Tujengane Kiuchumi

Villarreal 1

Member
Dec 21, 2020
12
20
Habari Wanajamii.Hongereni Kwa Kumaliza Mwaka Salama 2021, Na Pia Nawatakia Mafanikio, Amani, Furaha , Na Afya Njema Katika Mwaka Huu Mpya 2022.

Binafsi Namshukuru Mungu Sana Kwani Kuna Wengi Walitamani Kuona Mwaka Mpya Huu lakini Hawakuweza kutokana na Sababu Mbalimbali, Wapo Waliopata Ajali, Wapo waliotutoka kwa Magonjwa Mbalimbali, Lakini Hadi Naandika Ujumbe Huu Wako Ambao wamelala Kitandani wanageuzwa hawajiwezi ni wa kugeuzwa tu hawajitambui.

Hivyo Wana Jamiii tuna Kila Sababu ya Kumshukuru Mungu Kwani hii Ni Neema TU Mungu Katupendelea.

Haijalishi Unapitia Changamoto gani Mshukuru Mungu.

Kuna Jambo Nataka nililete Mbele Yenu Wana Jamiii , Tulichanganue kwa kina kwa Ufanisi , Utashi , mifano na Kadri tunavyoweza tuache Utani Kwani Kuna Wanajamii wanafaidika na Michango yetu.

Ni Hivi Unawezaje Kumsaidia Mtu ambaye anataka Kujiajiri Ili Hali Hana chochote Cha kuanzia, mfano hana wazo, Hana Mtaji , Hana Elimu, Hana Marafiki wa Faaida N.k,
pekee alichonacho ni Afya njema na Matumaini ya kusonga Mbele kwa Ushindi.
pamoja na Changamoto Hizi Zote zinazompata Mwanajamii huyu Bado Ana Familia inayomtegemea.

Huu Ni Mwanzo wa Mwaka tunamsaidiaje Mtu huyu.

Kumbuka Ushauri Wako waweza kumtoa mtu Mahali Fulani na kumpeleka Mbele zaidi.

Tupeane Maarifa, Uzoefu, ujuzi na Ushuhuda.
kazi kwenu .
 
Mkuu , Kubwa Hapa Mtu Anayepitia kipindi Kama hiki anasaidiwaje? Lengo SI kumjadili mtu Bali mtu mwenye Tabia hizo anasaidiwaje?
Hana Elimu, kuwa Ataajiriwa, Hana lolote Zaid ya Afya njema na Uwezo wa Kupambana
 
kama ni mwanamke na shepu inalipa naweza nikamsaidia kama atakuwa muelewa
Dah Mwanajamiii , Sio Wanawake Wote Wepesi Kama Unavyofikiri wewe Wapo Wanawake Wanajitambua na Hawapendi vitu Vya Bure, Hakika Nakuambia Kama Hujawahi kuktana naye Endelea Kuomba kwa Mungu.
 
Kuna vigezo nitaangalia ....mfano bidii zake kwenye mambo anayoyategemea

Kipaji chake na jitihada kubwa za kufanikisha hayo......hapo nitamsaidia


WE RISE BY LIFTING OTHERS
 
Kesho hasubuhi uwe na elf 10 yako tukutane mwenge palee kuna kazi kiwandani ila pesa ya kuhonga kupata kazi ni hiyo elf 10.. wahi mapema palee saa 12 na mbili utaona watu makundi kwa makundi yanashuka ilee barabara ya viwandani... utaona makundi ya watu yanasimama mule milangoni mwa viwanda simama hapo na sikilizia kazi... usiongee na mtu yeyote mface yule anaeandika majina tu pale gatini .. nakusisitizia chagua gate zuri hata la kiwanda cha soda za kopo au sabuni maana kuna viwanda vya kufua vyuma utapigika mkuu kesho usirudi tena... shukrani mkuu
 
Jambo zuri nikuwa ana afya njema kabisa. Waswahili wanasema "Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe" hivyo nashauri atumie ufahamu na nguvu alizopewa na Mungu kwenda kufanya kibarua sehemu yoyote ile pasipo kuchagua aina yakazi atakayopewa. Baada yakufanya hiyo kazi naamini atakutana na watu wengine watakao mshauri kitu kingine chakufanya kulingana na jitihada zake.
 
Back
Top Bottom