Tujihadhari na dhambi ya tamaa mbaya katika taifa letu

Emmanuei

Member
Feb 20, 2023
18
20
Leo mitandaoni Kuna gumzo kubwa litokanalo na walaka wa katibu mwenezi wa CCM, Sophia Mjema ambaye siyo wa kwanza katika Taifa hili kuwatamkia Watanzania masuala yahusuyo uongezeaji wa muda kwa viongozi wetu wa kitaifa.

Mlolongo huu wa matamko/walaka kutoka kwa Watanzania wenzetu unatutia shaka hasa sisi wazalendo halisi wa Taifa hili kutokana na historia, mila na tamaduni zetu ambazo zimetupelekea kuheshimu ushauri maelekezo na hata maisha halisi ya waasisi wetu hasa katika mema mengi kwakweli ambayo pasinashaka yanaonekana likiwemo suala la kupeana kijiti bila kuathili umoja mshikamano na amani ya inchi yetu.

Sasa siala la ukiukaji wa katiba na uvunjaji wa Sheria mila na desturi zetu unao endelea kukua na kustawi na hasa katika masuala ya ukomo wa madaraka ya uongozi wa urais unatufikirisha zaidi sana katika umuhimu wa uwepo wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi na pia Mahakama kuwa huru kweli kweli ili ziweze kutafathili vilivyo Katiba, Sheria, kanuni na taratibu zetu.

Hivyo ni muhimu kuwa roho hii ya TAMAA inapaswa kukemewa na kila mzarendo wa inchi hii, ikiwa ni pamoja na kuwaomba watanzania wote bila kujali rangi itikadi kabila au mahali mtu atokeapo kuungana kukemea mambo haya kujirudia tena.

TAMAA MBAYA SI WIZI TU, AU UNYANG'ANYI.
 
Hekima ilianzia Jerusalem na itamalizikia huko huko.

Dunia imeshabadilika Ujue Watu wataanza kuukimbia Uongozi.
 
Tutafakari zaidi hasa kwanini Leo na siyo mwanzo kule kwa waasisi wetu ambapo muda ulikua unaruhusu zaidi . The time will tell.
 
Back
Top Bottom