Tujifunze kwa huyu mama

Tujifunze kwa huyu mama

gwahe

Senior Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
147
Reaction score
84
Wana MMU Jumapili ni siku ya familia.

Tunaweza kujifunza maisha ya upendo kupitia kwa mama huyu ambaye nilimuuzia kiwanja maeneo ya Mbezi chenye thamani ya million 130.

Huyo mama ni advocate, baada ya maelewano na maamuzi ya kuamua kununua kiwanja, kitu cha kwanza kukifiria, aliniambia HATAWEZA KUMWELEZA HUSBAND wake mpaka hapo atakapokamalisha ununuzi.

Nilimuuliza kwa nini? Asiweze kumshirikisha mumewe? Alinijibu, anamwelewa husband wake vizuri maana ataanza complain kwa nini anunue kiwanja kwa bei kubwa.

Baada ya siku tano, tulikamilisha mauziano na kusign mkataba na kulipana pesa bank.

Kitu cha ajabu ambacho sikukitegemea, mkataba wa mauziano ulikuwa na majina mawili. Hii ina maana yeye huyo mama na husband wake ndiyo wanunuzi wa hicho kiwanja. Ingawa pesa ametoa wife tu. Na baada ya siku tatu husband wake alipelekwa na kuonyeshwa kiwanja na mikataba yake.

Je kwa nini wanawake wengi ndani ya ndoa hawawezi kufanya kama huyo mama?

Je kwa nini wanaume hawapendi kuwashirikisha wake zao mambo yao mengi ya maendeleo?

Tatizo nini?
 
Haya wale wenye wake na waume tiririkeni...

Hata hivyo kila familia ina taratibu zake za namna ya kuhandle mambo yao mkuu...
 
hakuna kuaminiana sasa hivi.....mie anko wetu amefariki kwa ajali.....na alipofariki mambo yake mengi ndiyo yamegundulika.....alikopa mil 30 hata mkewe hajui.....na haijulikani hiyo hela kapeleka wapi......kwahiyo ndiyo hvyo.........
 
mmmh!!! ndoa zina mengi na zinatofautiana, so siwezi walaumu wasofanya kama huyo mama
 
Kumbe ndo maana ukamlalia kwa 130 kwamaana mumewe hakuwepo, kwa hiyo ndo umekuja kutuonyesha furaha yako sio? Bahati yako kwamaana huyo mwanaume angekuwepo hapo ungekula m 60 tu.
 
Kwa sababu zile zile zinazowafanya wanaume wanaponunua viwanja waandike majina yao tu na sio majina yao na wake zao......



Je kwa nini wanawake wengi ndani ya ndoa hawawezi kufanya kama huyo mama?? Je kwa nn wanaume hawapendi kuwashirikisha wake zao mambo yao mengi ya maendeleo.? Tatizo nn??:?
 
Mahusiano ni ulimwengu wa kipekee sana. Ina kanuni na taratibu zake kwa ajili ya ku accomodate mwenzako! Ni ulimwengu pekee ambao kila dakika hufanyika amendment ya hizo taratibu tena bila makubaliano maalum na bila kikao maalum, sasa ku catch up amendments ya kila dakika ni ngumu kwa wengi; kwa wale wanaoweza ku catch up amendment hudumu na kudumu kwa kudumu kwenye ulimwengu huu mtamu zaidi kuliko hela!
 
Tatizo kubwa ni kwamba hakuna muongozo kwenye ndoa katika masuala ya pesa. Hii hupelekea kila mtu kujifanyia anavyowaza. Na suala kubwa si uaminifu bali zaidi ni namna watu walivyolelewa kuhusu masuala ya fedha. Ukikutana na mwanaume ambaye baba yake alikuwa hashirikishi familia kwenye pesa usitegemee yeye atafanya hivyo hata kama anamuamini mkewe vivyo hivyo ukikutana na mwanamke ambaye mama yake alikuwa anafanya mambo yake pembeni ni rahisi sana na yeye kuwa na tabia hizo.
 
Bora umetuletea "uzi" mzuri juu ya ndoa, maana kila siku, "Ooooohhh ndoa ndoano, mwenzenu yamenishinda, na wengine mnatendewaga kama mimi". Kwa uzi huu tunapata picha kuwa kuna mengi mazuri ndani ya ndoa.
 
Kila ndoa zinautaratibu wake toka mwanzo mnapangaje/kushirikishana maisha yenu ya ndoa kama mnaishi maisha ya changu changu au chake chake mwisho wa siku kila mmoja atakuwa na kiwanja , nyumba, gari yake
 
Wana MMU....Jumapili ni siku ya familiar.

Tunaweza kujifunza maisha ya upendo kupitia kwa mama huyu ambaye nilimuuzia kiwanja maeneo ya Mbezi chenye thamani ya million 130.

Huyo mama ni advocate, baada ya maelewano na maamuzi ya kuamua kununua kiwanja,kitu cha kwanza kukifiria, aliniambia HATAWEZA KUMWELEZA HUSBAND wake mpk hapo atakapokamalisha ununuzi. Nilimuuliza kwa nn?? Asiweze kumshirikisha mumewe?? Alinijibu, anamwelewa husband wake vzr maana ataanza complain kwa nn anunue kiwanja kwa bei kubwa......Baada ya siku tano, tulikamilisha mauziano na kusign mkataba na kulipana pesa bank.

Kitu cha ajabu ambacho sikukitegemea, mkataba wa mauziano ulikuwa na majina mawili. Hii ina maana yeye huyo mama na husband wake ndiyo wanunuzi wa hicho kiwanja. Ingawa pesa ametoa wife tu. Na baada ya siku tatu husband wake alipelekwa na kuonyeshwa kiwanja na mikataba yake.

Je kwa nini wanawake wengi ndani ya ndoa hawawezi kufanya kama huyo mama?? Je kwa nn wanaume hawapendi kuwashirikisha wake zao mambo yao mengi ya maendeleo.? Tatizo nn??:?

Hivi unauhakika na hilo neno ulilotumia? Hebu tazama tena nnauhakika silo, rekebisha.
 
Back
Top Bottom