Tujadiliane mikataba ya Simba na migogoro ya kifedha

Tujadiliane mikataba ya Simba na migogoro ya kifedha

Club ya Simba imeingia mikataba mingi tena minono ya mabillioni toka kampuni tofauti ambayo baadhi ya mikataba iko wazi na mingine sio wazi. Apo chini tuone mikataba na thamani zake.
BETWAY:- 20 billion kwa miaka 3
JAYRUTY:- 36 billion
MO foundation:- Sio wazi
MO energy:- Sio wazi
MO cola:-
Pilsner:- 2 billion
MO insurance:- Sio wazi
Air Tanzania:- Sio wazi
KNAUF:- 2 billion
Sandaland:- 3billion + sports items
AZAM:-

Izo ni kampuni ambazo club ya Simba imeingia mikataba nayo lakini tujadiliane kuhusu matumizi ambayo sio wazi na vile vile usajiri na gharama za uendeshaji wa timu ikijumuisha mishahara, usafiri, usajiri na hotels zote anatoa mfadhili wao Tajiri Mo Dewji. Lakini ivi karibuni tumeskia migogoro ndani ya klabu kuwa wachezaji hawalipwi posho mara tajiri hajatoa pesa na mambo mengi ambayo yananipa maswali mengi kuwa izo pesa mabillioni toka kwa izo kampuni zinatumika wapi? 🤦🏻‍♂️
TUJADILIANE KWA LENGO LA KUJENGA TASNIA YA MICHEZO. View attachment 3422991
Wewe ni Mwanachama wa Simba? Au ni shabiki wa Simba JF? Tuwekane sawa kwanza kabla ya mjadala!
 
Wewe ni Mwanachama wa Simba? Au ni shabiki wa Simba JF? Tuwekane sawa kwanza kabla ya mjadala!
Mimi ni mdau wa michezo kwaiyo niko kwaajiri ya maendeleo na kukuza tasnia ya michezo. Tujadiliane bila kuegemea upande wala mahaba na club ili tujenge
 
Mikataba mingi ya Simba inaongezwa sifuri ndio maana katika uhalisia aitekelezeki, mfano wa karibuni ni uo mkataba wa Jai ruuty.
Mkataba ule ata ukiwa mbumbumbu wa kiwango cha mwisho kabisa unaona wazi hautekelezeki kwakua hauna iyo Return kwa mazingira ya apa Nchini.
Hapa= apa
Autekelezeki= hautekelezeki
 
Back
Top Bottom