyotaifishwa ifanywe mapambo na mtakatifu. Kuna haja ya kupitia mkataba kuhusu mauzo na valuation provisional ilifanyika kwa criteria ipi? Nafikiri pupa haitusaidii ngosha ashauriwe kuwa na kifua kila kitu Tanzania ni bomu. Makosa yaliyofanyika awamu ya kwanza yanajirudia awamu ya nne. Pasipo kuwashirikisha wadau and the public at glance ubaguzi hasn't worked anywhere kumbuka mafuta ya Venezuela , Nigeria, Iraq , Libya utajikuta we go back to square one !
 
Hapo ndio tunapokosea...Hatushauriani vizuri
 
Acha uoga wewe, almasi yetu na ardhi yetu...hawataki masharti yetu wakachimbe barafu huko Atlantika
 
Acha uoga wewe, almasi yetu na ardhi yetu...hawataki masharti yetu wakachimbe barafu huko Atlantika
Unanini wewe wakati umepata uhuru kutoka kwa ngozi nyeupe....unazinduka leo wakati hata kutengeneza kifungo cha shati shida hahahahaha....Barafu kaja na old skool ya ukweli...angalia hata alivyoanza....sio unajambajamba tu...muelewe mshkaji alichoongea.
 
Hawa watu wa chato hawawajui vema mabeberu?
Eh wakataifishe alafu wao wasije taifishwa kama Gaddafi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom