Tujihadhari na yaliomkuta Patrick Mafisango

Poleni wote kwa msiba huu lakini katika hii Thread ya huyu jamaa nimependa sana huu usemi (jueni maisha ni akili na mpira ni nidhamu) R.I.P Patrick Mafisango!
 
Wabongo wengi wanatabia ya kusikiliza ushauri wakati wa tukio but baada ya muda husahau kila kitu thanks kwa kuwakumbusha mweye sikio asikie! RIP PATRIC MAFISANGO!
wanadamu tumeumbwa kusahau bila hivyo sura zetu zingekuwa kila siku ni za simanzi,au za kutoa machozi,na Mungu alituumba kwa maksudi kuwa wasahaulifu,la sivyo ningekuwa kila siku nalia kuwakumbuka wazazi,jamaa waliotangulia mbele ya haki na nyuso zetu zingekuwa na reception zilizochoka kwa kukumbuka yanayotakiwa kusahauliwa,watu wanasahau kama kuna megawatt wanajilipua sembuse maji ya Mchikichini au maji ya pale Veterinary machinjioni
 
Akili za wachezaji wetu sometimes ni kama; bongo flava artist, ki-single kimoja mtaani hatulali.
Wengi wetu tunaokimbilia ni baada ya kushindwa maisha huko kwengine.
Nidhamu ya kazi hakuna kabisa.
Waigizaji nao ndio hao kina kanumba (Rip).
Hapo mnategemea tupate kina Christian Reinaldo na Messi,
Au kina Tupack watokee bongo, thubutu
Mitungi na Mikasi ndicho wakiwazacho, zaidizaidi labda kuendeana Mlingotini Bagamoyo.
 
Nasubiri wale waandishi wa udaku waje na zile hypotheses zao : katolewa kafara!, kauawa na freemanson wenzake!‎؛‎ sudan walimpiga jini, waliokuwa kwenye gari lake walimmalizia!!!!!.................. RIP BRO...............
 
Back
Top Bottom