Tujikumbushe UMBWE

Yap Baba Mselle...mzee alikuwa hachekei ufisadi, dizaini flani hivi alikuwa conservative sio kama Tango. Ila kuna yule aliyekuwa Second Master akiitwa "Victor" alikuwa anajisikia kinoma noma...jamaa kutembea ilikuwa kwa maringo, kuongea maringo kweli cheo ni nuksi. Tulikuwa tunamwita "Abacha", maana alikuwa dikteta flani hivi. Kuna siku ametoka kupiga mipombe pombe yake huko Sweken sikumbuki kulikuwa za zali gani pale shule, nashangaa tunapangwa mstari pale basketball court jamaa alikuwa na guts za nguvu akaanza ku mpitia mwanafunzi mmoja mmoja na kumnusa mdomo kama amekunywa pombe ama la. Kweli waalimu wetu walikuwa na muda wa kuchezea.

Dah, umenikumbusha mzee, siku ile nilikuwa zangu uswekeni, kulikuwa na demu wangu mmoja wale wanafunzi wa day, we acha tu, bahati ilikuwa mitaa ya jirani, kuna masela wangu walikuwa wanapiga banana, walichofanya ni kupulizia pafyumu mdomoni, kuondoa harufu! mzee ilikuwa niondoke siku ile!

sikukoma uswekeni.....

waberoya
 
umenikumbushia Msele chalii angu.
nakumbuka accent yake akiwa anahubiri darasani.
'nyie waswahili'.. mke wake alikua mnoko kama nini kutoa dawa pale dispensary.
Nakumbuka Dorm 5 lilikua chafu balaa
 
umenikumbushia Msele chalii angu.
nakumbuka accent yake akiwa anahubiri darasani.
'nyie waswahili'.. mke wake alikua mnoko kama nini kutoa dawa pale dispensary.
Nakumbuka Dorm 5 lilikua chafu balaa

Unamkumbuka mtoto wa MSELE alikuwa anasoma Kibosho girls nafikiri,alikuwa bomba kiaina..Dorm 5 lilikuwa chafu sana,kuna mshikaji mmoja alikuwa kiongozi wa dorm 5 alikuwa na tabia ya kuhifadhi Maharage(baada ya msosi wa jioni) yanalala bwenini halafu asubuhi anayachanganya na uji(lol!!!) mwenyewe alikuwa anayaita MAINI
 
Farida yupo dar ameolewa na mwalimu ,simkumbuki kwa jina huyo mwalimu ila alikuwa anafundisha part time economics A,level, kwa sasa anafanyakazi azina makao makuu,mara kwa mara uwa nakutana na farida anaendesha Eskudo ALX T.....
 
Anaitwa mwalimu MARIDADI
 
Farida yupo dar ameolewa na mwalimu ,simkumbuki kwa jina huyo mwalimu ila alikuwa anafundisha part time economics A,level, kwa sasa anafanyakazi azina makao makuu,mara kwa mara uwa nakutana na farida anaendesha Eskudo ALX T.....

Ogwalumapesa,,umemaliza lini Mti Safi mkuu?????
 
we acha 'kusema ndizi shilingi ngapi kuna mtu alikuwa anajua unasemaje kwa kibosho??

''makundu bese-inga??'' sijui nimepatia.

masela wa dorm 9 mpo?? wajanja,watukutu walikuwa humu,

dah!
 
we acha 'kusema ndizi shilingi ngapi kuna mtu alikuwa anajua unasemaje kwa kibosho??

''makundu besa-inga??'' sijui nimepatia.

masela wa dorm 9 mpo?? wajanja,watukutu walikuwa humu,

dah!

Aisee umenikumbusha mbali sana mkuu! Umenikumbusha pale getini Kanteen. Wale wakina dada/mama waliokuwa miguu peku wakiuza "makunduu" na "maparachichi". That was a good life!
Kuna anayejua Salva "Mzee wa Madili" yuko wapi sasa hivi? Salva alikuwa King Pin wa ku supply mitihani ya Taifa. Ufisadi ulinza siku nyingi.
 
we acha tu mkuu yaani siku hazirudi nyuma ati!

