Tujikumbushe ILBORU

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
5,558
Reaction score
1,460
Kwa wale Ilborins Mnakumbuka hii Misamiati jamani?

KITEI = Kipunga Iva Tule Elimu Inatungoja (Wali)
CHUI = CHUkua chako Iboru (Ugali aka Bondo)
SUMU = Haya yalikuwa Makande
Half Life = Jina Maarufu la kiporo hasa cha SUMU au KIETI ( tulikuwa tunachanganya na Uji)
Umenyeni = Kijiji around Ilboru
Baghdad = Hii siikumbuki mwenye kukumbuka anikumbushie
Golgota = Huu ni Ukumbi juu ya Maktaba ambapo ndipo NECTA inafanyika
Mtego = Chandarua
KUKU = Kalale Upitwe Kama Umesimama ( Usingizi)
Twiga = Sikumbuki
Kufufuka = Kuamka Ucku wa Manane
Bafu Kubwa = Eneo Chini ya Daraja ambako Vijana hupenda kwenda Kuoga
Chief = Mwalimu katili kabisa na mpenda sifa Losujaki ,sijui sasa hivi yuko wapi
Kite = Alikuwa headmaster , Kitemango
Enabo = Enaboishi, hii ni shule Fulani ambayo walikuwa hawaivi na Ngarenaro,totoz zilikuwa
zinagombania Ilborians
 


The last time I heard about him is that he is nowadays a headmaster!
 
Macha (Machakura) aka Mugaya (RIP?)
Kwa mama Toni? Kule nyuma ya ile thieta?
 
Ok thanks guys. We now know that you go through special school and you are Vipangas

Congratulations.

Anything Else from your Special school??
Nyie ndio mlikuwa na akili nyingi? nasikia mlikuwa/mapewa mitihani ndio maana vibanda vingi.....a'u dizaini watu waliosoma boys walikuwa wachafu kwa kukopa(kutokuoga)

Pugu Boysss mpooo? Mkandawile alikuwa anaponda sana,Pugu boys walikuwa hawamlipi hela ya tuition.
 
Ok thanks guys. We now know that you go through special school and you are Vipangas

Congratulations.

Anything Else from your Special school??

....hawana lolote hawa mbele ya Umbwe.....tumewakimbiza kutoka weruweru, kibosho mpaka wameishia kwa wamenye wenzao Enaboishu duh!!!
 

Pugu boys wazee wa fungus!maana mkandawile alikuwa anawaita fungusboy!
Hivi mkandawile yupo wapi?
 
Pugu boys wazee wa fungus!maana mkandawile alikuwa anawaita fungusboy!
Hivi mkandawile yupo wapi?
ha ha ha FL unaua sasa!!! ile sio fungus ni "kupiga gitaa" ukitaka kumjua Pugu boy basi utamkuta mkono uko ndani ya sarawili(anapiga gitaa).
Mkanda sijui yuko wapi nahisi atakuwa anaendeleza libeneke la kula vichwa
 
MTEGO= kideo cha Shule
KATARA= mtu ambaye alikuwa na kichwa kikali, anafananishwa na lile gari la shule la bluu
KWA MAMA BENII= kibanda ambacho baadhi ya member wanakula fegi
PICHI= uwanja wa mpira, kule kilimani karibu na Nyumba ya headmaster.
ILBORIASIS MSULIATA= scientific name ya mwana ilboru
 
Mkandawile sijui kama bado anafundisha ila jamaa now anamiliki shule
 


Wewe wewe weee;

Pale Meru tuliruka sana dirisha za Mzulu, sijui yuko wapi na zile suruali zake kama bado anakua!!... Utamu zaidi ni pale tukiwa "POND"... mtu unatembea na panadol shule nzima kutafuta nusu glasi ya maji ya kunywa!! ...na Mihogo ya Mze wa shamba (sijui mwanga yule!?)

These were two best moments in my life -
 

Aisee hii imenichekesha sasa, hii nadhani ilikuja baadae. Sisi hatukuiacha.
Bravo G la N!
 
Samahani msinishambuliee natoka nje kidogo. Hivi mliwezaje kusoma bila mademu? Yaani wanaume watupu?
 
Umbwe walevi wa mbege tu....hawana mpango wowote!😀, enzi zetu tuliwaputa Machame Girls, Zoo na Ashira Girls! LOL, wakabaki kulialia tu...

Acha maneno bana...Mti safi tumewatesa sana nyie mpaka mkakimbia Weru Weru. Mkaanza kugombea watoto wa O'Level wa Machame Girls na competition yenu.. Lyamungo Sec.
 
Samahani msinishambuliee natoka nje kidogo. Hivi mliwezaje kusoma bila mademu? Yaani wanaume watupu?

We sajo nani kakwambia kuwa tulisoma bila "mademu"??? Mademu walikuwepo ila hawakuwa wanafunzi wa Ilboru. Tofauti ya Ilboru na Mkwawa ni kwamba Ilboru imezungukwa na shule kibao za mchanganyiko. Na iko proximal to city centre ambapo kuna shule kibao za day na boarding.
 
Hivi yule jamaa pale ilboru (mvuta bangi maarufu) aliyeandika list ya wachezaji wa form two during interclass games kwa mavi yuko wapi?

Nzowi wa pugu naye yupo?
 
Baghdad ni ile sehemu ambayo jamaa walikuwa wanakwenda kupata ganja na fegi kupunguza stress zao za masomo. Remember Mtui, Masaki , Medukenya, Kimasia,Machakura, Mama Mutabuzi, Boi, Quaressi,Lolo, Kweka, Chifu and Blanca and many more. Kwa madenti Carlos Mwaibula, Elisante Stanley, Jose James, Victor Maleko, Steven Alfred/ Ras. Rajabu Masale Kaka Zanda,Bandama,Omneni Laiser , Freddy Lowasa Olais Mwing'ori jamaa alikuwa vice prefect alikuwa mnoko sio mchezo. Kipindi hicho wasukuma walikuwa na magovi jamaa mmoja alikuwa na pesa akajitolea kuwatahiri. Namkumbusha mshikaji analikumbuka KATARA? Shule yangu Ilboru inasifika sana popote ninapoenda inasifika sana (Wimbo wa shule) Naishia hapa kwa leo...
 
Unakumbuka mikate ya "sunkista" pale kwa Loning'o? hv mama tonii bado anapika pilau kule chini? nasikia Shembilu alivuta je ni kweli? Kishuu na Geree bado wapo?

Shembilu aka Mswahili (RIP), Mgaya (RIP)

Kaka umenikumbusha kwa Loning'o, ha ha haaaaa Clasa areaaaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…