mndemeimran
Senior Member
- May 7, 2017
- 112
- 74
Lameck alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Mara akakutana na akina Mama watatu ambao walinyoosha mkono kumuomba lift.
Ingawa alikua na haraka lakini aliwaonea huruma na kusimama, sehemu waliyokuwa ilikuwa ni kichakani na kwakuwa alikuwa peke yake hakuona sababu ya kuwanyima lift.
“Samahani Baba, tunaomba utusaidie tunaelekea, Usangi kwenye msiba sasa tumechelewa na magari hamna…” Mama mmoja aliomba.
Lameck aliwaambia waingie kwani hata yeye alikuwa anaelekea huko huko.
Wale akina mama waliingia kwenye gari aliwasalimia na bila hata kuulizwa walianza kujielezea.
“Tunaenda kwenye msiba, kuna Mama mmoja kafariki huko...” Mama mmoja alianza kuongea na mwingine aliendelea…
"...Ahsante sana mwanangu, ni vijana wachache sana wenye roho nzuri kama wewe, wenzako wametupita kama sisi sio watu, magari mazuri kama haya yenu hata hayasimamagi.
Huko tunakoenda kuzika huyo Mama wa watu kaumwa kateseka lakini mtoto wake mwenyewe wa kumzaa hata hakuja kumuangalia, majirani ndiyo walimchangia kupelekwa KCMC…”
“Yaani watoto wasiku hizi mpaka mtu unajuta kuzaa, yule Mama alivyohangaika kumsomesha yule mtoto, alikua anatembea na mfuko wa viazi kwenda kuuza sokoni, anafanya vibarua mtoto mwenyewe hata akili alikua hana kila siku kufeli anarudia madarasa lakini Mama wawatu alivumilia.”
Mama mwingine aliongea.
“Tena basi alitelekezwa na mume wake.” Aliongea Mama mwingine.
“…Alikua mume basi, alizaa na msukuma mmoja aliyekuja kufanya vibarua akamkimbia na kumuacha na mtoto mdogo, Mama wa watu kalea mwenyewe mtoto huyo huyo mmoja ila kajumba kalekale ka nmatope ndiyo Mama wa watu kafia wakati mwanae yuko mjini anakula maisha…!”
“Mama wawatu kila siku analia hata aletewe wajukuu tu awaone…”
“Nakuambia, kila siku anasema mimi sitaki hata pesa zake aniletee tu wajukuu zangu na mimi nifurahie kuzaaa..”
“Kijana yuko mjini wala hana habari! Hawa watoto jamani! Heri Mama wa watu alivyokufa akampumzike, ameteseka sana, nasikia walishamtoa jicho lapili alikuwa haoni kabisa…”
“Usiniambie..”
“Kweli eee, mimi nilienda, majirani walikuwa wamemchangia KCMC wakamtoa jicho lingine, Kansa sio mchezo…”
“Sema kuishi na watu vizuri ni jambo jema sana maana asingekuwa na majirani angekua ashakufa muda mrefu... mtoto wa kumzaa anaweza asikusaidie lakini wa jirani akakusaidia..”
Kule mbele Lameck alikuwa akibubujikwa na machozi, yeye ndiye kijana walikuwa wakimzungumzia na Mama yake ndiyo alikuwa amefariki, tangu alipoenda mjini miaka 15 iliyopita alikuwa hajakanyaga tena nyumbani, alioa bila hata kumuambia Mama yake na hata alipojua aligoma kabisa kumpeleka mkewe na wanae nyumbani.
Maneno ya wale akina Mama yalimuumiza sana hasa walipozungumzia namna Mama yake alivyohangaika naye wakati akiwa mdogo, picha ya Mama yake akilima vibarua, namna alivyokuwa akitoka jasho, picha za mama yake akinyeshewa na mvua, picha za mama yake akatika ofisi za mwalimu mkuu wakati akimtete asifukuzwae shule, picha za Mama yake akimuwashia kibatari usiku ili asome vyote vilimjia akilini.
Alijiona hanathamani kwani hata baada ya kusikia kifo cha Mama yake alishindwa kufanya kitu amabcho Mama yake alikuwa akimuomba kila mara alipompigia simu. Hakutaka kuileta familia yake, hakutaka mke wake na wanae kuona sehemu alipozaliwa kuona hali ya nyumbani kwao hivyo aliamua kwenda mwenyewe mara moja kumaliza mazishi na kugeuza.
Aliumia zaidi aliposikia kuwa kumbe Mama yake alikuwa na Kansa na alitolewa macho yote, hakua na habari hizo kani ni zaidi ya miaka miwili alikuwa hajawasiliana na Mama yake. Mama yake baada ya kumuona hajibu na hamsaidii chochote alichoka kumpigia simu hivyo hata hakujua kuhusu ugonjwa wake.
Machozi yalianza kumbubujika kama maji, alijihisi kama kizunguzungu na kila alipojaribu kulicontrol gari alishindwa, gari liliacha njia na kuserereka mlimani. Alipoteza fahamu na alipozinduka masaa sita baadaye alijikuta amelala hospitalini, aliambiwa amepata ajali, ndipo alipokumbuka ajali ilivyotokea.
Aliulizia kuhusu kina Mama aliokuwa amewabeba akaambiwa walitoka salama bila hata mchubuko, alimshukuru Mungu kwa hilo, hakuwa akisikia maumivu kokote lakini alipojaribu kunyanyuka alishindwa hata kunyanyua kidole. Lameck alikuwa amevunjika uti wa mgongo karibu na shingo hivyo alipooza kuanzia mabegani kushuka chini.
Alipelekwa hospitali kubwa lakini ilishindikana, walimpeleka mpaka nje ya nchi lakini bado ilishindikana. Ni miaka mitatu sasa bado hajaweza kunyanyuka amelala akiwa hawezi kufanya kitu chochote kile. Mke wake ameshaolewa na mwanaume mwingine na wanae wanakuja mara moja moja kumsailimia katika nyumba anayoishi ambayo mkewe ameajiri kijana kwa ajili ya kumhudumia.
Lameck amebaki mpweke marafiki wote wamemtenga, hata wanae wanapokuja kumsalimia humuangalia kama kituko flani, huishia tu kumuonea huruma, hana mtu wakuongea naye. Amelia mpaka amechoka, anatamani kufa lakini hawezi hata kunyanyua mkono kuchukua sumu ajiue. Kila siku ni kulia na kumuomba mama yake msamaha.
*Me sikuambii ujifunze nini hapo,ila we endelea tu kujifanya "Me kwetu Dar"...*
*Kesho nenda kijijini kwenu kamcheki mama*