Tujikumbushe mwaka 2015 wakati wa kutafuta wadhamini hali ilikuwaje

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
5,669
9,055
Mwaka 2015 wakati kama huu kulikuwa na zoezi la kusaka wadhamini kwa lengo la kupata akidi ya kuweza kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama mtakumbuka vizuri wakati huo Edward lowasa alisimamishwa kuwa mgombea urais kwa upande wa ukawa mshindani wake akiwa Rais Magufuli.

Kama sio wasahaurifu tuliona jinsi utafutaji wa wadhamini ulivyokuwa kwa wakati huo, nipate kusema kwamba wagombea walisaka wadhamini kwa stahili hihii anayoitumia mh. Tundu Lissu.

Mania kwa maelfu ya watu walijitokeza barabarani kuwasikiliza wapendwa wao kama wafanyavyo sasa kwa mpendwa wao Tundu Lissu. na walitoa ahadi kemkem kwa wananchi ambao walijitokeza, tukumbuke kwamba hayo yote yalifanyika wakati wa kutafuta wadhamini mikoani na kwingineko.

Mwisho wa siku NEC iliwapitisha na kuwa wagombea kupitia vyama vyao, hatukusikia kuwa huyu au yule atakatwa kwa sababu ameanza kampeni mapema kabla ya kupitishwa na umekuwa kama wimbo sasa kwamba lazima akatwe.

Tofauti na mwaka 2015 ambapo wagombea shindani walikuwa wawili mwaka huu kila chama kimesimamisha mgombea wake lakini ukitazama duru za kisiasa wagombea wenye mvuto na ushindani wa hali ya juu kwa Tanzania bara ni wawili tu yaani Rais Magufuli na Tundu Lisssu.

Huyu mmoja anasaka wadhamini kwa stahili yake ya kupiga kampeni kwa kuitisha makongamano ya kidini na sanaa pamoja na kuzindua miradi kama vivuko pamoja barabara dk za mwisho za kuelekea uchaguzi. Wkt mwingine anatumia njia zilezile zilizotumika mwaka 2015 kwakuwa yeye hana miradi ya kuzindua wala nafasi ya kuitisha makongamano na matamasha ya wasanii.

Swali, kwa nn iwe nongwa kwa wakati huu wakusaka wadhamini na kutaka wagombea wajifiche ktk kutafuta wadhamini? au tatizo ni TL, mshindani ambaye hakutarajiwa na wengi na kufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa ushindani.

NEC msifanye makosa ambayo yataleta usumbufu usio na lazima kwa nchi yetu kwa kukata wagombea ambao wanaonekana ni challengeable kwa mgombea wa CCM, waacheni wananchi waamue mgombea wanayemtaka kupitia sanduku la kura.
 
Mkuu hakuna wa kumkata Lissu,Kama ccm wanataka kulipuliwa siku ya ufunguzi wa kampeni zao wajaribu waone,watu tumeshawachoka sana na hatuna Cha kupoteza mpaka sasa
 
Back
Top Bottom