Tujikumbushe asili ya Mungu

Tujikumbushe asili ya Mungu

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,009
Reaction score
17,457
Nianze kwa kuweka pembeni mafundisho ya dini yoyote kuhusu Mungu.

Nitakupa maana yangu niliyoibuni nilipokuwa mdogo chini ya miaka 10.

Nilimuuliza Bibi yangu mzaa Baba: Sisi tumeumbwa na Mungu. Je, Mungu aliumbwa na nani? Mungu alitoka wapi? Na kama hakuna Mungu ndo maana hakuna kitu, kila kitu hakuna kabisa ni utupu (empty) nikaingia ndani nikazama peke yangu nakuambia nilikaribia kuchanganyikiwa.

Hebu na wewe waza kama nilivyowaza hata sasa hivi kwamba kama hakuna asili ambayo hiyo asili ilipelekea wewe kuwako na fikilia kwa vile kila kitu kina mwanzo fikilia kuwa mwanzo haupo zama ndani baba/mama hawakuwahi kuwako na wewe automatically usingekuwepo nenda backwards ndani nakuambia utafikia kuchanganyikiwa.

Sasa hiyo asili ambayo ukitaka kuiondoa unapelekea ubongo kuchanganyikiwa ndio Mungu. Mungu ndio asili ya kila kitu! Mungu alikuwepo! Ilikuwaje akawepo hakuna ajuaye na ukitaka kumuondoa na kuamini hayupo automatically utachanganyikiwa.

Kitu cha kwanza kuumba ulikuwa muda. Muda uliumbwa kwasababu Mungu haishi kulingana na muda. Mungu huishi katika umilele.

Kwahiyo uumbaji wote ulianza pale alipoumba muda. Huu muda tunaoujua kwa sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka, majira, nyakati, n.k. viliumbwa.

Fuatilia mwanasayansi anaitwe Stephen Hawking' Anakubali kuwa kitu cha kwanza kuumbwa ni Muda na kwamba Mungu hayupo kwasababu angekuwepo angetakiwa kuwa na muda (time) ya kuumba muda na kwamba muda ulijiumba automatically (big bang).

Nahitimisha kwa kusema: Aliyeumba muda ndio Mungu kuanzia pale akaumba kila kitu tukiwemo wanadamu.
 
Una hoja nzuri ila ulianza Pilau ukaja Ugali naona ukamalizia na Makande. Wachache nadhani ndo wanaeza elewa kwa mtiririko uloenda nao
 
swali la lamsingi hapo ulitakiwa kujiuliza ni hivi

Vuta picha umekutana na mtu ambaye hajui chochote kuhusu uchawi wala hajawahi kusikia habari za mungu, shetani.

Umepewa kazi yakuhakikisha unamfundisha mtu huyo mpaka aweze kujua kua mungu yupo

Sasa kama ndio wewe hapo utaanza vipi? Utamuonesha biblia/quran na kumwambia hiki ni kitabu cha mungu?

Mtu huyo akikuuliza hicho kitabu unachosema cha mungu umekithibitisha vipi hadi ukakubali kua kimeongea ukweli? utamjibu vipi?

Au utatumia uwepo wa ulimwengu na viumbe vingine vilivyomo ndani yake ili visimame kama kielelezo cha kuonesha mungu yupo?

Ambapo ukiambiwa uthibitishe kivipi ulimwengu na vilivyomo viwe vimesababishwa na mungu na sio kitu kingine? Hutakua na jibu

Au ndo utarudi kule kule kwenye biblia/quran kua ulimwengu na vilivyomo vimesababishwa na mungu kwasababu vitabu vimesema? Na vitabu hivyo ndio vile vile ambavyo ulishindwa kuvithibitisha hapo awali kama vimeongea ukweli

Utajikuta huna majibu yakuridhisha, na itakubidi umgeuzie kibao

Utamuuliza haya niambie kama mungu hayupo huu ulimwengu na vingine vimetoka wapi?

Mtu huyo akisema kua kwani haiwezekani kitu kikawepo bila kuwa na chanzo? Kuna ulazima chanzo kuwepo ili kingine kiwepo? hapo utamjibu vipi?

Sasa jiulize, wewe ulianza vipi kuamini mungu yupo?
 
MUNGU NI NGUVU CHANYA(WEMA). SHETAN NI NGUVU HASI(UBAYA). biblia na quran etc ni miongozo ya wanadam namna ya kuishi kwa aman na upendo. Ni busara za watu wa nyakati zilizowekwa kwenye maandishi kwa ustad na werevu. Kwa lugha ya sasa ni KATIBA.
 
