Tujikumbushe ahadi za Mo

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
18,038
Reaction score
25,670
Jana mo kaongea mengi lakini tujikumbushe ahadi zake kabla na baada ya kuingia Simba.
Kabla ya kuingia Simbq alisema anataka kuifanya Simba ishindane na Mazembe ambayo wakati huo ilikuwa kiwango cha juu pamoja na Al ahly ya Misri pia alilalamika kwanini Simba inauza wachezaji wake wakati anataka Simba ishindane kimataifa.

Tukija kqenye uhalisia hakuna kipindi Simba imeuza wachezaji kama kipindi bodi yake imeingia, Konde boy, Chama, Bwalya, Sackho tena hata bei zilifichwa.

Alipiga picha na viongozi wq Juventus ya Italia na kusema ameingia makubaliano na Juventus kuhusu ushirikiano na Simba hayo makubaliano sijui yalifia wapi.

Baadae akaenda Marekani akapiga picha na timu moja ya huko akasem ameingia makubaliano na timu hiyo kuhusu uahirikiano na Simba wakati haijulikani lini mashirikiano yataanzq janq kasema kaingia makubaliano na Stuttgqrt ya ujerumani.

Wanaosema runamchukia mo waje watueleze kwanini anakuwa anatudanganya kama watoto wadogo.
 
Yote uliyosema ni ya ukweli na MO haeleweki kwenye ahadi zake.

Vipi kuhusu huyu hapa aliyeahidi hizi ahadi za kutoa kadi na kusajili wanachama, kumfunga Yanga, kukamilisha transformation ndani ya siku 60.

Na mbali zaidi akatuletea na Manzoki?
Your browser is not able to display this video.
 
Nimemuona peter wa mamelod na aziz hapa, ila hii Yanga hii ya msimu huu sijui aiseee. Simba kazi tunayo
 
Mo kwenye Ujenzi wa kiwanja hadi leo anazidi kutoa ahadi hewa..

Miaka ya nyuma mashabiki walikua wanamsikiliza sababu simba ilikua inafanya vizuri kimataifa kwahiyo kila analosema watu wanaamini ,..

Sasa hivi sio kwamba simba haifanyi vizuri,but imekwama pale pale kuishia robo kimataifa,.

This round maneno tupu hayatasaidia either simba afanye vizuri kimataifa,au awe bingwa Ligi kuu,.

Usajili wa simba miaka mitatu hii ni Janja Janja
 
Ujenzi umeshaanza pale jangwani
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani Yanga hawadanganywi? Si ni kwa sababu na wao league ya ndani wanafanya vizuri. Wakianza kuboronga utaona mashabiki na wanachama watakavyo anza kumkataa GSM na Hersi.
Lol
 
Kuna kipindi wakati wa uongozi wa Babra ceo Simba walisema wajenge uwanja wakawa wanachangishana, mo akasema atatoa bilioni 2 zile pesa za washabiki wakaja kusema walijengea fensi yeye bilioni 2 yake sidhani hata kama alitoa leo anasema anataka kutoa bilioni 30 ya uwanja anatuchukulia sisi mazuzu.
Uwanja wa Gwambina ambao Simba waliuzindua ulijengwa kwa shilingi bilioni 2 wakati huo tena ulikuwa na majukwaa.
 
Tusilaumu sana mkuu,hela ni hela tu hakuna mjinga kwenye Hela,labda mchakato wa transformation ukikamilika itakua rahisi kumuwajibisha..sasa hivi atoe billion 30 yeye kama nani???maneno mengine tusikilize tu na tuyaache maana ni habari za kuwaambia watoto..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…