Ipi dot com
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 306
- 166
- Thread starter
- #41
Sawa mkuuPoa poa jitahd ata ziwe post 4 au tano mzee baba per day
Sent from my SM-J730G using JamiiForums mobile app

Huwezi amini mkuuHatari story yako Mungu alisimamia kila kitu asee
Daaah hii movie nnInaendelea...
Hapo nipo ofisi za uhamiaji yule officer alienirudisha zimbabwe nipo kwake tena safari hii anataka show money,na mimi sina, akaniambia vinginevyo huingii Botswana nikachanganyikiwa safari hii ilikuwa zaidi nikawa najiuliza nitapata msaada wapi tena?
Nikaamua kuwa kichaa zaidi nikamfokea sana nikamuuliza una nini na mimi sikumbuki maneno mengine lakini nadhani nilinena kwa lugha(joke)
Mala akanigongea muhuri wa kuniruhusu akiwa na hofu kwa jinsi nilivyobadilika
Sura. Mdogo mdogo nikalielekea lilipo basi tayari kwa safari kwenda Gaberone.
Safari iliendelea tukafika Gaberone alfajiri nikiwa na Mtanzania mwenzangu ambaye baadae nikajua jina lake Ramadhan
Asubuhi tukiwa jijini hatujui wapi pa kuanzia lakini mwenzangu alikuwa akinipa moyo kutokana na vyeti alivyonavyo akiwa na imani kwamba ataanza kupata kazi yeye na atanisaidia
Kumbuka safari yangu ni kwenda SA pale Botswana nina siku tisini tu za kukaa.
Taswila tuliyokuwa kuwa nayo juu ya Gaberone tuliona kama jiji kuubwa kuliko hata Dar, tukajikuta kila tukienda huku tuko nje ya mji yaani mji ni mdogo.
Baada ya mizunguko jioni ikafika hatuna pa kulala na wakati huo ulikuwa ni mwezi mtukufu wa ramadhani, jamaa yangu rama akanishauri twende msikitini tukalale pale, lakini wakati tunatafakari tulikuwa bado tunazurula mtaani nikatoa wazo tofauti.
Nikamwambia moyo unanisukuma twende hiyo nyumba tujieleze kuwa tunatafuta kazi kisha tutawalekeza kuwa tupo msikitini ilikuwa kama saa mbili kasoro usiku,kwa vile pale palionekana kuna ujenzi unaendelea, jamaa kakubali tukajisogeza pale tukagonga hodi ghafla nikaona jambo ambalo sikulitegemea aliekuja kufungua mlango ni john tulieachana nae boda ya Botswana mara ya kwanza. nae aliponiona alifunga mlango kabla hatujaingia nikawa kama naota...
Tutaendelea kesho..
Sent from my SM-J730G using JamiiForums mobile app
Mmeingia mikononi kwa kunguruTuendelee..
Kumbe ndani ya ile nyumba walikuwa na mjadala mrefu kuhusu mimi kwa hiyo aliponiona alitahayari na kurudi ndani kuwaeleza kuwa nipo nje.
Alikuja mwenyeji na mke wake wakanihug nikashindwa kuelewa nini kinachoendelea baadae ndio tukapata kujua nini kilimtokea kila mmoja wetu na sasa tupo na rama maisha yaliendelea huku mimi na john tunaendelea kukusanya chochote kwa ajili ya kwenda SA.
Siku moja alikuja ndg mmoja alitoka SA lakini ni mzambia baada ya maongezi mengi alituachia bussness card yake lakini alitusihi kwamba baada ya muda twende SA
Akatuhakikishia atatupa support,ule mwaliko wake hatukuutilia maanani maana tuliamini tungeweza bila msaada wake.
Siku zilivyokaribia kuisha za kukaa Botswana presha ya kuondoka kwenda SA ilizidi kuwa juu ukizingatia sheria zao za ujamiaji ni kama zetu yaani kosa la overstay kwao ni jinai hivyo jela inakahusu.
Sasa mimi nilikuwa tayari kuondoka kwa vyovyote vile,maana naona bora ukamatwe SA utarudishwa kwenu kuliko pale,Hapo shughuli nyingine inaanza tena kumbuka hapo tayari tuna marafiki wenyeji kwa hiyo wengi hawataki tuondoke.
John naye kaingia kwenye mtego kawa mvivu kutoka kila siku anatafuta sababu ili tusiondoke,moyoni nikajiapiza kuondoka peke yangu.
Tulikuwa na hela lakini si nyingi sana na kutoka Gaberone mpaka boda ni karibu sana nikatafuta wenyeji wajanja wanipe ramani jinsi ya kuongia SA bila kupita uhamiaji,wakanielekeza kituo cha kushuka wakaniambia kuna vijana pale unawapa chochote wanakuvusha mpk ng'ambo ya pili.
Nikarudi home nikamuaga john kuwa kesho naondoka nakumbuka kulikuwa na mvutano sana usiku mzima asubuhi nikaanza maandalizi alivyoona nipo sirias naye kaanza maandalizi inafika saa tano asubuhi tupo ndani ya gari kwenda boda.
Dreva alijua tunaposhuka maana wao wanaelewa short cut kama huna pass, tukafika mahali penyewe hatukuwa na haraka mpk baada ya muda wakaja vijana wawili wa kiswana wakataka pesa na baadhi ya nguo ili watuvushe.
Kumbuka sisi tunavaa mitumba ya ulaya kwa hiyo vijana wa kule walikuwa wakipenda zile nguo,tukawapatia baadhi ya nguo na pesa wakatuambia tuwafuate tukaanza kupita katika kijiji hicho ambacho nusu kiko botswana na nusu nyingine SA tuka vuka senyenge sasa tukawa SA nikaona ndoto zinaanza kutimia maana safari ya siku mbili sisi tumetumia miezi mitatu.
Wakati huo kijana mmoja anatangulia mbele kama vile anasoma ramani kisha tunamfuata, tukafika barabarani lakini tunakuwa kichakani kidogo hivyo wakawa wanasimamisha magari kila gari imejaa baadae ikaja gari ndogo datsun milango miwili likasimama,jamaa wakamweleza dreva kuwa tunaenda mji uitwao mafikeng jamaa kakubali tukawaaga vijana kwa furaha tukaingia ndani ya gari tukakaa siti ya nyuma mbele walikuwa wawili yaani dreva na mtu mwingine.
Sasa dreva alikuwa akituuliza vitu vingi kuhusu sisi tukaanza kuangaliana na john kengere ya hatari ilingonga, hisia zetu zilithibitika baada ya kusikia radio call duu kumbe ni askari anaeleza mahali alipo na kwamba anatafuta boda jumpers ghafla anatoa kitambusho katurushia..you guys you are under arrest (mko chini ya ulinzi)..
Itaendelea....
Sent from my SM-J730G using JamiiForums mobile app
Duuuh harakati zote hizo mnaishia kwenye mikono ya polisi aiseeTuendelee..

Bado inaendeleaEbana enedeleza wino huu mzee ni balaa
Tulikua pretoria sunnysideMimi nipo naishi huku mkuu nataka kufahamu ulifika MJI gani hapa South Africa