Tujifunze ya Afrika Kusini, Kumhoji Rais sio Kujipendekeza Kinafiki

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,335
72,799
Nimeipenda style ya Afrika kusini ya wabunge kuweza kumhoji Rais pale anapohisiwa kakiuka katiba au maadili ya cheo chake bila woga wala unafiki. Mfano wa karibuni ni huu uteuzi wa Naibu waziri wa Fedha ambao habari zimenaswa kuwa uteuzi wake ulikuwa na shinikizo la familia ya matajiri. Rais Zuma kawekwa kati atoe ufafanuzi bila ya kumuogopa wala kumvunjia heshima.
Hiyo ni tofauti na hapa kwetu, ambako hakuna awezaye hata kukosoa ila ni sifatuu,mapambio,
 
Tanzania haiwezekani hilo kwanza tu wakitaka rais kuhutubia lazima jeshi la polisi na kikosi cha mbwa kiingie ndani ya bunge
 
Tanzania Yule mama ataomba miongozo kwa spika zaidi ya michango Yake refer ya sugu mizuka alivyopambana
 
Tanzania tuna shida moja tu.....Katiba sio ya wananchi ni ya mtu mmj ndio alioandika imempa nguvu za ajabu...Mr Pres
 
Mkuu katiba yao iko vzuri but yetu inampa magu kufanya lolote atakalo Bila mtu kuhoji kuhoji tu makonda anakutupa ndani lakini hahii itafikamwisho tu sisi wote nchi hii ni yetu ipo siku
 
Mimi nafikiri sio katiba pekee ya kulaumu, hata hulka zetu pia. Ina anapojitokeza yeyote wa kumkosoa Rais anaonekana kama adui, lakini haohao wamsifiao akiharibikiwa wanamuachia Rais binafsi lawama kama ilivyokuwa kwa JK.
 
Mimi nasisitiza kwamba vyama vyetu vya upinzani viwe mfano wa uwajibikaji ili tuweze kuwa na uhakika kwamba tukiviweka madarakani havitafanya yaleyale ya CCM. Kwa jinsi upinzani wetu ulivyo ni kwamba hata huko maamuzi ya viongozi hayahojwi, ukihoji tu utaitwa msaliti na kutimuliwa.
 
Unajua kuwa wanachama wa vyama vya siasa hawazidi hata 20℅ ya raia wote na kujiunga chama cha siasa ni hiari? Chama kama kina katiba na uongozi mbovu sii mnakikimbia na kukiacha kama TLP?
 
Back
Top Bottom