TUjifunze kukubali ukweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUjifunze kukubali ukweli

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dena Amsi, Mar 3, 2011.

 1. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Salut!!

  Nimesikia hiki kisa kimenisikitisha sana.

  Mwanaume alikuwa na mpenzi wake wakakorofishana mwanaume kamweleza msichana kuwa kuanzia sasa mimi na wewe basi kwa njia ya simu.

  Msichana kusikia hivyo kapanic kweli kamwambia Mwanaume kuwa "We need to talk" jamaa kakubali kamwambia njoo tuzungumze. Msichana kafika kabla ya mwanaume na kwa kuwa alikuwa na ufunguo wa nyumba kaingia kumsubiri.

  Jamaa alipofika kamweleza kuwa kutokana na tabia yako ya kuwa na wanaume wengine mimi nimeamua sikuhitaji tena endelea na maisha yako na mimi na maisha yangu msichana kusikia hivyo kaja juu na hasira na kachukua laptop ya mwanaume katupa nje (gorofa ya pili).

  Mwanaume kabaki na msimamo ule ule kuwa sikuhitaji tena fanya chochote unachotaka lakini sitabadili msimamo wangu. Cha kushangaza zaidi msichana kaondoka na hasira na kurudi baadae kachukua nguo, vyeti na vitu vingine vya mwanaume kachoma moto na kuondoka.

  Najiuliza kwanini huyu msichana hakubali kuwa kaachwa??? Ni lazima uendelee kuishi na mtu ambaye hakuhitaji????. Kwanini asikubali kuwa hahitajiki tena???

  Hapa ndipo pale lile swala la wanawake hupenda toka moyoni na wanaume hupenda kwa macho linapokuja na kuwa gumu.

  Tujifunze kukubali ukweli na upendo wetu usizidi kipimo, maana hata ukiambiwa mimi na wewe basi usiumie sana kiasi hiki.

  Hiki ni kisa kimetokea huku nilipo na huyu msichana anapelekwa mahakamani leo kwa kosa la uharibifu wa mali za huyu mwanaume.

  Nawasilisha
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kwa hiyo unamaanisha kuwa hilo swala la kuwa na wana ume wengine kama ulivyosema sio ukweli??
  Ila jamaa alikuwa hamtaki tu??
  Kama ni hivyo basi hajamtendea haki huyu msichana/mwanamke kabisa.
  Anyway, wanasema penzi ni kiti cha basi ukiondoka wanakaa wengine.
   
 3. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nachosema mimi ni kuwa kwanini msichana hataki kukubali kuwa jamaa hamuhitaji tena?? Ndio swali langu mpaka amefikia hatua hiyo ya kumkomoa mwenzie na kumchomea vitu vyake laptop kaharibu nguo, vyeti hapo ndo pagumu
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Huyo dada nae kama kweli alipenda toka moyoni kwa nini alikuwa na wanaume wengi??
   
 5. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Atakubalije ukweli wakati bado anampenda mwanaume?Tuwe wakweli na tutambue kuwa mtu yeyote ambaye anakuwa hajajiandaa kwa jambo fulani na linapokuja kwake huwa anakuwa haamini kinachotokea na si rahisi kukubaliana na ukweli,hebu jaribu kumuuliza mtu aliyewahi fukuzwa kazi wakati hakuwa na hata chembe ya taarifa.
  Kitu ambacho sijapenda tu ni kuharibu mali za mwenzake,ila inawezekana pia laptop iliyovunjwa alichangia katika upatikanaji wake na akaona nayo ni bora ivunjike ingawa kitendo hicho si chema ila ndio hasira za kukataliwa zilipoenda.
   
