Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Leo hii Marekani ni kinara wa kuisakama Urusi juu ya kutunguliwa kwa ndege ya abiria ya Malaysia na kuua watu wote 296. Japokuwa sote tunalaani kitendo cha ndege ya abiria kutunguliwa na abiria wasio na hatia kuuawa, huenda watu wasichokumbuka au walichosahau ni kwamba tarehe 3 July 1988 Meli ya kivita ya Marekani, kwa makusudi kabisa, na ikiwa katika eneo la maji la Iran, iliitungua ndege ya abiria Iran Airflight 655 aina ya Airbus A300 B2-203, na kuua abiria wote 290 waliokuwa kwenye ndege hiyo, kutia ndani watoto 66 na wafanyakazi wa ndege 16. Ndege hiyo ya Iran ilikuwa ikisafiri toka Teheran kwenda Dubai.
Walipoulizwa juu ya hili na Mahakama za Kimataifa, Wamerakani walijibu kwamba walidhani hiyo ndege ya abiria ya Iran ilikuwa ni ndege ya kivita. Wamarekani hawajawahi kuomba msamaha juu ya jambo hili hadi leo, japo walikubali kulipa $213,103.45 kwa kila abiria aliyekufa. Hakuna hatua zozote za kimataifa zilizochukuliwa dhidi ya Marekani kwa tukio hili.
Iran walichapisha stemp za kumbukumbu ya tukio hili
Abiria waliokufa katika tukio hilo ni kama ifuatavyo;
Source: Wikipedia

Nationality | Passengers | Crew | Total |
---|---|---|---|
| 238 | 16 | 254 |
13 | 0 | 13 | |
10 | 0 | 10 | |
6 | 0 | 6 | |
6 | 0 | 6 | |
1 | 0 | 1 | |
Total | 274 | 16 | 290 |