Tujadili, vibigo wapigwao wadada. je ni chachu ya mapenzi

Tujadili, vibigo wapigwao wadada. je ni chachu ya mapenzi

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Nimeliona sana hili. Wanakuja wanalia, ukiwauliza kwa nini. Boyfreind wangu kanipiga, siku nyingine tena hivyo hivyo. Huwa najiuliza kwa nini huwa wanaendelea na mahusiano. Nyinyi wadada kwa nini mnaendelea kwenye mahusiano ambayo kupata vipigo ni sehemu ya kawaida kwenu.

Naombeni uzoefu kidogo, jana usiku nilikuwa kwenye kituo Fulani cha Polisi hapa Dar. Jamaa alimdunda mpenzi wake ikambidi yule dada akodi pikipiki akimbilie polisi, jamaa yake pia akawa amekodi pikipiki kumkimbiza. Yule dada anakaribia kufika polisi jamaa yake akawa amemuwahi kwa mbele. Dada akawa analia huku akiwa analalamika amepigwa
sana na mpenzi wake huyo. Polisi wakamweka jamaa ndani. Leo asubuhi nimefika pale kituoni kwa mambo yangu, nikamkuta yule dada kadamka mapema yupo pale polisi anamuombea msamaha mpenzi wake atoke. Kama mjuavyo, Polisi kuingia bure kutoka kwa rupia. Mdada kawapooza mandata, jamaa katoka wakaondoka.

Kitu ambacho ningependa kufahamu, je kuna aina ya mapenzi bila kipigo ayaendi? je wadada kitendo cha kupigwa ni ufahari? je kipigo wanachokipata ndicho uwafanya kushidwa kusema hapana?

Any contribution and experience are welcome
 
hivi hao wanaume wanaowapiga wanawaokotaga wapi!!!
 
Mapenzi bila kipigo yanaenda kinachowaponza ni huruma waliyonayo wadada jamaa likilala lupango au likija linasema nisamehe baaasi huruma mpaka machozi jamani!tofauti na wanaume.
 
Tumetofautiana, binafsi mwanaume akinipiga naona kwanza amenidharilisha mi ni mtu mzima kama nikikosea anatakiwa aniambie nitaelewa pia akinipiga naona hanipendi ndio maana anafurahi anaponiumiza kwa vipigo so mtu wa aina hiyo nitaachana naye mara moja.
 
kuwapiga vibao hiyo sawa inaleta heshima kwa mwanaume la sivyo atakupanda kichwani. kuwapiga ngumi mateke kichwa hiyo hapana.
 
Duh hivi baunsa kama mimi nikimpiga mwanamke si ntamuumiza sana. Hii nadhani ni malezi. Kama hukuona baba yako akimpiga mama yako, kwa nini umpige mtoto/dada wa watu?
 
Husninyo
Re: Tujadili, vibigo wapigwao wadada. je ni chachu ya mapenzi
hivi hao wanaume wanaowapiga wanawaokotaga wapi!!!


JE UMESAHAU KUWA KUNA KABILA AMBALO WANAWAKE BILA KUPIGWA WANAONA KAMA HAWAPENDWI?​
 
Inategemea pengne wamezoea maisha hayo ya kupiga/gwa.na ndo maana wanarudiana.
 
kwamtoro, nimeshangaa kumbe bado tabia za kupigana bado zipo! Huwa nashangaa zaidi mwanaume anaposhindwa kutumia mdomo wake na mamlaka yake ndani ya nyumba kuimanage familia yake mpaka anafikia hatua ya kumpigia mkewe/mpenzi. Kitendo cha kumpiga mke/mpenzi ni udhaifu wa mwanaume kushindwa kuhimili mikiki ya nyumba yake mwenyewe na hivyo kutumia mabavu kama njia ya kujinga na kujilinda baada ya kuzidiwa na mkewe/mpenzi.

Tukirudi kwenye mada yako:
Binafsi siamini kama ukimpiga mtu anaweza kuleta mapenzi ndani ya nyumba. Kwa uelewa wangu, kipigo huwa kinamuumiza mtu kimwili, na saa nyingine pia kudisturba hata akili na moyo wake. Siamini kama kwa muktadha huu, kipigo kinaweza kumfanya mtu kumpenda mtu, na badala yake nafikiri kinaweza kupunguza mapenzi ndani ya nyumba.

Nalazimika kuamini kuwa wanawake wanaopigwa na kisha kurudi nyuma na kusamehe inawezekana wanafanya hivyo kwa sababu ya kubanwa na sheria za ndoa, mila, kukosa namna ya kuishi bila huyo mtu (kuwa tegemezi), kuhofia kuvunja ndoa/kuharibu familia, upendo uliopitiliza (ujinga wa kushindwa kutambua haki) nk.

Ila nafikiri wanaume tuna uwezo wa kutosha wa kuwa-control wadada, sidhani kama kuna uhitaji wa kutumia kipigo, kipigo ni dalili ya udhaifu na kushindwa kuimudu nyumba.
 
