Tujipange: Kutaifishwa mzigo wa almasi Airport ni mwanzo wa vita ya kibiashara kati ya Tz na De-Beers

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Andiko hili lisichukuliwe kama ni uwoga au ukibaraka wa mabeberu,bali ukweli na uhalisia juu ya biashara ya madini ya vito duniani.Uzalendo ni pamoja na kuambiana ukweli na uhalisia wa kile dunia inachokijua.

Mara moja tulijadiliana hapa juu ya fitna na hujuma za biashara ya madini duniani.Mjadala niliouleta ulikuwa ni juu ya "wamiliki" wa madini ya almasi duniani na wale wa dhahabu.Kupitia uzi huu
Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere
tulijadiliana juu ya familia mbili za kiyahudi "zilizojimilikisha" madini katika ardhi ya dunia hii,almasi ikiwa chini ya De-Beers Co. Ltd na dhabahu ikiwa chini ya Barrick Gold Corporation.

Hawa De Beers wanaamini,popote katika ardhi ya dunia hii,almasi ni mali ya familia yao.Hii ni familia ya Oppenheimer,Wayahudi wenye makazi yao katika ardhi ya Afrika Kusini.Ujio wao Kusini mwa Afrika,ilikuwa ni kuifuata almasi ya Kimberley ambayo,kwayo ni "mali" yao.

Hao Petra Diamond wa Mwadui ni kama "vibaraka" tu wa De-Beers Co.Ltd,almasi yote inayochimbwa Mwadui inaenda mikononi mwa De-Beers ambao toka mwaka 1950's walikuwa na 50% ya hisa za mgodi wa Mwadui,kutaifishwa kwa mzigo wao uwanja wa ndege Dsm,kunawakumbusha machungu ya safari ya damu na jasho walioianza miaka 100 iliyopita katika sekta ya madini ya almasi.Hawatakaa kimya

Hapo kabla katika ulimwengu wa madini,madini ya vito kama almasi hayakuwa na thamani yoyote,iwe katika soko la dunia au katika uhitaji wa kutengeneza urembo.Dhahabu ilikuwa ndio kila kitu,dhahabu ilikuwa ni alama ya utajiri,ufahari,urembo na utanashati miongoni mwa matajiri na wafalme wa Ulaya na Afrika.Kutokea "Gold Coast" magaharibi mwa Afrika (Sudanic States) mpaka Uyunani,Ulaya ya Mapinduzi ya viwanda, Amerika ya Kaskazini mpaka Vatican ya Kanisa Katoliki,ufahari ilikuwa ni dhahabu.

Kampuni ya De-Beers iliamua kuanzisha kampeni maalumu kuhakikisha kuwa almasi inapata umaarufu wa kibiashara katika dunia.De-Beers wakaamua kuiweka almasi ya Afrika Kusini kama alama ya upendo,utajiri na ufahari wa watu wote duniani,kwa watu maarufu kama wafalme na malkia.Lengo la De -Beers ilikuwa ni ile leo Clouds Media wanaita "Fungua Fursa".Kuongeza thamani ya almasi katika soko la dunia.

Haikuwa kazi rahisi,kuchukua soko la dhahabu na kuiweka almasi kama mbadala wa ufahari,utajiri na alama ya upendo kwa wapendanao duniani.Ilikuwa ni vita ya kibiashara,vita ya jasho na damu,utu na uhai,vita ambayo haikuwaacha watu wengine waliokuwa kama kuzuizi salama.Hii ni vita ambayo De-Beers walijimilikisha,wakaifanya almasi kuwa "fahari" katika urembo,utajiri na alama ya ufalme na umalkia.Gharama ya majitoleo haya ya De-Beers,huwa hayamuachi mtu salama anayeingia kwenye maslahi yao.

Ili kufikia lengo lao,mwaka 1938,Harry Oppenheimer mmiliki wa De-Beers Co.Ltd aliingia mkataba na kampuni ya matangazo ya N.W.Ayer & Son ya jijini New York,Marekani.Lengo ilikuwa ni kuhakikisha Wamarekani na dunia yote wanahamisha mawazo yao toka kwenye madini mengine na kutazama almasi ya Afrika Kusini kama ndio madini ya vito yenye thamani na ufahari.Haikuwa kazi rahisi kwa kampuni ya N.W.Ayer & Son,ilikuwa ni mapambano ya "jasho na damu" ili kuiweka almasi katika macho ya dunia.

Mwaka 1943,Kampuni ya N.W.Ayer & Son ilimpa kazi mwanamke aitwaye Frances Gerety,kazi yake ikawa ni kuhakikisha almasi ya De-Beers inatangazwa duniani na kuteka soko la dunia.Gerety hakuwa na kazi nyingine,bali kuhakikisha kuwa almasi inatamkika na watu wote,kuanzia masikini mpaka matajiri,wafalme pamoja na malkia.

