Tujadiliane kuhusu swali hili?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,316
Hivi mtu aliteuliwa na Raisi kuwa Mbunge na baadae mtu huyo akaamua kujiuzulu ubunge wake kwasababu yoyote ile au akakoma kuwa mbunge kutokana na sababu za kikatiba kama zilivyoanishwa katika Ibara ya 71-(1)(a) mpaka (g),idadi ya wabunge walioteuliwa na Raisi itapungua au itabaki vile vile?

Tusaidiane hapa.
 
Nilitaka kuleta swali hili.
Baada ya kufikiri nimepata jibu hili..
Kama mbunge wa kuchaguliwa na wananchi akijiuzulu kuna hesabika kuna pengo na uchaguzi kupigwa upya basi hata ubunge wa kuteuliwa akijiuzulu ni pengo na anapaswa kuteuliwa mwingine.

Nahisi hata mbunge wa viti maalum nae akifariki chama hupeleka mwingine.
Hivyo idadi inapungua.
 
Mnajihangaisha bure,serikali haishindwi kitu,.watu wameshakaa na kuumiza vichwa.Mbunge akiandika barua ya kujiuzuru nafasi yake inabaki wazi.. Kama wa kuteuliwa anateuliwa mwingine nafasi yake,kama ni wa kuchaguliwa jimboni unaitishwa uchaguzi,kama viti maalum,anapachikwa mwingine.Kumbuka wabunge wote wana haki sawa,haijarishi kachaguliwa au kateuliwa.
 
Hiyo umiza kichwa ilifanyika baada ya kutenda madudu au?
 
Back
Top Bottom