Hii ndio definition sahihi ya Mungu. GOD IS ENERGY.

The force behind all power is energy. Sasa haya mambo ya dini ndio mvurugo balaa.

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Mkuu mimi huwa nikitaka kumuelewa Mungu na-refer kwenye Mambo mengi, mfn dawa za asili zinavyofanya kaz..napata kujua kuwa haya yote ni just a small drop of power from the ONE HUGE INFINITE POWER!!


Nafika mahali nashuidwa nielezee vp nieleweke

Goite
 
MUNGU NI NGUVU CHANYA(WEMA). SHETAN NI NGUVU HASI(UBAYA). biblia na quran etc ni miongozo ya wanadam namna ya kuishi kwa aman na upendo. Ni busara za watu wa nyakati zilizowekwa kwenye maandishi kwa ustad na werevu. Kwa lugha ya sasa ni KATIBA.
Mkuu (nje ya dini zetu) sidhani Kama shetani yupo!!

Mimi nachojua kila kitu kina + & - energy(side)

Umeshawahi kuangalia video za wanyama mfn zile za NATIONAL GEOGRAPHY??

Huwa naona wanyama wanapigana, Kuna wanyama wanaiba mayai ya ndege wanachimba ardhi wanaficha, Kuna wanyama wanaua wenzao!! Huwa najiulza nao wanafanya hayo yote kwa sababu ya shetani???

Mimi naamini kuwa UBAYA NA WEMA (+&-/ two sides) is NATURE OF EVERYTHING.

Goite
 
Hebu fikiria waliowengi kama tunavyojua kuwa vitu vyote viliumbwa. Sawa nakubaliana na kila mtu kuwa kila kitu kiliumbwa lakini kiliumbwa lini? Hapa tunaposema "lini" tunaongelea muda. Hivyo basi wakati muda in zero "0" ina maada hapakuwepo na kitu. Viumbe, dunia, mfumo wa sayari kama nyota, sayari zooote, jua, n.k. havipo! Pia mwanga hata giza hakuna! Kuko kimya kabisa kabisa utupu kabisa hata hiyo kimya haipo kwasababu illiumbwa!! Yaani tupu utupu kabisa hakuna kitu hata cha kuanzia! Then, from nothing (hivyo kutoka katika utupu) labda "sauti" "sound" came out and said something out of nothing! But that sound to create came from where wakati ni tupu endelea kutafakari ingia ndani kabisa kwasababu hata kitu cha kuanzisha kitu hakuna na hakuna uwezekano wa kusababisha kitu kianze labda "may be" akili zinapogota kupata jibu ndo "MUNGU"
 
Una hoja nzuri ila ulianza Pilau ukaja Ugali naona ukamalizia na Makande. Wachache nadhan ndo wanaeza elewa kwa mtiririko ulo enda nao
Hebu fikiria waliowengi kama tunavyojua kuwa vitu vyote viliumbwa. Sawa nakubaliana na kila mtu kuwa kila kitu kiliumbwa lakini kiliumbwa lini? Hapa tunaposema "lini" tunaongelea muda. Hivyo basi wakati muda in zero "0" ina maada hapakuwepo na kitu. Viumbe, dunia, mfumo wa sayari kama nyota, sayari zooote, jua, n.k. havipo! Pia mwanga hata giza hakuna! Kuko kimya kabisa kabisa utupu kabisa hata hiyo kimya haipo kwasababu illiumbwa!!

Yaani tupu utupu kabisa hakuna kitu hata cha kuanzia! Then, from nothing (hivyo kutoka katika utupu) labda "sauti" "sound" came out and said something out of nothing! But that sound to create came from where wakati ni tupu endelea kutafakari ingia ndani kabisa kwasababu hata kitu cha kuanzisha kitu hakuna na hakuna uwezekano wa kusababisha kitu kianze labda "may be" akili zinapogota kupata jibu ndo "MUNGU"
 
Mkuu (nje ya dini zetu) sidhani Kama shetani yupo!!

Mm nachojua kila kitu kina + & - energy(side)

Umeshawahi kuangalia video za wanyama mfn zile za NATIONAL GEOGRAPHY??

Huwa naona wanyama wanapigana, Kuna wanyama wanaiba mayai ya ndege wanachimba ardhi wanaficha, Kuna wanyama wanaua wenzao!! Huwa najiulza nao wanafanya hayo yote kwa sababu ya shetani???


Mimi naamini kuwa UBAYA NA WEMA (+&-/ two sides) is NATURE OF EVERYTHING.