1947,Gerety akawasilisha "kauli mbiu" ya kuitambulisha almasi duniani,ambayo mpaka leo ndio kama motto wa kampuni ya De-Beers na ndio [HASHTAG]#tag[/HASHTAG] yao katika mitandao kama Tweeter nk.Hii ni kauli ya "A DIAMOND IS FOREVER".

Slogan hii ilianza kama mzaha,lakini baadae ikaenea kwa kasi,kwamba "A Diamond is forever".Kauli ikasambaa na Wamarekani wakaiona katika majarida,magazeti,Tv na Radio zao.Ikaingia akilini kwa wengi kuwa almasi ni alama ya utajiri,upendo wa pete ya umpendaye,alama ya ufalme,urembo na fahari pindi ivaliwapo.

N.W.Ayer & Son wakatumia vyombo vya habari na wasanii wa Hollywood kuitangaza almasi huku wakiwa na msemo wao wa "A Diamond is Forever".Kufukia mwaka 1950's, Wamarekani 55% wakawa wanatumia almasi kama pete za uchumba na harusi.Mauzo ya almasi yakapanda maradufu,na malengo ya De-Beers yakawa yamefanikiwa kwa asilimia kubwa sana.

De-Beers kama "Client" wa N.W.Ayer & Son,baada ya kupewa "slogan" hii waliandika katika taarifa zao "De Beers Consolidated Mines Ltd., owner of diamond workings in South Africa, plans a fall campaign in leading national magazines which will stress the engagement-ring tradition. Four-color ads will reproduce paintings by well-known artists and carry the slogan 'a diamond is forever.' N.W. Ayer & Sons, Inc., Philadelphia, is the agency."

Kwenye report yao ya kiabishara,N.W.Ayer & Son ya mwaka 1951,waliandika "Our 1951 annual report, N. W. Ayer noted that, for a number of years we have found evidence that the diamond engagement ring tradition is consistently growing stronger. Jewelers now tell us ‘a girl is not engaged unless she has a diamond engagement ring.’ ”

Almasi ikachanganya sana katika soko la dunia,De-Beers wakawa wamefanikiwa sana.Almasi ya Afrika Kusini ikawa inatajwa sana katika soko la dunia.Ile ya Mwadui Shinyanga,mgodi wa Dr John Williamson ikawa haisikiki sana.Dr Williamson hakukaa kimya,na yeye alitumia mbinu yake kuitangaza almasi yake katika dunia(Wakati huo De-Beers wakiwa hawajampoka 50% ya mgodi wake)

1948,Dr Williamson akishauriana na mshirika wake wa kibiashara na mwanasheria wake Iqba Chandi Chopra aliyekuwa anakaaa Mwanza,waliamua kuchukua almasi ya "pink" ya uzito wa carat 23.6 na kumpa Princess Elizabeth ili kuitangaza zaidi almasi ya Mwadui na kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia(Almasi hiyo huvaliwa na Malkia wa Uingereza sehemu ya kushoto mwa bega lake).Hii ikafanya soko la almasi liimalike na litangazike,sasa ikawa ni "vita" ya almasi ya Afrika Kusini na almasi ya Mwadui.Matokeo ya vita hivi,tuliyajadili katika uzi huu

Vita dhidi ya mabepari wa madini inahitaji umoja, ilimshinda Dr Williamson wa Mwadui na Mwl Nyerere
De-Beers wakatumia njia nyingi kuendelea kujitangaza.Mwaka 1956,Ian Fleming alidhaminiwa na De-Beers na kuandika kitabu cha "A Diamond is Forever",baadae wakaisimamia James Bond Series ya "A Diamond is Forever",mtengeneza filamu na maandalizi ya mapambo ya filamu hiyo akatunzwa tuzo iliyoandaliwa na De-Beers Annual Diamond Award.

Mwaka 1999,Slogan ya "A diamond is forever" ikapata tuzo ya "Slogan of the Century" kutoka "Advertising Ages".Mwaka 2005,hawa De- Beers Co.Ltd walikuwa na support kubwa ya kifedha nyuma ya wimbo wa Kanye West wa "Diamond From Siera Leone",na wimbo huu uliandandaliwa "kimkakati" ili kuijibu movie ya "Blood Diamond" ambayo ililenga kuwachafua wafanya biashara wa madini ya almasi.

Kanye West akatumika kuisafisha De-Beers na kupigia debe biashara ya almasi,ndio maana sehemu ya mistari ya West inasema "Please Purchase Conflicts free diamond";na mwanzoni mwa wimbo wake pale unapoanza tu,yanatokea maandishi yanasema "Little is known of Siera Leone,and how it connects to the diamonds".Hii yote ni kazi ya De-Beers wenye almasi zao. De-Beers wakamzawadia Kanye West pete ya almasi yenye uzito wa carat 15 ili amvalishe mpenzi wake Kim Kardashian.

