Tujikumbushe UMBWE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujikumbushe UMBWE

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Balantanda, Nov 25, 2008.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi kuiona thread ya wadau wa Ilboru napenda na siye wa Umbwe tujikumbushe japo kidogo baadhi ya misamiati tuliyokuwa twaitumia pale 'Mti safi'..Baadhi ya misamiati ni kama: Fongo (Uji),, Katizi (Maandazi ya ubapa marefu hivi),, Maini (Maharage),,,, Fulu (Mbege)-lol nimeimiss,,, Maputo (Vyoo vya shimo kule juu dorm 8 na 9 Ukitaka kuingia wavua nguo zote ukiwa nje otherwise darasani hakutakalika). = Wadau nipeni misamiati mingine..Naikumbuka sana Umbwe a.k.a Mti safi a.k.a Umbwe Dume..Nakumbuka kipindi nasoma alikuwepo Mwalimu mmoja wa nidhamu aitwa Mallya a.k.a LOBILO alikuwa mkali huyo kama nini,ukiingia kwenye anga zake tu umeumia...Pia kuna dada mmoja aitwa Farida alikuwa anatuuzia maandazi(Katizi) sijui yuko wapi sasa hivi.................... = Nakumbuka sana Mbege ya Corner bar(ipo karibu na Mto Umbwe) kila weekend tulikuwa tukienda hapo kupata kitimoto na Mbege(lol) = Bila kuusahau ule Wimbo wetu wa shule 'Mungu baba mwenyezi bariki shule yetu.......................Umbwe ni Mti safi wa Matunda bora,yanayojenga maisha(dah)............ = Pia nakumbuka vijiji vya jirani kama KWA RAPHAEL,KOMBO,MANGO,LYAMUNGO,KIBOSHO CENTRAL,LYAMUNGO,NARUMU,UMBURI,KINDI,MANUSHI n.k Naomba kuwasilisha wadau
   
 2. H

  Herbert Member

  #2
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ok si semi ni vibaya kukumbuka tulikotoka ila naona mlolongo utakua. Mpaka shule zote zote ziishe, na bila shaka stori ni zile zile uji, Ugali, Kande, vijiwe vya fegi ndumu, mikahawa, Mademu Samaki na nyimbo za shule.

  Tulijumuishe kwa madenti wa miaka hiyo watupe michapo mbalimabli sehemu moja.
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ha-ha-ha-hah!
  Your environment was hash.... :)
  ...'Maini' = Maharage? :)

  .
   
 4. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Haaha haha ahahah! Nimecheka kwa sauti....Eti Maharagwe kwao yalikuwa sawa na maini! Very funny!
   
 5. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Balantanda.

  Umemaliza mwaka gani mti safi?
   
 6. Mchana

  Mchana Senior Member

  #6
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 181
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakika hatutamsahau KIBADENI (mpishi mwanamke) kwa umahiri wake wa kuning'inia na mwiko wa ugali kwenye mchakato wa kuwasongea ugali wanafunzi wote 400 wa shule hiyo wakati huo. Nakumbuka maparachichi , pamoja na duka la mzee Makini, na binti yake mrembo aliyekuwa anasoma Kibosho Girls, nakumbuka bendi ya muziki ya mti safi iliyokuwa inatumbuiza kwenye function mbali mbali, nakumbuka duka la shule na shamba la migomba na mradi wa ndizi mbivu aliokuwa anausimamia mzee Kirama, nakumbuka zoezi la kumenya karanga kwa mzee kirama kule Mkomongo. Naikumbuka shule ya jirani ya mlama , na hotuba za mzee wa Kiraracha Mzee Lyatonga alizokuwa akija kutoa maeneo yale wakati akiwa mbunge wa Moshi vijijini. Je , Daraja la kuvukia machame girls la mto Machame ambao ni mti mmoja tu umelazwa ku-cross huo mto?......nk nk
   
 7. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  My favorite: Unaposhuka na basi pale kwa Raphaeli, wakibosho wanakuuliza unaenda Mlama au unaenda Sekondariiii (meaning Umbwe)., and I remember how we use to hate Mlama. Those were good days...unakumbuka mambo ya NIDO?
   