Goite
Unaweza kuwa sahihi. Mi na wewe tunajarib kufikiri tu nje ya box yan nje ya kukaririshwa. MUNGU tumwite WEMA. Shetan tumwite UBAYA. Hata hivyo wema na ubaya ni suala la utashi na dhamira. Navyo hutegemea mazingira ya kiumbe mwenyew kulingana na tafsir ya kanuni za kuishi alizojiwekea.Ubaya eneo X unaweza kuwa Wema eneo Y. Na kinyume chake.

Mungu hujitokeza pale ukomo wa kufikir na kutenda unapoishia. Shetan hujitokeza pale mazingira yanapokataa kuendana na matakwa ya mazingira yako. Zote ni hali. Ndo maana Mungu anakuwa na maana pale usipoweza binafs kumudu mazingira yako ili ukabiliane na hofu hiyo. Vitab vya Sheria na simuliz za kale yan Biblia na Quran vimelenga kuweka mizan namna ya watu na mazingira yao kuhusiana.

Yote haya chanzo ni HOFU. Itoshe kusema kwa habari kuumba, MUNGU ni UKOMO WA KUFIKIRI. na kwa habar ya kuishi MUNGU ni WEMA yan CHANYA.
 
Uko sahihi. Kuna vitu mleta uzi ame mix japo ana hoja nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu fikiria waliowengi kama tunavyojua kuwa vitu vyote viliumbwa. Sawa nakubaliana na kila mtu kuwa kila kitu kiliumbwa lakini kiliumbwa lini? Hapa tunaposema "lini" tunaongelea muda. Hivyo basi wakati muda in zero "0" ina maada hapakuwepo na kitu. Viumbe, dunia, mfumo wa sayari kama nyota, sayari zooote, jua, n.k. havipo! Pia mwanga hata giza hakuna! Kuko kimya kabisa kabisa utupu kabisa hata hiyo kimya haipo kwasababu illiumbwa!! Yaani tupu utupu kabisa hakuna kitu hata cha kuanzia! Then, from nothing (hivyo kutoka katika utupu) labda "sauti" "sound" came out and said something out of nothing! But that sound to create came from where wakati ni tupu endelea kutafakari ingia ndani kabisa kwasababu hata kitu cha kuanzisha kitu hakuna na hakuna uwezekano wa kusababisha kitu kianze labda "may be" akili zinapogota kupata jibu ndo "MUNGU"
 
Unaweza kuwa sahihi. Mi na wewe tunajarib kufikiri tu nje ya box yan nje ya kukaririshwa. MUNGU tumwite WEMA. Shetan tumwite UBAYA. Hata hivyo wema na ubaya ni suala la utashi na dhamira. Navyo hutegemea mazingira ya kiumbe mwenyew kulingana na tafsir ya kanuni za kuishi alizojiwekea.Ubaya eneo X unaweza kuwa Wema eneo Y. Na kinyume chake. Mungu hujitokeza pale ukomo wa kufikir na kutenda unapoishia. Shetan hujitokeza pale mazingira yanapokataa kuendana na matakwa ya mazingira yako. Zote ni hali. Ndo maana Mungu anakuwa na maana pale usipoweza binafs kumudu mazingira yako ili ukabiliane na hofu hiyo. Vitab vya Sheria na simuliz za kale yan Biblia na Quran vimelenga kuweka mizan namna ya watu na mazingira yao kuhusiana. Yote haya chanzo ni HOFU. Itoshe kusema kwa habari kuumba, MUNGU ni UKOMO WA KUFIKIRI. na kwa habar ya kuishi MUNGU ni WEMA yan CHANYA.
Mkuu, for sure nimekuelewa Sana!!
Zaidi nimependa ulivyoita VITBU VYA SHERIA NA SIMULIZI ZA KALE..hii umenipa wazo jipya kabisa jins ya kuzielewa biblia na Quran

Goite
 
Mkuu mm huwa nikitaka kumuelewa Mungu na-refer kwenye Mambo mengi, mfn dawa za asili zinavyofanya kaz..napata kujua kuwa haya yote ni just a small drop of power from the ONE HUGE INFINITE POWER!!


Nafika mahali nashuidwa nielezee vp nieleweke

Goite
Hata mimi nikifika kwenye lugha ndo huwa nachanganyikiwa, iweje tuwe na lugha tofauti ili hali tumetokana na mtu mmoja? Na hapo uwa nafikiria binadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa mwanamke na alipata mimba pasipokujua imetoka wapi na walikuwa mapacha wengi tuu zaidi ya 4, kadri miaka ilivyosonga hiyo hali ilitoweka na kujamiana kukaanza na uwezo wa kuzaa watoto wengi kwa pamoja ukapungua kutoka watoto 8 mpaka 1
 
Back
Top Bottom