Mpaka sasa,kwenye "Business and Marketing Classes" katika vyuo vikubwa kama New York University na The University of Massachusetts,slogan ya "A diamond is forever" hutumika kama "Case Study" ya moja kati ya slogan za kibiashara zilizofanikiwa sana.Maprofesa na Wahadhiri waandamizi huitukia sana katika kufundisha kwao.Si ajabu ukakutana na swali linasema "A dimond is Forever.Discuss in reference to De-Beers Co.Ltd"

Jitihada hizi za De-Beers kuliteka soko la almasi la dunia,kwa jasho na damu,zinaifanya kampuni ya De-Beers ambayo tumetaifisha almasi yao uwanja wa ndege Dsm,kuwa ndio "Monopoly and Monopsony" wa soko la almasi duniani.Walio na ABC ya Uchumi,wataelewa tunaposema "Monopoly na Monopsony of the diamond market",inamaanisha nini.

Kuitaifisha almasi yao,haliwezi kuwa jambo dogo na la kawaida katika ulimwengu wa biashara ya madini.Iwe ni katika soko la hisa London,New York,Japan na Australia.Mtikisiko wenye mwangwi utakaofika mpaka Tanzania lazima usikike.Hawa wanajua walipoitoa hii "almasi yao".Ni lazima patakuwa na mapambano ya jasho na kukamiana

Usishange almasi ya Mwadui ikapigwa "ramli nyekundu" ikawa haiwezi kununulika wala kuwekwa hata "bond" popote duniani.Ni ukweli unaouma kuwa,hata tukiwa na tani 100 za almasi,kama huko duniani hao wenye "monopoly na monopsony" wamekaza,hakuna tutakapopenya.

Jambo hili lisitutie woga,jambo hili lisitutie wasiwasi na kutukatisha tamaa.Tupambane na Rais wetu kuhakikisha sheria zetu za mambo ya madini zinabadilika.Wale waliotuingiza kwenye majanga haya wanawajibishwa na mwisho wa siku,tunakaa mezani na "wenye madini yao" na kufanya biashara ya "win to win" kama wenzetu Bostwana.Tukitaifisha tu bila kuwa na mbadala,tutabaki na viroba vya almasi uvunguni mwetu,wakati tunapiga miayo kwa njaa.Kushinda njaa wakati una chakula ndani sio ushujaa.Tuchukue hatua

barafu wa Jf
 
Kwa nini Namibia na Botswana wanafanikiwa katika biashara ya almasi kama nchi wakati sisi tunaambulia patupu..? Huko pia wachimbaji na wanunuzi wakubwa ni hao hao De Beers. Au wana akili na uzalendo kuliko sisi..???
The problem is how you handle the situation , dunia haiendeshwi tu kwa fikra za mtu mmoja tena duni kutoka Tanzania .
 
image.jpeg
image.jpeg
Kwa nini Namibia na Botswana wanafanikiwa katika biashara ya almasi kama nchi wakati sisi tunaambulia patupu..? Huko pia wachimbaji na wanunuzi wakubwa ni hao hao De Beers. Au wana akili na uzalendo kuliko sisi..???
Ni uzalendo wa wale wanaowatuma kwenda kujadiliana juu ya mikataba ya madini.
Tazama upande wa kushoto wa bega la Malkia....Hiyo ni almasi kutoka katika ardhi ya Mama Tanzania,iliyochimbwa na kijana mmoja wa kisukuma...Ambaye mpaka sasa hana uhakika wa huduma bora za maji achilia mbali afya!!Ni uzalendo Uzalendo Uzalendo....Wale tuliowaamini wanatuchuuza Mkuu Kop
 
Mkuu umeongea kila, kitu what I like most, you go beyond the borders, ujue washamba hawana mda wa Ku reason, wanajiamulia tu.


Kubalini mkatae, dunia tuliikuta, tulikuta watu, na watu ni kama wewe, Acheni ujuaji nyie watu msiojulikana.
Fanyeni mambo kisomi, hakuna ubabe unaoshinda

Mkuu barafu shukrani kwa nondo muhimu , week end njema
 
Umesema ukweli mchango..
Lakini Rais wetu anajitahidi kupambana inatakiwa tumuunge mkono maana mabepari kila siku wanakuja na mbinu mpya...

Tanzania sasa inasimama na pia hii inatoa alerts kwamba Tanzania ya sasa siyo kama ya awamu mbili au Tatu zilizopita..

Endelea kupambana Rais najua upo humu na mawazo ya watu yachukue na uyathimini kabla ujayatekeleza maana Muda mwingine unakurupuka mno. Ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom