Tujikumbushe ya Vijijini Kwetu

Tujikumbushe ya Vijijini Kwetu

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
Kijijini kwetu huwezi kuwa kiongozi kama huna VIATU.....................kwa maana nyingine ukineda na viatu unachaguliwa kiongozi kwa urahisi

Kijijini kwenu kuna ushamba gani?
 
Kijini kwetu mbu ni wakubwa kama vifaranga vya kuku, vyandarua vyetu ni kwa oda maalum maana matundu yake ni kama yale ya matenga
 
Kijijini kwetu tunakula ugali kwa picha ya samaki
 
Darasa nililosoma kijijini kwetu hakukua na mwanafunzi mwenye kiatu lakini miguu ilikua inan'gaa muda wote sababu ya kujipaka sabuni ya mipapai
 
Mlikua mkifika na basi abiria wote mnaenda kumwambia dereva asante.
pia tunavyoenda sehemu ata barabara iwe pana mkubwa ndo anatangulia mbele as if mstari wa benk.
halafu kila ikifika jioni tukiwa tumetoka shamba kwenda kilabuni kuskiliza na kuanggalia watu wanavyocheza muziki hata kama sio walevi, redio inatumia betri la gari.
 
Mlikua mkifika na basi abiria wote mnaenda kumwambia dereva asante.
kila ikifika jioni tukiwa tumetoka shamba kwenda kilabuni kuskiliza na kuanggalia watu wanavyocheza muziki hata kama sio walevi, redio inatumia betri la gari.
sisi taarifa ya habari na matangazo ya vifo tuliruhusiwa kusikilizia kwa mjumbe
 
Mlikua mkifika na basi abiria wote mnaenda kumwambia dereva asante.
.
umenikumbuasha staili ya kutuma barua/hela KWA KUMPA KONDA, sitasahau siku ambayo nilimpa hela halafu gari likapinduka
 
Unaikumbuka ile ukiwa mdogo unakabidhiwa kwa konda afu kule town ndugu wanakuja kukupokea.
 
Unaikumbuka ile ukiwa mdogo unakabidhiwa kwa konda afu kule town ndugu wanakuja kukupokea.
kuna konda aliambiwa akifika Morogoro amstue dogo akasahau, walipofika Mikumi akataka ampakie kwenye gari arudi akashangaa dogo anafungua menyu...............
 
Kijijini kwetu dish la satellite [ ungo] limefungwa juu ya nyumba ya nyasi (mbavu za mbwa). Nje imepaki vx,bodaboda 2.
 
ole wako kiongozi wa kijiji afike na usimpishe kiti cha mbele kwa dereva
 
Back
Top Bottom