Tujifunzeni kusoma mikataba yoyote kabla ya kuweka sahihi

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
20,234
47,000
Ebwana wanaJF Mzuka!

Wengi wetu naamini kabisa tunapapara na vitu ikifika kuukubali mkataba na kuweka sahihi hasa wa Kazi na mikopo na kazi. Hatuchukui muda kuusoma na kuuliza maswali. Huenda labda ni desperation.

Halaf wanaotoa mikataba wajanja sana hasa wa mikopo. Unakuta mikataba ina kurasa nyiingiii na sehem zingine maandishi madogomadogo hili ikuchoshe. Sasa ikukute una papara na si mvumilivu unawahi kuweka sahihi nakujifunga.

Pia mikataba ya Kazi hivyo hivyo ukimwaga wino umeshajifunga no excuse. Ndio maana unakuta wakati hule Kigangwala alipofungia watu geti eti walilalamika wanaishi mbali wakati mkataba unasema wazi muda wa kuripoti kazini. Siwalaumu sana kwasabab ni hulka yetu.

Tuwen makin sana tunapopata na kuipitia mikataba kabla hatujaweka sahihi hili kuepuka mambo yanapotutokea puani na kuambiwa hil neno ambalo nalichukia "am sorry my/our hands are tied, nothing i/we can do"

Nawakilisha
 
Tena hii mikataba ya kazi ndio huwa hatusomi, ukizingatia ulitafuta kazi kwa miaka kadhaa tokea uhitimu, yaani ukipewa ule mkataba badala ya kusoma unachofanya ni nikuhoji hivi: SAMAHANI NATAKIWA KUSAINI WAPI. hahahahaha. lakini jambo lingine ni kwamba hiyo mikataba ameiandaa mwajiri wewe hujashiriki kuandaa kwahiyo hapo huwezi kusema toa kipengele hiki weka hiki, sana sana ni kwamba ukitaka kazi saini hutaki potezea
 
nimeshudia Wengi mimi nikiwamo. Yani ikitokea hitilaf kazini hata ukimpeleka mwajir mahakaman kumshtak atakushinda tu. Unaona hata nchi yetu inavyodhulumiwa na hii mikataba ambao inasahiniwa gizan angalia hadi Magu his hands are tied nothing he can do no matter how hard he tries and the clear conscious in him
 
Back
Top Bottom