 8. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Nyie kumbe ndio mliokua mnatuona sie wa Lyamungo wapori pori eeeh! Mzee Hata mimi pale Lyamungo Makeresho nimetandika sana Fongo=Uji
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kibadeni si ndo mama Mary mkuu..Hilo daraja la mto Machame tumelivuka sana kwenda Machame Girls siku za weekend
   
 10. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi Mzee Wawa bado yuko? Yule mzee alikuwa anakuja kupika yuko bwii!
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hahaaa umenikumbusha mbali sana,,mi mpaka naondoka Mti safi mzee WAWA alikuwepo Mkuu
   
 12. RR

  RR JF-Expert Member

  #12
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  LOL...Huyu mzee alikua anajifanya anaelewa sana lugha ya madenti, basi watu tulikua tunamchomekea matusi bila yeye kuelewa anajibu..


  Kibadeni ni tofauti na Mama Mary...Kibadeni alikua mwembamba sana na alikua kikohozi/mafua yasiyoisha!

  Nakumbuka dark room (nadhani kilikua chumba cha kusafishia picha zamani), yule Luka muuza karanga (alikua ni mtoto wa mwalimu wa fine art Mwetamba - sometimes alijifanya denti). Yale mabweni ya Matemu, Kirama, Sokoine....kule Kembriji (form three),
  Nnya (mbege)!

  Headmaster Savimbi (A. Shayo) baadae M. Tango.

   
 13. Mchana

  Mchana Senior Member

  #13
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 181
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wakuu kuna waliomaliza nami Umbwe miaka ya 1989 humu ndani ?
   
 14. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #14
  Nov 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Lyamungo was the modest school wacha utani kabisa! Hard working, na kwa ulimwengu wa sasa ni kwa vile tu baadhi ya wasimamizi/management hawakuwa makini ile shule ni sawa na Roya Palm Moven Pick kwani ni shule chache sana zina swimming pool and of such an architecture. Kwa aliyesoma pale atakubali baada pia ya kupata exposure ya shule nyingine.
   
 15. RR

  RR JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Hizi picha zaweza kuwakumbusha mambo ya mti safi kidogo

  [​IMG]

  [​IMG]  [​IMG]


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 16. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #16
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Lol,,Mzee wanikumbusha mbali,,Naiona OLD TRAFFORD(tulikuwa tukiuita uwanja wetu hivyo) kwa mbaali..Pia naiona bar ya staff hapo karibu na getini,kuna mwalimu alikuwa anaitwa PROTEA alikuwa anahudhuria sana katika hiyo bar ilikuwa akitoka hapo anapandishapandisha suruali usawa wa tumboni(Yenu) kisha anaanza kupiga mikwara wanafunzi lol...Pia alikuwepo Mbise (unaleta UKUDA UKUDA hapa) sijui kama bado yupo mti safi,bila kuwasahau mwalimu LOLO,KITUA,MUSHI,MWETAMBA,SOKA,PANGANI,LYAKURWA na wengine ambao najaribu kuwakumbuka
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Umemaliza mwaka gani Mti safi Mkuu????
   
 18. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #18
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Wakuu wadau wa Umbwe kama kuna mtu ana picha za Mabweni,Kanisa letu la ndani ya campus,'Temperature room' na 'Maputo'(lol) atuwekee humu basi jamani bila kuisahau picha ya uwanja wetu mkali wa Basketball
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Nov 26, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Misamiati zaidi ya Mti safi: Kufufuka (kuamka usiku wa manane kwa lengo la kujisomea),,Kicheche (Mtu mwenye bidii ya kujisomea),,kupiga ucheche (Kujisomea kwa nguvu zote hasa kipindi cha Mitihani)
   
 20. Capitol Hill

  Capitol Hill JF-Expert Member

  #20
  Nov 27, 2008
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 733
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Niliwahi kupigwa search na "mwalimu mmoja hivi wa social" hapo kwa Raphael..alinilia time ile nimeshuka tu kwenye ki Hiace na yeye huyo, basi akachukua shs 500 yangu. Nilikuwa nimepanga nikamuone Aunt Mary pale Canteen...ah basi tena ikawa nimevurugiwa budget.
   
Loading...