Tujikumbushe, je tulikwama wapi?

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,602
5,569
Ninanukuu makala ifuatayo ili kuweka kumbukumbu sawa tujue tulianguka wapi na makosa gani yalitugharimu ili tunyanyuke na kujiondolea mawaa hayo:

Nyerere Alitawala Kondoo; Mbuzi Wasingemuelewa!
Kuna mchezo mbaya unaoendelezwa na kulindwa na Serikali ya CCM; nasema ni mchezo mchafu kwa vile badala ya kutufungua macho tunaendelezwa kurudishwa nyuma zama zile za giza za watawala walioshindwa maisha ya kisiasa! Kumekuwa na utaratibu wa kuziweka hutuba za Nyerere kwenye aidha vipindi vya redio au televisheni na wananchi wa kizazi hiki kuzisikiliza kama vile ni hutuma zenye maneno ya busara yanayotakiwa kuigwa na kufuatwa na kila mtanzania!

Kuna hutuba za Nyerere zinazoenyesha wazi kwamba anayoyasema yalikuwa hayakubaliki na hayakuwa na mashiko yoyote hata kwa wakati huo, lakini utakuta watu waliokuwa wanamsikiliza wanampigia makofi na kushangilia! Kwanini tusione kwamba hilo lilikuwa ni la kitaifa kwamba kiongozi na jamii yake aliyokuwa anaitawala wote kwa pamoja walikuwa na mtizamo mdogo wa kufikiri na kuona kule walikotakiwa kupaona?

Kwa mfano, kuna hotuba ya Nyerere anayosisitiza na kuonya kwamba ni hatari kwa Tanganyika kuitwa Tanganyika kwa vile eti ikiitwa Tanganyika makabila ya watu waishio Tanganyika wataanza kujivunia ukabila wao na nchi itaingia katika tatizo la ukabila! Na wakati anayasema hayo anapigiwa makofi na kushangiliwa kwa vigelegele! Kama ukishindwa kujijua, huwezi kulijua kabila lako, na kama huwezi kulijua kabila lako huwezi kulijua taifa lako na kama utakuwa huyajui hayo yote basi hujui wajibu wako katika dunia hii!

Mfano mwingine, kuna hotuba ya Nyerere anakemea rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na katika mkutano huo mawaziri anaowashutumu kwa ubadhirifu wapo jukwaani amekaa nao meza moja na huku anawahutubia wananchi kwa kauli kali na hasira ya hali ya kuu akionyesha kwamba amekasirishwa sana na vitendo vya ufisadi, waliohusika na ufisadi huo hawawajibishwi bali wanaishia tu kukemewa na kubadilishwa wizara! Na huku wananchi wakiishia kumshangilia na kumpigia vigelegele!

Mfano mwingine, makamu wa kwanza wa rais Rashidi Mfaume Kawawa aliwahi kumuuzia Lord Rajipa meli ya Serikali kwa shilingi milioni 60 bila ya ridhaa ya wananchi na pesa ya mauzo ya meli hiyo haikuonekana hadi leo! Wananchi walipolalamika na kulifikisha swala hili kwa aliyekuwa waziri mkuu wakati huo Edward Moringe Sokoine alimuuliza Kawawa pesa ya umma ipo wapi na hakupata jibu! Hili lilikuwa tatizo la kitaifa kwani lilitangazwa kwenye vyombo vyote vya habari na lilijadiliwa kila kijiwe nchini kote! Lakini cha kushangaza pamoja na kwamba nchi ilikuwa na meli moja tu na ilikuwa inakabiliwa na hali mbaya sana kiuchumi Nyerere hakuwahi hata siku moja kulizungumzia hilo tatizo mpaka akatoka madarakani na hata baadae akafariki dunia! Huyo ndiye Nyerere ninayemkumbuka mimi, huyu anayefagiliwa kila gazeti na vyombo vya habari leo hii, kwa kweli simfahamu!

