Tujifunze kutembea na pesa ya ziada

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,700
9,779
Dakika chache zilizopita nikiwa hapa dukani kwangu, nimetoka kutazama kisa cha kufurahisha na kuuzunisha kwa wakati mmoja!

Mwanaume mmoja wastani miaka 25 hadi 30 alikuwa akikatiza maeneo haya akiwa kwenye baiskeli yake iliyokuwa inaenda kwa kasi! Ghafla bin vuu kamparamia mwanamama aliyekuwa amebeba tray zake nane za mayai yaliyochemshwa na kupakwa chumvi kwa juu juu tayari kwa kuwaburudisha wenzetu waliotoka kwenye mfungo siku chache nyuma zilizopita!

Kwa haraka haraka, tray moja lina mayai 30, tray nane zilizokuwa juu ya kichwa cha yule mwanamama zilikuwa na jumla ya mayai 30×8, sawa na mayai 240, kila yai la kuchemshwa anauza 500 na hapo alikuwa anaelekea gengeni tayari kwa kuanza kuuza kwa ajili ya kupata pesa ya mahitaji ya familia! Hivyo pesa iliyokuwa juu ya kichwa cha yule mwanamama ni 120,000 Tsh

Ilisikika sauti ikitamka kwa nguvu "kyiruuuu" hakuna muda wa kupoteza, watu tulisogea eneo la tukio na kujivika uhakimu kwa ajili ya kutatua kesi!

Zilisikika kelele za "mlipe! Mlipe! Alipe huyo!. Baada ya kuweka mambo sawa ilionekana kuwa mwanaume yule hakuwa na hata senti moja mfukoni! Hivyo mwanaume mwingine mwenye kitambi na midomo iliyojawa mafuta mafuta alisika akisema "kwani hiyo samsung uliyonayo ni aina gani?"

Kijana alijibu kwa masikitiko makubwa! Kisha furushi yule akapendekeza, "kama utakubari niichukue kwa laki na nusu nikupatie cash ili ulipe deni itapendeza zaidi". Sauti ya upole ilisikika ikisema, "hii simu ni ya laki nne na sitini mzee". Lakini baada ya muda malipo ya laki na nusu yalifanyika, na ndipo kiasi cha 120K kilihamishwa kuelekea mikononi mwa yule mwanamama!

Ndipo kelele zilianza kupungua! Huku watu wakisambaratika kuelekea kwenye biashara zao! Mimi nikarejea dukani kwangu huku nikimtazama mwanaume yule akiweka akiba yake ya 30K mfukoni ili imsaidie kama ikitokea akaparamia manisinia ya karanga huko mbele!

Funzo:
Pesa ya akiba ni muhimu pindi unapotoka ndani! Hata ikiwa ni 5,000 sio mbaya! Huwezi ijua leo yako itakuwa vipi! Huenda ukaparamia sahani za watu sokoni!

Nawasilisha:
 
si bora alikuwa na hiyo simu,maana imemsaidia.

simu ya gharama wastani angeweza hata kumsusia huyo mama mwenyewe akafate hela na angeeleweka,fikiria ana kishwaswadu.
 
Dakika chache zilizopita nikiwa hapa dukani kwangu, nimetoka kutazama kisa cha kufurahisha na kuuzunisha kwa wakati mmoja!

Mwanaume mmoja wastani miaka 25 hadi 30 alikuwa akikatiza maeneo haya akiwa kwenye baiskeli yake iliyokuwa inaenda kwa kasi! Ghafla bin vuu kamparamia mwanamama aliyekuwa amebeba tray zake nane za mayai yaliyochemshwa na kupakwa chumvi kwa juu juu tayari kwa kuwaburudisha wenzetu waliotoka kwenye mfungo siku chache nyuma zilizopita!