Last edited by a moderator:
Kumpiga Mwanamke ni kitu cha aibu sana kwa kweli. Sijui Unaanzia wapi lakini hata kama ni hasira zimekukaba ndio umpige? Then ukishampiga ndio umesolve hio tabia labda, kama kipigo kinakomesha tabia kwa mtu mzima, ngoja nikaongee na kova atembeze kichapo kwa wanaojiuza usiku, nadhani watakoma.

kwani kwa nguvu wanaume tuliojaliwa ni wapi sasa utampiga mwanamke? Then mwanaume umeenda shule mtaani wanaku-refer kama mpiga Mke? Utakuwa umepita shule kama josho bila shaka. There so many ways za kurekebisha mtu mzima and kipigo is the least expected tena sio as a means ya kurekebisha bali kutoa hasira kiuonevu.
 
Nangojea wale watu wa kanda maalum waje nione watoe maoni yao! Wakina chacha, mwara, mwita, ghati, nyankolema, wankuru!
 
kupiga si suluhu ya matatizo yenu kwenye mahusiano.

Mdomo una uwezo wa kufikisha ujumbe vema,inategemea na muud,uelewa,hekima,busara na malezi ya wawili hawa.


KUPIGA NI UDHAIFU MKUBWA,INAONYESHA NI JINSI GANI ULIVYOISHIWA HOJA NA UELEWA WA MIHEMKO YA DADAZETU.
 
Tumetofautiana, binafsi mwanaume akinipiga naona kwanza amenidharilisha mi ni mtu mzima kama nikikosea anatakiwa aniambie nitaelewa pia akinipiga naona hanipendi ndio maana anafurahi anaponiumiza kwa vipigo so mtu wa aina hiyo nitaachana naye mara moja.
Shosti samahani, wewe ni kabila gani? Sisi kwetu hakuna kipondo hakuna mapenzi.
 
Duh hivi baunsa kama mimi nikimpiga mwanamke si ntamuumiza sana. Hii nadhani ni malezi. Kama hukuona baba yako akimpiga mama yako, kwa nini umpige mtoto/dada wa watu?[/QUO Commanche, hata kama uliona. Does it mean it was right and therefore you are emulating your dad. Come on!!
 
Last edited by a moderator:
huo ni mtazamo[ uliojijengea na upo kisaikolojia zaidiQUOTE=Binti.com;7414283]Pole agwe, kama hao waume zenu hawakumbuki "kuwapapasa" angalao mara moja moja basi hawawapendi![/QUOTE]
 
Boyfriend na Girlfriend ni maneno ya kishetani-kwa MUNGU kuna mchumba ni nadra sana kusikia mchumba amempiga mchumba wake na kufukuzana hadi polisi kwa style hii uliyoisimulia. Girlfriend na Boyfriend ni ushetani ndio maana kugombana na kupigana kupo waziwazi na hata rushwa kama hii uliyoisema kwa mandata anaona kitu cha kawaida. Mapenzi bila kipigo yapo, na hakuna mdada aliye na akili timamu anayependa kupigwa, bali wanapenda kupendwa na jukumu lao kuu ni kutii.
Nimeliona sana hili. Wanakuja wanalia, ukiwauliza kwa nini. Boyfreind wangu kanipiga, siku nyingine tena hivyo hivyo. Huwa najiuliza kwa nini huwa wanaendelea na mahusiano. Nyinyi wadada kwa nini mnaendelea kwenye mahusiano ambayo kupata vipigo ni sehemu ya kawaida kwenu.

Naombeni uzoefu kidogo, jana usiku nilikuwa kwenye kituo Fulani cha Polisi hapa Dar. Jamaa alimdunda mpenzi wake ikambidi yule dada akodi pikipiki akimbilie polisi, jamaa yake pia akawa amekodi pikipiki kumkimbiza. Yule dada anakaribia kufika polisi jamaa yake akawa amemuwahi kwa mbele. Dada akawa analia huku akiwa analalamika amepigwa
sana na mpenzi wake huyo. Polisi wakamweka jamaa ndani. Leo asubuhi nimefika pale kituoni kwa mambo yangu, nikamkuta yule dada kadamka mapema yupo pale polisi anamuombea msamaha mpenzi wake atoke. Kama mjuavyo, Polisi kuingia bure kutoka kwa rupia. Mdada kawapooza mandata, jamaa katoka wakaondoka.

Kitu ambacho ningependa kufahamu, je kuna aina ya mapenzi bila kipigo ayaendi? je wadada kitendo cha kupigwa ni ufahari? je kipigo wanachokipata ndicho uwafanya kushidwa kusema hapana?

Any contribution and experience are welcome
 
Ukweli ni kuwa sipendi kupigwa;
Kupigwa ni unyanyasaji na udhalilishaji wa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom