super black
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 566
- 540
Mhe. RAIS USIMGUSE MPENZI WANGU.
Leo nikiwa ninaperuzi video kadhaa huko YouTube, mara nikaifikia video moja iliyoniacha hoi, nikatamani ku-share nanyi. Ilikuwa mwaka 2014 wakati wa upigaji kura, Chicago, Marekani. Rais Obama alikuwa amesimama karibu na Aia Cooper (msichana aliyekuwa akipiga kura jirani yake).
Katika kile kilichotafsiriwa mwanzo kama wivu wa mapenzi, ghafla tu aliibuka Mike Jones (mpenziwe Aia Cooper), na bila aibu wala soni, alimfikia Rais Obama na kumuonya kwa sauti, "Mhe. Rais usimguse mpenzi wangu."
Ukumbi mzima ukaduwaa kwa fadhaa. Sasa ukisikia wivu ndo huo. Haungalii sura wala mazingira. Haujalishi Rais wala kiongozi wa dini. Ingalikuwa Afrika unadhani Rais au wasaidizi wake wangelifanya nini? Mungu ndiye anajua. Lakini katika hali ya kustaajabisha, papo hapo huku akiendelea kupiga kura, Rais Obama alimjibu Mike: "Hata mimi sikuwa na mpango huo."
Kila mmoja alijikuta akiangua ucheko. Hata mimi nilijikuta nikicheka. Akijaribu kujichekesha ili kuweka mazingir sawa, msichana (Aia Cooper) alijaribu kumtaka radhi Rais Obama, kwa niaba ya mpenzi wake: "Kumradhi. Nakuomba umsamehe. Nilitegemea anatasema jambo la maana..."
Lakini Rais Obama wala hakuonesha kukerwa na kitendo kile, bali alikichukulia kama mzaha tu wa kawaida. Na huku akiwa ametabasamu alisema: "Huo ni mfano wa vijana wengi tu kupenda kunisababishia usumbufu bila hata sababu za msingi."
Kufuatia tukio hilo, huku akiigiza sauti, Rais Obama alimtania Aia kuwa, walau kwa tukio hilo, akifika nyumbani kwao atawasimulia watu: 'Yaani sikuamini kama Mike ni mpuuzi vile... Nilifadhaika sana. Lakini mhe. Rais alichukulia poa tu'.
Baada ya Rais Obama kumaliza kupiga kura yake, alimsogelea yule msichana na kumkumbatia huku akimwambia: "Haya, sasa nibusu tumpe cha kusema."
Na kweli, huku akiendelea kucheka, akiwa amekumbatiwa na Rais, Aia akambusu shavuni. Na baada ya busu, Obama akamalizia kwa kutania, "Sasa ndo apate wivu kiukweli."
Inawezekana kweli Obama hakuwa na mpango huo kama alivyojitetea. Lakini kuropoka kwa Mike, ndo kukamfanya Obama sasa si tu amguse Aia, bali amkumbatie kabisa na kumbusu.
Utani wao huo unaweza kuwa funzo kwetu. Kuhendekeza mihemko pamoja na kutokuchunga ulimi, kunavyoweza kupelekea jambo usilotaka lifanyike ndo likafanyika.
Lakini yote hayo yanabaki hukohuko kwao, sijui Mike angelikutwa wapi baada ya 'kumdhihaki' hivyo Rais wa nchi mojawapo Afrika.[emoji80][emoji80][emoji80]
Mungu Ni Mwema