Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 1,318
- 4,044
Mr Blu mtoto wa mjini daslam aliwahi kusema "Bongo nyoso, Bongo balaa" huku Becka akiimalizia balaa kwa kusema "aaa aaah" kwa kumaanisha bongo ni balaa sana.
Kipindi hicho unaiona Dar es Salaam kama sehemu muhimu kwa ajili ya maendeleo yako lakini daslam yenyewe inakuona kama boya lingine la kulikaanga na hili joto kali.
Unapambana kugombania dala dala za gomz, unamwambia mchoma chips aku balansie za buku, bahasha ya vyeti hadi imekakamaa kutokana na kuishikilia sana unapotembea kutafuta hata ku-volunteer, mpenzi ulienae anakuomba hela ya pedi wakati hata wewe umeshindwa kuongeza boxer nyingine, baba ukimwomba pesa anakuambia wewe upo dar huko pesa hauwezi kosa, hapo hapo vishoka wameshakula pesa zako kwa kudanganya watakutafutia mishe, huku geto majirani wanakusema eti unajifanya msomi sana hauwachangamkii bila ya kujua una pitia depression ya hatari.
Hakika dsm ni connection, dsm ni kujipanga. Wanaenjoy dsm ni wale walio kuja wakiwa katika "control mode".
Simaanishi dsm sio sehemu sahihi, ila sio sahihi kwa kila mtu, haikuwa sahihi kwangu, nilisepa mapema, nikarudi mikoani na namshukuru Mungu nilijitafuta huku na nikajipata, Maisha yanaendelea.
TUSICHOKE KUPAMBANA, ILA TUSIONE HAYA KUBADIRISHA MAZINGIRA.