Nyerere alitawala wakati mmoja na kina Dr. Makhdhari wa Malaysia, Rais Lee wa Singapore na Rais Sukhato wa Indonesia na nchi zote hizi zilikuwa masikini na pia zilikuwa nyuma kimaendeleo kuliko Tanzania, lakini nchi hizi leo hii zimeingia dunia ya kwanza, na sisi bado tupo kule kule kwa miaka ya sitini na bado tunaendelea kuabudu fikra za yule aliyetufikisha hapa tulipo! Kwa maana hiyo ndiyo maana nasema Nyerere alitawala Kondoo, sisi ni Mbuzi tusigeuke tukawa Kondoo kama walivyokuwa wenzetu!

Dr. Noordin Jella

Chanzo: Nyerere Alitawala Kondoo; Mbuzi Wasingemuelewa!

Kwa hali ya sasa makala hiyo inaweza kuwa uchochezi (kila ukweli ni uchochezi) Ikiwa tuna dhamira ya kweli kuelekea UCHUMI WA KATI NA NCHI YA VIWANDA lazima tutambue kilichoua viwanda vilivyokuwepo na kufisidi nchi kama inavyoonekana katika makala tajwa hapo juu, kubebana baina ya viongozi na kufumbiana macho ambako kumelelewa na kukuzwa na CCM.

KUTISHANA NA KUITANA HAWA WAZALENDO HAWA WAPINZANI HAKUTATUVUSHA WALA KUTUPELEKA KOKOTE. SOTE NI WATOTO WA MAMA TANZANIA TUNA HAKI MAMBO YASIPOENDA SAWA TUSEME, TUKEMEE MAANA HILI NI JAHAZI LETU SOTE LIKIZAMA SOTE TUNAATHIRIKA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Yaani Nyerere alitawala mbuzi na kondoo?Yan wahenga wetu,mababu zetu,wazee wetu,wazazi wetu walikuwa mbuzi na kondoo kifikra na kimtazamo?Hii sio haki kabisa.
Hivi hao aliowatawala Nyerere na hawa jamaa wa EPA,ESCOROWS,BUZWAGI,MEREMETA NA RICHMOND nani bora?????Wale wazee walikuwa watulivu kwa ajili ya kutuandalia msingi bora ambao hao wa kisasa wamekuja kuharibu na kuua kabisa msingi bora wa nchi yetu.
 
Yaani Nyerere alitawala mbuzi na kondoo?Yan wahenga wetu,mababu zetu,wazee wetu,wazazi wetu walikuwa mbuzi na kondoo kifikra na kimtazamo?Hii sio haki kabisa.
Hivi hao aliowatawala Nyerere na hawa jamaa wa EPA,ESCOROWS,BUZWAGI,MEREMETA NA RICHMOND nani bora?????Wale wazee walikuwa watulivu kwa ajili ya kutuandalia msingi bora ambao hao wa kisasa wamekuja kuharibu na kuua kabisa msingi bora wa nchi yetu.
Mkuu soma vizuri makala hiyo uone waliomzunguka Mwalimu walifanya nini!? Ndipo utajua hizo EPA, ESCROW, BUZWAGI na ndugu zao hazikuanza leo! Je viwanda vilianza kufa lini? ni wakati gani Mwinamila aliimba "1. ... sukari imepotea! 2. Tuache kazi za miradi tutakula kwako?" Na laiti angekuwa hai kwa CCM hii ya sasa angeitwa mchochezi!!!

Hebu sikiliza vipande vya hotuba za Mwalimu vinavyowekwa kwenye redio zetu na luninga kisha usikie watu wakicheka wakati mwalimu anakemea mambo maovu na ufanye tathmini ya vicheko vile vilimaanisha nini toka meza kuu
 
namuelewa sana dr. Jella, ana makala za kufikirisha sana
Tukijenga uwezo wa kufikiri na kuhoji ndipo tutasogea kuliko fikra za "zidumu" ambazo pamoja na kuwekewa mabango zilitukwamisha na kutuzika ili tusichomoke kwenye makucha kandamizi ya MATUMBULI!! na MATUMBILI hayataki tufikiri tena kama wakati ule!! Hatari sana hii
 
Back
Top Bottom