Pastor Achachanda
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 3,023
- 1,317
TOFAUTI KATI YA URU WA UKALDAYO NA URU WA UCHAGANI
Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
Mwanzo 15 : 7
Najua na ninafahamu kila jina la mahali lina chimbuko na maana kubwa.
Kuna mambo mengi yanashangaza kuhusu watu wa kaskazini hususani Wachaga na jamii zinazofanana nazo na majina ya wachaga yanavyofanana na watu wa zamani waliotajwa katika Biblia. Huu ni mfano mmoja:
Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi sawasawa na vizazi vyao.
Kutoka 6 : 19
Huu ni mfano mdogo tu. Sote tunajua kuwa Mushi ni wachaga. Tena kuna hilo jina la Mali ama maandiko mengine yanataja jina la Mahli. Wapo baadhi wa watu hukiri kuwa jina la Mali, Mahli laweza kutokeza jina likawa Malya. Huko Image Iringa KILALA KIDEWA wakati nafundisha semina ya NAFASI YA MWAFRIKA KATIKA HISTORIA YA UKOMBOZI niliposoma mstari huu angalau kudodosa juu ya waafrika mama mmoja akasema: Kwa kuwa wachaga ni miongoni mwa watafutaji, huenda Mahli na Mushi walikwenda huko Mashariki ya kati ili kutafuta. Baadaye wakasahau kurudi.
Anyway tuendelee kushangaa na kujifunza maana biblia imemtaja hadi Maasai. Soma hapa:
".......na Maasai, mwana wa Azareli, mwana wa Azai, mwana wa Meshilemothi, mwana wa Imeri"
Nehemia 11 : 13 B
TUENDELEE KUJIFUNZA
Sent using Jamii Forums mobile app