 6. P

  Pomole JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo mwanaume nae *****,mtu atupe laptop unamwangalia tu, achome nguo unasema hewala achome vyeti unasema asante!!!jamani si li ***** hilo!!!Utashindwa vipi kumdhibiti mtu aharibu vitu vinavyohusisha ustawi wako!!!
  Hii ishu umeiweka kiupande lakini ni two way traffic-wapo wanaume ambao nao wameachwa lakini wakang'ang'ania penzi-hii inatokana na kutoamini kutokana na jinsi ulivyompenda na kumchukulia mwenzio kwa moyo wote
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Nachozungumzia hapa ni kwamba huyu msichana kama anampenda huyu mwanaume iweje awe na wanaume wengine na pale jamaa anapofikia uamuzi msichana hataki kukubali. By the way hii nimesikia kwenye taarifa ambapo msichana hajazungumza bali ni kesi ambayo mwanaume amelalamika kuharibiwa vitu vyake.

  Swala linakuja kuwa mtu kashasema hakutaki wewe bado unamng'ang'ania wa nini?? Kubali yaishe kwani yeye ndo uhai wake bana??? Na huwezi kuishi bila yeye??
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Katika hali ya kawaida sio rahisi kujua kama huyo dem alipenda kweli tokea moyoni. Inawezekana alikuwa anajutia atakavyozikosa pesa zake...
   
 9. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
   
 10. LD

  LD JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hasira hasira, kwa nini huyo dada anamharibia vitu vyake huyo kaka!!!
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  We bwana acha tu yote tisa hivyo vyeti tu ndo mie vimenishangaza kweli huyu bidada anaonekana kama sijui vipi vile aahhh simuelewi kabisa
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wadada wa design hii wanakuwa na wanaume zaidi ya wawili kwa marengo tofauti
  Huyo mwenye laputopu yawezekana alikuwa ndo ATM sasa kuona hivyo misaada imeisha ndo maana kapanic
  Huyo mwingine ni wa kumkuna binti wa watu pindi anapo elemewa na kiu anamfuata huyo wa kumfikisha kunako.
  Kinacho muumiza huyo binti ni jinsi gani ataweza kutatua mahitaji yake ya kila siku kama kwenda saloon, kula mishkaki na chipsi bila kusahau vimiminika kama Redds n.k atavimiss maana kuja kupata kidume kingine cha kumwezesha ni kazi ingine tena ambayo inahitaji thread ingine.
   
 13. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Hii imenikumbusha nikiwa chuoni enzi za mwaka ule 1947.. wanawake walikuwa na wanaume wenyewe wakiwaita... 1. Financer, huyu kazi yake ni mshiko. 2. Mzee wa ngwini, yeye huyu kazi yake ni homework, assignment na mambo yote ya academic. 3. Mpenzi kutoka moyoni, ambaye anapendwa jinsi alivyo. Kwa hiyo nadhani huyo dada alikuwa amewa categorize hawa wanaume kwajinsi hiyo. Sasa huyu probably financer aliposhituka akaona anamharibia mipango yake ya maisha kwenda sawia. Huwezi ukasema unampenda mtu alafu unagawa hovyo alafu utake mwanaume akuangalie tuu.
   
 14. RR

  RR JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Methodology za kuachana........
  Naamini huyu jamaa angweza kutafuta njia nzuri zaidi ya kumwambia huyu dada kwamba yamefika mwisho.......
  Kuacha sio kosa...ila njia za kuachana ziangaliwe kwa umakini (kupunguza madhara).
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Amechanganyikiwa ATM kamfungia milango
   
 16. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Fidel bwana umeongea kweli sana
   
 17. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Tatizo ni kukubali na ku move on...... wengi wetu huwa tunakata tamaa pale tunapojua kitu fulani kimeishia ukingoni.........
   
 18. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Mtakatifu unataka kuniambia kakosea kumwambia?? ukweli?? Ulitaka ambembeleze?? No no no no
   
 19. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  hivi inaingia akilini kuchoma vyeti vya mtu????do u knw how severely i struggled to get all thoze certs??aagh hapa naona tunadanganyana...labda uniambie kachoma xerox za vyeti na sio original ones!!
   
 20. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Hilo ndo tatizo kubwa sana
   
Loading...