Kwa haraka haraka, tray moja lina mayai 30, tray nane zilizokuwa juu ya kichwa cha yule mwanamama zilikuwa na jumla ya mayai 30×8, sawa na mayai 240, kila yai la kuchemshwa anauza 500 na hapo alikuwa anaelekea gengeni tayari kwa kuanza kuuza kwa ajili ya kupata pesa ya mahitaji ya familia! Hivyo pesa iliyokuwa juu ya kichwa cha yule mwanamama ni 120,000 Tsh

Ilisikika sauti ikitamka kwa nguvu "kyiruuuu" hakuna muda wa kupoteza, watu tulisogea eneo la tukio na kujivika uhakimu kwa ajili ya kutatua kesi!
Zilisikika kelele za "mlipe! Mlipe! Alipe huyo!. Baada ya kuweka mambo sawa ilionekana kuwa mwanaume yule hakuwa na hata senti moja mfukoni! Hivyo mwanaume mwingine mwenye kitambi na midomo iliyojawa mafuta mafuta alisika akisema "kwani hiyo samsung uliyonayo ni aina gani?" Kijana alijibu kwa masikitiko makubwa! Kisha furushi yule akapendekeza, "kama utakubari niichukue kwa laki na nusu nikupatie cash ili ulipe deni itapendeza zaidi". Sauti ya upole ilisikika ikisema, "hii simu ni ya laki nne na sitini mzee". Lakini baada ya muda malipo ya laki na nusu yalifanyika, na ndipo kiasi cha 120K kilihamishwa kuelekea mikononi mwa yule mwanamama! Ndipo kelele zilianza kupungua! Huku watu wakisambaratika kuelekea kwenye biashara zao! Mimi nikarejea dukani kwangu huku nikimtazama mwanaume yule akiweka akiba yake ya 30K mfukoni ili imsaidie kama ikitokea akaparamia manisinia ya karanga huko mbele!

Funzo:
Pesa ya akiba ni muhimu pindi unapotoka ndani! Hata ikiwa ni 5,000 sio mbaya! Huwezi ijua leo yako itakuwa vipi! Huenda ukaparamia sahani za watu sokoni!

Nawasilisha:
Sasa hiyo alfu 5 ya akiba ingemsaidia nini huyo mwamba kwa kesi hiyo ?

Muhimu tutembee tukijua kwamba hatuna uwezo wa kucontrol kila jambo la baadae,na kila jambo linalotokea lina makusudi yake.

Mimi wallet yangu natembea na 50K kushuka chini kwa mujibu wa uweO wangu.

Alafu pia huyo jamaa wa mayai angechukua hayo mayai kwa sababu sidhani kama yalivunjika,angeyachukua akayakosha na kuendelea na bizness au akayale mwenywwe kama chakula.
 
Mjuba kachukua simu janja kwa bei ya kuokota,

Kweli kufa kufaana.

Ila maisha haya Yana fumbo kubwa sana,unaweza sema waganga wa kienyeji hawafai lakini Kuna muda utawafuata wenyewe
 
Mkuu, kama pesa ya kula mlo mmoja tu inakua changamoto.... je hiyo ziada itatoka wapi..??😎
 
Hayajakukuta Ndugu yangu, au labda kama umeandika kufurahisha baraza.
Nikwel ukisemacho , ila kama balance IPO tembea nayo , hapa hatutizami shida TU, hua na vyabure hupatika ,kuna siku utakutana na kitu Cha M1knauzwa alf50 na uliziacha nymban zle helaaa utabak ukishangaa TU.
 
Sasa hiyo alfu 5 ya akiba ingemsaidia nini huyo mwamba kwa kesi hiyo ?

Muhimu tutembee tukijua kwamba hatuna uwezo wa kucontrol kila jambo la baadae,na kila jambo linalotokea lina makusudi yake.

Mimi wallet yangu natembea na 50K kushuka chini kwa mujibu wa uweO wangu.

Alafu pia huyo jamaa wa mayai angechukua hayo mayai kwa sababu sidhani kama yalivunjika,angeyachukua akayakosha na kuendelea na bizness au akayale mwenywwe kama chakula.
Mkuu unaweza kula mayai ya kuchemsha trei 8?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tembea na Mastercard, Visacard au eMoney...

Kutembea na pesa taslimu unafanya uwe na wasiwasi wa kuporwa au hata kupoteza...
Kuna jamaa alipokea kikoba juzi kati laki sita akavamiwa kwake na kuuwawa.

Najiuliza kwanini watu wanapenda kukaa na cash wakati kuna mpaka mobile money unafanya transactions muda wowote mahali popote.
 
Back
Top Bottom