wahenga walisema chanda chema huvikwa pete na mchagua jembe si mkulima! na pia aliye juu mngoje chini! hembu na wewe tupia ya kwako ya wahenga! karibu....
Vyakutwanga vianike angali jua lingalipo! 2.mchuzi wa mbwa unywe ungali wa moto. 3. Raha ya sebene mtu uichezee kenele 4. Kina cha fikra hakipimwi kwa kamba. 5. Mchuzi wa kibua mkabidhi mzigua
haba na haba hujaza kibaba! asiyeskia la mkuu, huvunjika guu! mbio za sakafuni, huishia ukingoni! heri nusu shari kuliko shari kamili! majuto ni mjukuu!
Uzi huu ungefaa sana kule jukwaa la lugha, mi naona ndo mahala pake. Hata hivyo nachangia:
1. Mwenye dada hakosi shemeji.
2. Angaruka juu kipungu hafiki mbinguni.
3. Mwenda tezi na omo marudio ngamani.
4. Ukitaka kuruka agana na nyonga.
5. Mbaazi ukikosa maua husingizia jua.
6. Mchelea mwana kulia hulia yeye.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.