Tujifunze kunyamaza

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
1. Kunyamaza wakati fulani maishani mwako siyo kipawa bali ni nidhamu (Wathesalonike 4: 11).

2. Nyamaza unapohisi hasira (Mithali 14:17).

3. Nyamaza unapokuwa huna taarifa ya kutosha au ukweli kuhusu unachotaka kusema (Mithali 18:13).

4. Nyamaza unapokuwa ni wakati wako kusikiliza na kujifunza (Mithali 13: 1).

5. Nyamaza ukigundua kwamba maneno yako yataleta picha mbaya (Mithali 17: 27).

6. Nyamaza ukijua kile unachotaka kusema kitaharibu jina na sifa ya mwenzio (Mithali 16: 27).

7. Nyamaza ukijua utakachosema kitaharibu urafiki na kujeruhi mwenzako (1Wakorintho 15: 33).

8. Nyamaza ukigundua kwamba utaaibika baadaye kwa sababu ya ulichokisema (Mithali 8:8).

9. Nyamaza ukijua unachotaka kusema kitamdhalilisha Mungu, wewe mwenyewe au familia yako (1Petro 2: 21-23).

10. Nyamaza ikiwa wakati ulio nao ni wakati wa kazi (Mithali 14: 23).

11. Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu (Mithali 21: 23).

Mungu akupe neema ya kujenga nidhamu ya kunyamaza kwa maana maneno ya kinywa chako ni mtego kwako (Mithali 6:2).
Niwatakie tafakari njema
 
Juzi nilishindwa kunyamaza baada ya kulipa nauli kwenye kapricom nakaribia kushuka dada ananiambia aliye chukua nauli yako ameshuka mtera kwa hiyo mm siwezi kukupa chenji. Niliwasha moto wa kukafokea kale kadada mpaka nikajistukia maana siyo tabia yangu.

Tatizo binadamu mwenzako anaweza kkufanya ukorome kwa hasira. Bible yenyew inasema usibaki na hasir mpaka Jua linazama
 
Miongoni mwa vitu nilivyojifunza hapa duniani ni hichi:

Don't you ever stop advocating for yourself
 
Alipoimba sadala alishukiwa kwa maneno yoote na kutukanwa bila kusahau kufanyiwa kampeni ya kukosa tuzo BET
 
Ni nzuri ila Kuna wakati unaona unaonewa, hapo hapana siwezi kunyamaza lazima nijiwekee uwajili mimi mwenyewe ikiwezekana
 
Back
Top Bottom