Nilikutana naye mwaka juzi, polisi makao makuu kulikuwa na document anafuatilia, yeye anafanya kazi bandarini DAR.

WABEROYA
 
Namkumbuka sana mzee wawa [mpishi ambaye alikuwa promoted from mlinzi, before that anasema alianzia kwenye kufundisha Geography], siku zote alikuwa akituhimiza tujitahidi tupate divishen 4 [maana ni kubwa kuliko divisheni 1]. Farida nasikia aliolewa na Mwalimu anayekwenda kwa jina la Maridadi.
Hao wanaoshangaa maharage kuwa equivalent na maini watuulize vizuri tulipokula maharage ya nguruwe mwaka 1995/96.

Salva alikuwa Tumaini University [Dar college] mwaka jana, sijui kama amemaliza au la.

Halafu misamiati mingine ukiitumia siku hizi ina maana tofauti kabisa. Kwa mfano neno "kicheche" lilivyotumika Umbwe ni tofauti na linavyotumika siku hizi.

Wale waliomaliza 97 tupeni whereabouts za kika kyaraa, Kiarage, Mnyama, etc.
 
Balantanda
Nimemaliza umbwe A,level 2000,Headmaster Alikuwa Msele ,Academic master alikuwa P M mushi akisaidiwa na Protas,kulikuwa na mkuda mmoja anaitwa Mbise alikuwa mwl wa O.level sijui yupo wap na jamaa langu Sarinjo,Headprefect alikuwa prosper lawrence baadae akamwachia JOSEPH karobe,dorm leader wangu alikuwa machume,na prefect wa usafi na mazingira alikuwa Sango kasera
 
Hahaaaa,basi tulikuwa wote mtu wangu...Sarinjo,Mbise,Protas...lol...Prosper mshikaji wangu sana june nilivoenda Tz likizo nilonana nae... I hope mlikuwa na akina Martina,Kashoka,Mjengi,Ommy BUSTA,SPYTER...Hivi unamkumbuka jamaa mmoja alikuwa aitwa SHANELI na mwingine ZERO BRAIN aka KOSOVO...Kama vp ntakutumia PM mzee
 
Bila kuwasahau Mzee mzima Zagalo(Kinauche),Ras Ezekiel Mgimwa,Kisingi a.k.a Mpendwa, Mangesho,Soldier(Muyanja),Karata mzee wa Misosi,dah nawakumbuka sana jamaa wa Mtisafi
 
Balantanda ulikuwa ECA au HGL?, mie nilikuwa hapo 1994 - 2000 [Both A-level na O-level]. I miss those good moments. I wish pangekuwa na University ningerudi mlemle.
 
Unamkumbuka Shehe B. Musa?, alikuwa kwenye misosi na Karata. Je Kentigen?, alikuwa mbishi kinoma. Dom 5 lilikuwa linaongoza kwa watu kupenda kula maini [maharagwe ya jana] na uji asubuhi. Yaani ukipiga hayo hata kama bili ya katizi kwa mama msele imeisha huna stori.
 
Shehe B.Musa namkumbuka,si alikuwa mwembamba mrefu hivi....Dorm 5 walikuwa balaa kwa maini hasa Dorm leader wao Shaneli Mtei yule ndo alikuwa mtaalamu wa kula maini yalochanganywa na Fongo...Hivi CHARLES NYANGE yuko wapi???
 
Chaaz Nyangi tupo naye hapa jijini, anaishi Sinza kwa Remmy. So ulimaliza na kina shanel?, sie tulimuachia dorm 5 mwaka 2000.
 
Chaaz Nyangi tupo naye hapa jijini, anaishi Sinza kwa Remmy. So ulimaliza na kina shanel?, sie tulimuachia dorm 5 mwaka 2000.

Yap nilimaliza na kina Shanel,Kosovo na wengine..Angalia PM
 
Back
Top Bottom