Tujifunze kwa wairan

Tujifunze kwa wairan

Nikweli kabisa mkuu, maana yule mtoto wa ki Iran Najrat alikua na shuzi miksa limeibana hijab sio poa....😋
 
Sijajua umekusudia nini lakini hao jamaa hawakuanza kujiimarisha leo ni swala la kizazi hadi kizazi. Tunatakiwa kurithishana ujasiri na imani kwa kila hatua.
Iran wamewekeza sana kwenye Elimu ya Sayansi na pia kuboresha sana shule zao za Uma na vyuo.
Hata sisi tunaweza kwa kuanza sasa kuajiari waalimu wa kutosha WENYE SIFA za kufundisha Hesabu, na wa masomo yote ya Sayansi wafike angalau 80% tofauti na sasa ambapo wapo takribani 30 to 40% ya mahitaji.
Tukifanya hivyo ndani ya miaka 10 Nchi intakuwa na badiliko makubwa hata namna ya kufikiri itabadilika...
 
Iran wamewekeza sana kwenye Elimu ya Sayansi na pia kuboresha sana shule zao za Uma na vyuo.
Umenena vema.

Hata hivyo, Uwekezaji kwenye sekta ya Elimu uendane na mabadiliko ya fikra kwenye jamii zetu.
Mpaka sasa watu wetu wanasoma ili wapate kazi zenye mishahara mikubwa.

Hawana uwezo wa kufanya tafiti zenye maslahi kwa taifa na vizazi vijavyo.
Irani wameshaondoka huko.

Ndiyo maana wanazalisha drones, makombora na kujenga miundombinu mingi ya chini ya ardhi kulinda watu wakati wa hatari na pia kuhifadhi silaha.

Lakini majirani wa Irani ingawa wanazo pesa za kutosha kufanya yote hayo wameshindwa, kwakuwa Elimu yao ina waaminisha kuwa mwenye jukumu la kuwalinda .ni Marekani tu.
 
Nilisikia zamani Jeshi la wanaccm lilikuwa linatengeneza makombora na magari ya kivita yaliitwa nyumbu pamoja na Meli za kivita za kufyatua makombora kutoka pwani ya dar hadi Tanga.Hiyo ilikuwa enzi za nyerere baadae huo mradi ukafa kwa nini?
 
Back
Top Bottom