Tujikumbushe ya Vijijini Kwetu

Tujikumbushe ya Vijijini Kwetu

Kijiji kwetu ukiongea English hata cha kunywa maji tu.. tuna kupa cheo cha mwenyekiti wa kijiji
 
nakumbuka miaka ya 90 sikuku ya wakulima walikua wana nunua ng'ombe na kugawana kijiji kizima kupitia mabalozo wa nyumba kumi
 
Unaikumbuka ile ukiwa mdogo unakabidhiwa kwa konda afu kule town ndugu wanakuja kukupokea.

hiyo mkuu bado ipo! watu bado wanakuja dar es salaam kwa kukabidhiwa kwa konda! lol
 
nakumbuka miaka hiyo ,jamaa alifaulu darasa la saba akapangiwa mzumbe sec,huyo ni mwanafunzi wa kwanza kusoma sec,aliporudi likizo jamaa akawa anapiga difinition ya biology na geography tu siku nzima basi kijiji kizima wakawa wanamsifu jamaa anaweza kingereza baraha ,mda,wote anaongea kiingereza tu
 
Kijijini kwetu wanawake wenye hela huoa mabinti na kuwaruhusu wakananilihi na wanaume ila watoto ni mali ya mwanamke aliyeoa. Inaitwa nyumba ntobho
 
Kijijini kwetu watu wote mnaoga pamoja mtoni,,,wanawake kwa juu na wanaume kwa chini,,,dahhhhhh
 
Kwetu mgeni ukitaka kwenda chooni unapewa jembe uende kichakani
 
Back
Top Bottom