TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,434
- 3,553
Alikuwa anazama.
Na hakuna aliyegundua...
Hakuna, isipokuwa yeye mwenyewe.
Ilikuwa Juni 2022, kwenye Mashindano ya Dunia huko Budapest.
Anita Álvarez, mwogeleaji wa sanaa kutoka Marekani mwenye asili ya Ki-Mexico, alikuwa akifanya onyesho lake kwa ustadi wa hali ya juu.
Lakini maonyesho yalipoisha… hakupanda juu kuvuta pumzi.
Alikuwa amepoteza fahamu.
Mwili wake ulibaki juu ukielea kwa sekunde chache, kisha ukaanza kuzama.
Polepole. Mpaka chini kabisa ya bwawa.
Watazamaji hawakugundua. Wala majaji.
Kila mtu alikuwa akipiga makofi.
Lakini kocha wake, Andrea Fuentes, aligundua.
Alimjua Anita—alijua muda halisi anaotumia kurudi juu baada ya onyesho.
Alihisi moyoni mwake kwamba kuna jambo si sawa.
Bila kusita hata kidogo, aliruka ndani ya maji.
Akiwa amevaa nguo kamili—na viatu pia.
Aliogelea moja kwa moja na kuzama hadi chini, akamshika Anita kiunoni,
akamrudisha juu.
Aliokoa maisha yake.
Hadithi hii ilinifanya kuwaza…
Ni nani anayekujua vya kutosha kugundua kwamba hauko sawa, hata kama bado unacheka?
Ni nani ambaye angeweza kujitosa majini kwa ajili yako bila kusita, pale unapokuwa huna tena nguvu ya kupumua?
Na zaidi ya yote…
Je, wewe unaweza kuwa mtu huyo kwa mtu mwingine?
Je, uko karibu vya kutosha katika maisha ya wapendwa wako kiasi cha kuhisi pale wanapoanza kuzama?
Au wewe ni mtazamaji tu, unapiga makofi, bila kufahamu kwamba ndani yao, wanapotea?
Katika maisha haya, sote tunahitaji mtu ambaye haoni tu uso wetu— bali anatugundua kwa kweli.
Mtu anayejua pale tunakaribia kukata tamaa,
na anayekuwa na ujasiri wa kuruka ndani ya bwawa na kutuokoa.
Credit: Emmanuel Akyoo